sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,256
Ni utamaduni unaonishangaza sana, kila ikifika december wiki 2 za mwisho Wachaga wa nje ya mikoa na nje ya nchi hukusanyika pamoja kwenye sehemu za asili zao huko Kilimanjaro.
Kwa miaka kadhaa nishazoea kuona status za wachaga watatu wanaoishi nje ya nchi wanapost status wamerudi, Yupo anaeishi China jiji la Guangzou, Marekani jiji la San Fransisco na mwengine Australia jiji la Sydney.
Kurudi kwa pamoja hukutanisha kila mwaka ndugu, majirani mpaka marafiki wa utotoni, kwa wale watoto waliozaliwa huku mijini ama nje ya nchi nao wanapelekwa kuijua mizizi yao, nadhani hata kama ulikopa duka la mangi mwaka jana basi hii December utadakwa tu.
Tukija huku makabila mengine ni nadra sana, achilia mbali kabila yani hata ndugu kurudi kwa pamoja kwenye mizizi yao ni suala zito, Labda itokee kuna msiba wa babu huko kijijini watazika na kutawanyika.
Binafsi upande wa baba ni mtu wa kanda ya ziwa, Yeye alikulia kijijini huwa anarudi kila mwaka lakini mimi nilienda mara 2 tu nikiwa darasa la sita na la saba shughuli ikaishia hapo !! kwakweli ni kipindi kirefu sana kimepita, connection za kijijini zimepotea kabisa hata watoto wakiulizia kijijini kwao nawaambia ni mtaa wa mjini niliozaliwa, naowahesabia ni ndugu ni wale tunaokutana mjini ila kule kwenye mizizi nishapoteza connection.
Nipo mikoa ya Iringa ya Mbeya kuna makabila kadhaa mambo ni hayo hayo tu, tukianza na Wanyakyusa wa Mbeya waliozaliwa nje ya sehemu za mizizi yao (Tukuyu ama Kyela) hawajazoeshwa kurudi kwenye mizizi yao hata undugu ni ule wa kujuana ndugu wa mjini. Ikitokea wamerudi huko kwao labda kuwe na mazishi, hali inakuwa mbaya zaidi kwa watoto wa hawa wanyakyusa waliozaliwa mijini wanaweza hata wasipajue Tukuyu.
Wengine nao ni wakinga wa huko Njombe wapo sana hio Iringa na Mbeya, watoto wanaishia kupajua mjini tu na ndugu wa mjini, Nina rafiki aliwahi kurudi kwenye msiba wa bibi yake tu tangu hapo hapajui Makete,