Tukimtazama Rais Magufuli katika maono ya Mwalimu Nyerere: Je, wanyonge tungejibu nini?

Oct 6, 2020
27
50
Mwasisi wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika uhai wake alitoa hotuba nyingi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, ndani na nje ya nchi. Moja ya hotuba zilizovuta hisia za Watanzania wengi ni ile aliyoitoa katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi mnamo mwaka 1995 wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mambo yote aliyoyasema katika hotuba yake yanaakisi taswira ya jamii yetu leo hii.

Lengo la makala haya ni kukusafirisha kumpima Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, tuone kama angesimama wakati huo na kama anavyosimama sasa, ungeulizwa maswali haya na Mwalimu Nyerere ungejibuje.

Akiwa mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Mwalimu aliwahutubia Watanzania kupitia mkutano huo wa kumchagua kiongozi akisisitiza kero kubwa nne ambazo Watanzania wanataka kiongozi atakayeteuliwa kuwania urais ayashughulikie. Mwalimu alitaka mgombea atakayeteuliwa aweke mifumo imara ya kuondokana na rushwa nchini, ashughulike na kero za Watanzania akitambua kwamba asilimia kubwa ya Watanzania ni maskini, aondoe dhana ya udini, na mwisho asikumbatie ukabila.

Tukianza na kero ya Kwanza, Mwalimu Nyerere aliwataka wajumbe wamchague mgombea ambaye atapambana na rushwa nchini. Nikinukuu maneno yake,Mwalimu alisema “Watanzania wamechoka na rushwa” akitoa rai mbele ya wajumbewamchague mgombea atakayesaidia kupambana na rushwa nchini. Tunayo kila sababu ya kuangalia jinsi Rais Magufuli alivyopambana na kero hii ambayo ni adui mkubwa wa haki za Watanzania, hasa wanyonge.

Je, Rais Magufuli ameitikiaje rai hii ya Mwalimu Nyerere katika juhudi za kupambana na rushwa nchini kwa miaka mitano ya uongozi wake? Tunatambua kwamba rushwa huanzia katika ngazi ya chama cha siasa, na mwanasiasa anapokamata dola basi rushwa ileile inahamia katika mfumo wa dola. Rais Magufuli alipokea uenyekiti wa CCM mwaka 2016. Akiwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli amekiwekea misingi imara na bora ya kupambana na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vimekithiri ndani ya Chama.

RaisMagufuli ameondoa dhana ya ‘ushindi wa pesa’ kwa wagombea wanaowania ngazi mbalimbali za kukiwakilisha chama ndani ya serikali. Dhana hii iyolikuwa imekithiri ndani ya Chama ilisababisha Chama kupata asilimia kubwa ya wawakilishi ndani ya serikali ambao ni wala rushwa na wabadhirifu. Rais Magufuli ameondoa dhana na fikra hii kwa vitendo. Kwa mfano, mchakato wa kuwapata wabunge ulikuwa kwa asilimia kubwa unaegemea ni mtia nia yupi ametoa pesa nyingi hivyo kupigiwa kura nyingi za maoni na wajumbe katika ngazi ya husika.

Utaratibu huu uliwanyima Watanzania wengi wasiokuwa na pesa fursa ya kuwa viongozi kama madiwani na wabunge. Kupambana na hali hii sasa, Rais Magufuli ameimarisha Chama nakujenga CCM ile aliyoisema Mwalimu Nyerere kama ‘CCM Madhubuti’ kwambatunapata viongozi ambao sio matokeo ya nguvu ya rushwa. Ni viongozi hawahawa wasio wala rushwa watakaokamata madaraka makubwa serikalini na kutambua kwamba haki ya Mtanzania mnyonge inakuwa kipaumbele kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akifanya siku zote.

Vivyo hivyo, ndani ya serikali Rais Magufuli ameelekeza juhudi kubwa kupambana na adui rushwa, uhujumu uchumi na ufisadi. Kwa mfano, mwaka mmoja tu baada ya kuingia madarakani Rais Magufuli alianzisha Mahakama ya Uhujumu Uchumi ambayo mpaka sasa imepokea mashauri 407, ambapo mashauri 385 tayari yamesikilizwa.

