Tuliohamia makwetu 2024 kabla hata ujenzi hujaisha tukutane hapa kutiana moyo na kupeana changamoto

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,368
50,739
Uzi maalumu kwa wale baba wenye nyumba walioamua 2024 liwalo na liwe wamefanikiwa kuhamia kwao na maisha yanasonga na hawalipi tena kodi bali wanaweza hata kugombea ujumbe wa nyumba 10 tukutane hapa.

Wengine shida maji wengine umeme na wengine usafiri.vp una solve ishu hizo kuzirahisha.mpewe maua yenu kwako kwako tu.
 
Unahamia kibishi ukidhani ndo utamalizia kumbe ndo mazima ndani ya kuta za mbavu za mbwa, vumbi, mijuzi, hakuna paa joto la bati kama loote, hakuna milango ni frame ya gate umejazia makaratasi, n.k, kwa ufupi ni shida mpaka unatamani ungeendelea kupanga
 
Kabisa. Baada ya pagale langu kukaa bila kupauliwa kwa miaka 3 mwezi uliopita nimefanikiwa kupaua.

Sasa wife ana force tuhamie eti madirisha tuyapige mabati na tuweke milango ya grill. Sina hela ya umeme na system za maji. Nimegoma itachukua miaka 2 niweze kuhamia. Ujenzi kwa hela za kuunga unga ni balaa.
 
Uzi maalumu kwa wale baba wenye nyumba walioamua 2024 liwalo na liwe wamefanikiwa kuhamia kwao na maisha yanasonga na hawalipi tena kodi bali wanaweza hata kugombea ujumbe wa nyumba 10 tukutane hapa.

Wengine shida maji wengine umeme na wengine usafiri.vp una solve ishu hizo kuzirahisha.mpewe maua yenu kwako kwako tu.
Hongera zenu wakuu
 
Raha sana upo kwako choo self umesahau mambo ya kushare choo na wapangaji wenzako

Raha sana kujua kumbe mwanamke kukuchemshia maji ya kuoga na kukupelekea bafuni ni umaskini siyo heshima kwani maji unapaswa kuyakuta bafuni na unachagua uoge ya moto au maji ya baridi

Raha Sana kujua kumbe unaweza kununua umeme wa buku si lazima umeme wa elfu kumi mlizokuwa mnachangishana

Raha sana kujua kumbe Bill ya maji unaweza kukaa miezi mitatu bila kulipa na maji usikatiwe tofauti na nyumba ya kupanga lazima ulipe kila mwezi
 
31/122023 ndio siku nimeingia mpaka sasa burudani tele nimeweza kupiga plasta vyomba vyote
 
Back
Top Bottom