Tuliopanga Uswahilini tuna vituko na maswahibu mengi, tuambiane hapa

Kati ya mambo yanayofurahisha uswahilini hasa kwenye nyumba za kupanga ni tabia ya kuazimana hata visivyoazimwa..
1. Mtu anasonga ugali huko kwake anakuja kwako na bakuli umuazime mboga!
2. Mtu ana TV ila deki hana, anaenda kuazima muvi kisha anakuja kuazima deki. Na akichukua harudishi hadi uifate
3. Ukiwa na friji utahifadhi nyama, maziwa, samaki, wa nyumba nzima
4. Jirani akipata wageni, wengine anakuja kuwaombea walale kwako..
5. Ratiba ya usafi
Teh teh teh!! Doh!! Hatari
 
Tumeshafika bwana .

Vipi nyie mnaishi wapi?

Suala la umeme kwenye nyumba yenye watu wengi ni kero.

Dukuduku langu : kuna Tabia imezuka hapa JF watu hawaandiki mada kwa aya. Na nyingi hazivutii kusoma. Unakuta mada ina aya moja au mbili na hizo aya zina mistari 20 au 18. Aya ikizidi mistari iwe 8. Tunachoshana mazee.
Kama unachoka acha kusoma hujalazimishwa
 
Mtu kazoea kuchangia buku tu ya umeme na inamtosha kwa mda anaoutaka so kisa umehamia na mijagi na mi pasi na mazagazaga kibao eti akuige nayeye anunue!! we kama uko freshi mfukon jiwekee sub-meter yako iwe inakuhesabia unit zako uone mziki,kutaka jirani aliyekonda anenepe kama wewe ni sawa na kumlazimisha mwenye kitambi azae,maisha yana hatua,hatua ulionayo wengine hawajaifikia so kama kweli we ni wa level hiyo basi lipa kwa levo yako bn
 
Changamoto kubwa ni umeme, kauzima vitu na kuna watu hawarudishi kabisa. Ila hapa ndo utagundua kuna tatizo kubwa sana la elimu yetu hivi wasomi wa umeme na computer wanashindwa kuona fursa hii ya kutengeza portable luku mita kwa mpangaji. Mfano mtu anakuwa na mita yake kwa ajili ya chumba chake akihama anauwezo wa kuhama nayo.
 
Changamoto kubwa ni umeme, kauzima vitu na kuna watu hawarudishi kabisa. Ila hapa ndo utagundua kuna tatizo kubwa sana la elimu yetu hivi wasomi wa umeme na computer wanashindwa kuona fursa hii ya kutengeza portaple luku mita kwa mpangaji. Mfano mtu anakuwa na mita yake kwa ajili ya chumba chake akihama anauwezo wa kuhama nayo.
Zipo bana,mi nyumba nnayoishi mzee mkubwa kaweka sub-meter kila mtu analipa kulingana na matumizi yake,tena ni raha sana yani,nikichangia buku 5 utasikia wananisema tu kimyakimya, "LIMECHAKACHUA METER"
 
hahahahahahaha lol! Kumbe we mtundu eeh!

Duku duku langu kubwa ni kelele za mziki, kuna huyu mmoja nakaa naye chumba cha pembeni alikuwa anapiga muziki mpaka hatusikilizani, kila tukimwambia anajifanya kutuambia eti hatuna redio ya muziki mkubwa.

Nilimtegeshea siku moja wamekuja ndugu zake nikaweka CD ya mambo yetu yale ya jukwaa la chini kabisa, nikaongeza sauti nikafunga mlango nikaondoka zangu, nimerudi baada kama ya masaa manne nikafungua mlango nikaingia kwangu, toka siku hiyo sijasikia tena mziki wa sauti ile.
 
Sasa mimi natumia taa tu tena hasa siku zingine situmii kabisa umeme maana nipo kwenye kazi ya ukolokoloni huko ushuani.Eti unataka tulipe bili sawa ya umeme wakati wewe kama haupo basi yupo mkeo na watoto mnatumia friji,pasi,hita,rice cooker,tu,radio,feni,grenda halafu unataka tulipe bili sawa huoni kuwa huo ni wizi.Eti unasema kuwa tulipe sawa kwani nani kakuzuia wewe usinunue yaani unajifanya kupingana na sera ya kuwa lipa kadri unavyotumia. Yaani mimi nifanye ukolokoloni huko ushuani nije kukulipia bili ya umeme wewe? Nenda kakae na washua wenzako siyo kutuibia wanyonge. safari hii silipi umeme na mwenye nyumba kasema atanikatia umeme mimi nasema poa tu nitanunu solar ya elfu kumi maisha yanakwenda.
 
uswazi mpaka watoto wamehamia digitali
hqdefault.jpg

ma beki 3 nao hata hawaeleweki
New+Picture+(10).png

masela nao harakati kibao yani
Image+2.jpg
IMG-20140821-WA0002.jpg

paka wa huku uswazi wanafunua mpaka masufuria na kuipua kabisa walie chini kikiwa kimepoa
10393759_820747051307687_6890417375921913198_n.jpg

ukileta utata tunakudhibiti kwasababu utata tunatatua..
1006136_488721117862958_1940143674_n.jpg
11340197__6d8b11bf780675635a76d19317a4a4a5.jpg

BILA KUSAHAU CHAKULA CHETU NI UGALI SANA
trt.PNG
 
Umeme ulikuwa unaisha tarehe 15 sasa,mpaka kuipata tarehe 1 ulikuwa mziki.Yaani hiyo tarehe 15 unatoa 20k na wapangaji zaidi ya 6.Hii ndiyo ilinifanya nihamie sehemu nyingine angalau kidogo suala la umeme na maji,umbea mbea hakuna tena
 
Tupo mubashara kabisa yaan huku uswazi kwetu kibok kabisa yaan wapangaji mpk wanasusa hawanunui umeme muda mwengine tunakaa siku tatu na giza tunashindan kununua umeme
Kuna jamaa yangu anasema ubishi wa nani anunue umeme ulimshinda. Kichekesho sasa akirudi mida ya saa moja jioni umeme hamna anakuta wapangaji wenzie wamekaa nje wanapiga stori kwasababu ndani joto na umeme hamna. Basi ananunua umeme akiweka tu kila mtu anaingia ndani mara itv mara star tv huku singeli!
 
Changamoto za uswazi ni:
Maji
Umeme
Usafi wa choo na bafu kama mnachangia
Usafi wa uwanja
Umbea kibarazani kwa wanawake
Kuchunguzana maisha
Kucbunguza wageni hasa kwa sisi tusiooa

Kero ni nyingi, kwa ufupi, sio mahali salama pa kuishi
 
Back
Top Bottom