Nyerere+pic-2.jpg

Vilevile kupitia TAKUKURU serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 273.38, zikiwemo fedha walizokuwa wamedhulumiwa wakulima. Kama hiyo haitoshi, tumeshuhudia viongozi na watanzania wala rushwa, wahujumu uchumi na wabadhirifu wakichukuliwa hatua za kisheria bila kujali uwezo wao wa kifedha. Mifumo hii ya kupambana na rushwa ni matokeo ya kuwa na Rais ambaye alitambua kwamba rushwa ni adui wa haki, na Mtanzania hasa mnyonge ni muathirika namba moja wa matokeo ya rushwa. Kwa kuzingatia juhudi hizi za dhati na maksudi alizoziweka Rais Magufuli kupambana na rushwa, turejee katika swali alilouliza Mwalimu Nyererekatika hotuba yake, “Huyu atatusaidia kupiga rushwa vita?”. Kwa kumtazama usoni kwa dhati ya moyo wako wewe Mtanzania mnyonge ungejibu nini?

Licha ya rushwa, Mwalimu Nyerere vilevile alisisitiza kwamba Tanzania inahitaji kiongozi ambaye anatambua kwamba Tanzania ni nchi ya maskini, hivyo nguvu na juhudi zinatakiwa zielekezwe katika ustawi wa afya, elimu, kilimo, biashara kwa Watanzania hawa wanyonge. Serikali ya Rais Magufuli imeelekeleza juhudi zake katika kuboresha maisha ya Mtanzania hasa mnyonge kwa asilimia kubwa. Tukianza na elimu, Rais Magufuli amemuona Mtanzania maskini na kuamua kumpa elimu ya sekondari bila malipo. Kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, serikali ya Rais Magufuli imewapa kipaumbele cha kupewa mkopo watoto wa maskini na yatima, hivyo kuleta usawa na haki ya kupata elimu kati ya masikini na tajiri.

Kuhusu afya, tunatambua kwamba vituo vya kutolea huduma za afya nchini vilikuwa vichache kulingana na uhitaji wa wagonjwa, hali iliyosababisha vifo hasa kwa mama wajawazito, vichanga, na wazee. Hivyo, miaka mitano ya serikali ya Rais Magufuli ilielekeza nguvu na juhudi kubwa kuhakikisha inaokoa maisha ya mama wajawazito, wazee, na vichanga waliyokuwa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za afya kwa kuwasogezea zahanati na hospitali karibu. Hata hivyo, serikali ya Rais Magufuli imemuwezesha Mtanzania maskini, na asiyekuwa katika sekta rasmi ya ajira kupata huduma za afya kwa kumpatia kadi ya kupatiwa matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa gharama rafiki.

Ikumbukwe kwamba biashara ya kutembeza bidhaa alimaarufu kama umachingailighubikwa na sintofahamu na kuwafanya vijana, akina mama kufanya biashara zao katika mazingira magumu ya kufukuzana na askari mijini. Kwa muda hali zao za kiuchumi zilikuwa duni. Kwa kutambua hali duni waliyokuwa nayo, na kwa kutambua kwamba hizo ndizo shughuli zinazowaletea kipato ili waweze kula na kutunza familia zao, Rais Magufuli aliamua kuwaondoshea wafanya biashara hawa wadogo kadhia hii kwa kurasimisha biashara zao na hivyo kuwafanya wafanye biashara zao popote bila usumbufu wowote.

Ushuru wa bidhaa ilikuwa kadhia nyingine iliyokuwa ikimkwamisha Mtanzania maskini. Mfano, mwananchi huyu analima anasafirisha mahindi chini ya tani moja kutoka shambani kijijini kwenda sokoni mjini kwa ajili ya kuyauza ilia pate kipato cha kuendesha familia yake. Awali Mtanzania huyu mnyonge alikuwa analazimika kulipia ushuru mzigo huu wenye uzito chini ya tani moja, na hivyo kumpunguzia faida katika mauzo yake. Rais Magufuli kwa kutambua kwamba Mtanzania huyu anahitaji kukuza kipato chake kwa manufaa yake na familia yake, akaamua kumuondolea ushuru wakati akisafirisha mzigo wake usiozidi tani moja kutoka shambani kwenda sokoni.

Katika mwendelezo huohuo, tumemuona Rais Magufuli mwenyewe na wateule wake kwa nyakati tofauti tofauti wakisikiliza na kutatua kero za wananchi moja kwa moja mashambani, hospitalini, shuleni, maeneo ya biashara nakadhalika.

Naam, kwa kuzingatia juhudi zote hizi, leo hii turejee rai aliyotoa Mwalimu Nyerere“…tunamtaka Rais atakayeshughulika na matatizo ya wananchi maskini” kwakuangalia hali zao za hospitalini, mashuleni, mashambani viwandani.” Kwa kuzingatia juhudi hizi za Rais Magufuli kwa miaka mitano, wewe Mtanzania ungelijibuje swali la Mwalimu Nyerere kuhusu uthubutu imara wa Rais Magufuli kuboresha maisha ya Watanzania hasa wanyonge?

Kero ya Tatu na Nne aliyoisema Mwalimu Nyerere ni Udini na Ukabila. Rais Magufuli anamaliza kipindi chake cha miaka mitano bila kuwepo na makundi ya udini wala ukabila. Kipimo kizuri cha kiongozi ni kuwaleta Watanzania pamoja, kuimarisha udugu na umoja na matokeo yake ni ustawi wa jamii imara. Chini ya uongozi thabiti wa Rais Magufuli muungano umelindwa na kudumishwa; Chini ya uongozi imara wa Rais Magufuli Watanzania hatuna ubaguzi wa kidini; Chini ya uongozi madhubuti wa Rais Magufuli hakuna machafuko yoyote ya kikabila, badala yake kumekuwa na kabila moja ambalo Rais Magufuli amekuwa akilisimamia na kuliongoza imara ambalo ni kabila la Watanzania.

Uimara huu ni matokeo ya kuwa na kiongozi asiyeendekeza udini wala ukabila katika utendaji wake. Katika majukwaa mbalimbali Rais Magufuli amekuwa akiwataka Watanzania kuwa wamoja,na kauli yake maarufu ni kwamba “Maendeleo hayana chama, dini, wala kabila.”Anatambua kwamba nchi ikishatumbukia katika udini na ukabila, basi hapatakuwa na Tanzania ya Watanzania hivyo kwa kauli yake hii Watanzania wamekuwa wamoja na ni umoja huu uliyowafanya Watanzania kwa pamoja kuwa na amani na kufanya kazi kwa bidi na kuipaisha Tanzania katika kiwango cha Uchumi wa Kati.

Juu ya hili, wewe Mtanzania mnyonge ungeulizwa leo na mwalimu Nyerere, “Je huyu anajua kwamba nchi yetu haina udini wala ukabila?”, ungejibuje?

Kwa kuitimisha makala haya, turejee katika hitimisho aliyoitoa Mwalimu Nyerere. Mwalimu Nyerere alisema “Tunataka nchi yetu ipate kiongozi safi; Kiongozi safi hawezi kutoka nje ya CCM, ninyi wapiga kura [wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM] mnaweza kutupatia kiongozi safi, sasa tupatieni kiongozi safi!” Julai 11, 2020 wajumbe wa Mkutano Muu wa CCM Taifa waliitika wito huu wa Mwalimu Nyerere kwa kumpitisha Rais Magufuli kwa ushindi wa kishindo kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mingine mitano, 2020–2025.

Rais Magufuli alipitishwa tena kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu alikwishaonyesha kwa vitendo juhudi zake za kupambana na rushwa, alikwishaonyesha kwa vitendo juhudi za kumuinua Mtanzania hasa mnyonge kiuchumi, alikwishaonyesha kwa vitendo kulinda ustawi wa Tanzania isiyo na udini na ukabila, amekwishaonyesha kwa vitendo namna kaulimbiu yake ya “Hapa Kazi Tu” ilivyowapa hamasa kubwa Watanzania kufanya kazi na hivyo juhudi hizi kuzaa matunda ya kuipaisha Tanzania katika uchumi wa kati. Oktoba 28, 2020 ni zamu yako Mtanzania mzalendo na mpenda maendeleo kumpitisha Rais Magufuli ili aendeleze juhudi hizi na maisha yako yazidi kuboreshwa kwa manufaa yako, familia yako, jamii inayokuzunguka, na taifa kwa ujumla.
 
Rais wetu mpendwa Dr JPM amemuishi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Vitendo, Yale Maono ya Baba wa Taifa ameyaishi yoote Anza na serikali kuhamia Dodoma, Ujenzi wa Mradi mtakatifu wa Bwawa la Umeme Rufiji, JuliusNyererePowerPlant aka Stigglers gorge, Ujenzi wa Miundombinu kambambe Ili kuwaokoa Wanyonge na adha ya usafirishaji, Ujenzi wa Vituo Vya Afya kuondoa Maradhi kwa nguvu Kazi na hilo Baba wa Taifa alilisema sana, pia la ujinga Elimu Ni Bure ya Msingi Mpaka sekondari na Kubwa zaidi kaboresha maabara na kaweka wataalamu wa maabara wa sayansi nk nk Hivyo kwa kifupi Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli Amepita kwenye Maono ya Baba wa Taifa.
 
Rais wetu mpendwa Dr JPM amemuishi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Vitendo, Yale Maono ya Baba wa Taifa ameyaishi yoote Anza na serikali kuhamia Dodoma, Ujenzi wa Mradi mtakatifu wa Bwawa la Umeme Rufiji, JuliusNyererePowerPlant aka Stigglers gorge, Ujenzi wa Miundombinu kambambe Ili kuwaokoa Wanyonge na adha ya usafirishaji, Ujenzi wa Vituo Vya Afya kuondoa Maradhi kwa nguvu Kazi na hilo Baba wa Taifa alilisema sana, pia la ujinga Elimu Ni Bure ya Msingi Mpaka sekondari na Kubwa zaidi kaboresha maabara na kaweka wataalamu wa maabara wa sayansi nk nk Hivyo kwa kifupi Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli Amepita kwenye Maono ya Baba wa Taifa.View attachment 1593608
kuna mtu hua anatoa hela yake kununua hilo gazeti?
 
Acha kudanganya umma.Hakuna kiongozi ambae amefanya ufisadi mkubwa pamoja na rushwa kubwa kwenye nchi hii kama Magufuli.Ufisadi wa 1.5 trillion hautasahaulika kamwe,ufisadi wa Mayanga contractors,ufisadi wa kununua ndege bila budget kupita bungeni achilia mbali ufisadi wa kujenga miradi mbalimbali mikubwa bila budget kupita bungeni.

5430210.jpg
 
Bandiko ni refu sana sijalisoma. Natoa maoni yangu kufuatana na Kichwa cha habari nilivyokielewa.

Hakuna mlinganisho wowote unaoweza ukautumia kati ya Magufuli na Mwalimu, ni watu wawili tofauti kabisa karibu kwa kila kitu.

Hilo la wanyonge, mmoja alizungumzia waTanzania kwa ujumla wao ambao hali zao zilikuwa duni sana, mwingine anazungumzia 'wanyonge' anaotaka wamsifu na wasihoji lolote analofanya kwa wale wanyonge wanaojaribu kuhoji anayofanya kwa kisingizio cha kuyafanya kwa niaba yao.

Kwa kifupi tu hii ni tofauti inayowatenganisha hao viongozi wawili.
 
Hakuna Rais ambae ni mkabila,mdini na ambae amewagawa watanzania kuwahi kutokea Tanzania kuliko Magufuli:

1. Mashee wa uamsho wapo ndani bila kufunguliwa kesi yoyote kwa sababu ya dini yao ya uislam

2. Magufuli amekuwa akiongea kisukuma sehemu mbalimbali anazopita akijaribu kuonyesha kuwa kabila la kisukuma ni superior jambo ambalo hata sheria za tume ya uchaguzi zinakataza

3.Magufuli amekuwa akiwagawa watanzania kutokana na vyama vyao.Amekuwa akisema kuwa msiponiletea mbunge hapa sileti maji
 
Akiwa mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Mwalimu aliwahutubia Watanzania kupitia mkutano huo wa kumchagua kiongozi akisisitiza kero kubwa nne ambazo Watanzania wanataka kiongozi atakayeteuliwa kuwania urais ayashughulikie. Mwalimu alitaka mgombea atakayeteuliwa aweke mifumo imara ya kuondokana na rushwa nchini, ashughulike na kero za Watanzania akitambua kwamba asilimia kubwa ya Watanzania ni maskini, aondoe dhana ya udini, na mwisho asikumbatie ukabila.
Sasa nimekusoma hadi hapa.

Aya hii ni muhimu sana kwenye hotuba hiyo. Hakuna sehemu hotuba hii ya Mwalimu ilipoelezea kwamba wakati haya yanafanyika kwa maslahi ya nchi, uhuru na haki za wananchi ziwekwe pembeni. Haya yote yaliwezekana kufanyika bila kukanyaga na kunyanyasa watu. Hapakuwa na sababu yoyote iliyopelekea hayo mabaya yafanyike huku hayo mavitu mazuri yakifanyika.

Mazuri yote yangefanyika ndani ya taratibu zilizowekwa, bila kukiuka taratibu zozote. Sheria zimetungwa kutuongoza sote, kama hazifai zingeweza kurekebishwa kupitia bungeni.

Kosa kubwa ni hilo la mtu mmoja kujidhani kwamba yeye yupo juu ya sheria zilizopo. Mwalimu hakufanya hivyo.
 
Bandiko ni refu sana sijalisoma. Natoa maoni yangu kufuatana na Kichwa cha habari nilivyokielewa.

Hakuna mlinganisho wowote unaoweza ukautumia kati ya Magufuli na Mwalimu, ni watu wawili tofauti kabisa karibu kwa kila kitu.

Hilo la wanyonge, mmoja alizungumzia waTanzania kwa ujumla wao ambao hali zao zilikuwa duni sana, mwingine anazungumzia 'wanyonge' anaotaka wamsifu na wasihoji lolote analofanya kwa wale wanyonge wanaojaribu kuhoji anayofanya kwa kisingizio cha kuyafanya kwa niaba yao.

Kwa kifupi tu hii ni tofauti inayowatenganisha hao viongozi wawili.
Mwalimu alikuwa mtu wa dunia nzima. Mpigania uhuru na haki dunia nzima. Mwanafalsafa. Je, huyu wa sasa ni wa eneo hilohilo, ni mwanafalsafa? Je, ni mpigania haki sawasawa na Mwalimu?

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu afya, tunatambua kwamba vituo vya kutolea huduma za afya nchini vilikuwa vichache kulingana na uhitaji wa wagonjwa, hali iliyosababisha vifo hasa kwa mama wajawazito, vichanga, na wazee. Hivyo, miaka mitano ya serikali ya Rais Magufuli ilielekeza nguvu na juhudi kubwa kuhakikisha inaokoa maisha ya mama wajawazito, wazee, na vichanga waliyokuwa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za afya kwa kuwasogezea zahanati na hospitali karibu. Hata hivyo, serikali ya Rais Magufuli imemuwezesha Mtanzania maskini, na asiyekuwa katika sekta rasmi ya ajira kupata huduma za afya kwa kumpatia kadi ya kupatiwa matibabu kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa gharama rafiki.
Uandishi wako ni wa kishabiki.

Huduma zote unazoziandika humu ni kama huko nyuma kabla ya Magufuli hazikuwepo?

Mtu mwenye kujitambua anaposoma andiko kama hili anadharau kila kitu kilichomo ndani yake.

Mwinyi, Mkapa, na hasa Mkapa. Kikwete wote hawa walifanya vizuri katika hiyo miundombinu na huduma. Kuna yaliyowashinda, hasa Kikwete juu ya huo ufisadi.

Unapofanya uchambuzi, chambua mambo ya kipekee aliyofanya huyo unayemchambua, na usipende kuegemea alipodandia kwa watangulizi wake.

Na kwa huyu nitakubaliana nawe juu ya Dodoma, Stiegler's, ufisadi na urasimu maofisini. Sioni zaidi ya hapo.

Lakini katika upande wa pili, usiokuwa mzuri, ambao Mwalimu pia angeukemea, orodha ni ndefu na ni ya kusikitisha.
 
Mwalimu alikuwa mtu wa dunia nzima. Mpigania uhuru na haki dunia nzima. Mwanafalsafa. Je, huyu wa sasa ni wa eneo hilohilo, ni mwanafalsafa? Je, ni mpigania haki sawasawa na Mwalimu?


Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Huwa nakereka sana, ninapoona mtu anamfananisha JPM na JKN. Ni mbali sana! Ni matusi makubwa sana kwa MTAKATIFU MTARAJIWA!
 
Mwl. Nyerere aliwahi kujenga uwanja wa Ndege wa kimataifa kijijini kwake?
Kama mnakumbuka aliyewahi Kuwa waziri wa ujenzi, (kama sikosei alikuwa Hayati Lusinde) aliwahi kusema kuwa, yeye ndiye aliyemhamisha Mwalimu kutoka Msasani, na kuhamia Ikulu. Yaani, Mwalimu Ikulu ilikuwa kama ofisi tu. Analala nyumbani kwake Msasani, kazi anafanyia Ikulu.

Wakati huo, barabara ya kwenda huko Msasani ilikuwa mbovu, lakini Mwalimu hakutaka itengenezwe. Kisa, barabara nyingi ni mbovu, hivyo angeonekana ni m'binafsi.

Mwalimu, akaja kusafiri safari ndefu ughaibuni. Waziri kwa kihere here chake, akatuma greda kwenda kurekebisha hiyo barabara.
Mwalimu aliporudi na kuiona barabara ya kwenda nyumbani kwake imekwanguliwa, alikasirika sana, na kumgombeza Waziri. Akaamua kuihama nyumba hiyo na kuhamia Ikulu, eti wananchi watamuona anajipendelea.

Huyo ndiyo Mwalimu. Kajengewa nyumba nzuri Butiama, akawaambia mbona nyumba yake ya zamani inatosha tu!?
 
Acha kudanganya umma.Hakuna kiongozi ambae amefanya ufisadi mkubwa pamoja na rushwa kubwa kwenye nchi hii kama Magufuli.Ufisadi wa 1.5 trillion hautasahaulika kamwe,ufisadi wa Mayanga contractors,ufisadi wa kununua ndege bila budget kupita bungeni achilia mbali ufisadi wa kujenga miradi mbalimbali mikubwa bila budget kupita bungeni.View attachment 1593612
Mkuu tuwekee ushahidi vinginevyo ni majungu tu utakuwa unabweka kama bweha.
 
Kama mnakumbuka aliyewahi Kuwa waziri wa ujenzi, (kama sikosei alikuwa Hayati Lusinde) aliwahi kusema kuwa, yeye ndiye aliyemhamisha Mwalimu kutoka Msasani, na kuhamia Ikulu. Yaani, Mwalimu Ikulu ilikuwa kama ofisi tu. Analala nyumbani kwake Msasani, kazi anafanyia Ikulu.
Wakati huo, barabara ya kwenda huko Msasani ilikuwa mbovu, lakini Mwalimu hakutaka itengenezwe. Kisa, barabara nyingi ni mbovu, hivyo angeonekana ni m'binafsi.
Mwalimu, akaja kusafiri safari ndefu ughaibuni. Waziri kwa kihere here chake, akatuma greda kwenda kurekebisha hiyo barabara.
Mwalimu aliporudi na kuiona barabara ya kwenda nyumbani kwake imekwanguliwa, alikasirika sana, na kumgombeza Waziri. Akaamua kuihama nyumba hiyo na kuhamia Ikulu, eti wananchi watamuona anajipendelea.
Huyo ndiyo Mwalimu. Kajengewa nyumba nzuri Butiama, akawaambia mbona nyumba yake ya zamani inatosha tu!?
Aisee hebu ona sasa Maisha/itikadi hizo za Nyerere halafu linganisha na itikadi za huyu mzee baba,nadhani kuwafananisha hao watu wawili ni kujidanganya sisi wenyewe tu mkuu.
 
Back
Top Bottom