Tujikumbushe kidogo Dkt. Karl Peters na Mikataba ya Kilaghai

Zanaco

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,611
1,590
Jumamosi ya Novemba 15, 1884, Kansela wa Ujerumani, Otto von Bismarck, aliitisha mkutano mkubwa kwa ajili ya kuligawa Bara la Afrika. Mkutano huo uliofahamika kama Berlin Conference, ulifanyika kwenye makazi yake huko Wilhelmstrasse, Berlin.

Mkutano huo ulilenga katika kuwaepusha wababe wa Magharibi kutumbukia vitani wakati wakigombania mali za Afrika. Mataifa 14 yalihudhuria, wakiwemo Ujerumani wenyewe, Uingereza, Marekani (wakiwakilishwa na Henry Morton Stanley), Himaya ya Ottoman (Dola ya Mtukufu Sultan , Denmark, Ufaransa, Muungano wa Austria na Hungary, Urusi, Ureno, Hispania, Muungano wa Sweden na Norway, Ubelgiji, Italia na Uholanzi.

Mkutano huu ndio uliosababisha ukoloni barani Afrika, kwani uliazimia katika kuligawa bara hili miongoni mwa wababe waliohudhuria, kwa faida yao. Baada ya mkutano huo, mataifa hayo yakatuma wawakilishi wao kuja Afrika kuchukua maeneo na mali.

Ujerumani ikamtuma kijana wa miaka 28, aliyeitwa Karl Peters, akiwa na vijana wenzake watatu; Dk. Karl Juhlke, Pfeil na August Otto.
Vijana hawa wakafunga safari hadi Afrika na kutia nanga Zanzibar na baadaye kuanza safari ya bara hadi walipofika Usagara ambako walikutana na Chief Mangungo katika Ikulu yake ya Msovero. Usagara kwa sasa ndio Kilosa.

Karl Peters akatumia ujanja, hila na ulaghai kuingia mkataba na kiongozi huyo wa kiafrika uliosababisha Ujerumani kuchukua eneo lake lote pamoja na watu wake.

Mkataba huo uliandikwa kijerumani na Chief Mangungo akamtumia mkalimani wake kutoka hapo hapo Msovero (Ramazan) ambaye na yeye wala hakuijua lugha hiyo.

Mkataba huo ulisomeka kama ifuatavyo:

“Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani, kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.

Dk. Karl Peters, kwa niaba ya jina la Umoja wa Ukoloni wa Ujermani anatangaza dhamira yake ya kuitwaa himaya yote ya Sultan Mangungo na haki zote kwa ajili ya Koloni la Ujerumani inayohusisha kila kona na amali za Mwenyi Sagara.”

Baada ya mkataba huu, Karl Peters akalichukua eneo lote lililokuwa chini ya Mangungo na kuliweka chini ya kampuni yake ya Deutsch-Ostafrika (German East Africa) ambayo ilikuwa ikimiliki eneo lote ambalo leo hii ni Tanzania Bara na Rwanda na Burundi.

Wakati machifu wengine, kama Mkwawa, walipigana na Ujerumani kukataa maeneo yao kuchukuliwa, Mangungo alilitoa eneo lake kirahisi kabisa.

Hayo yalitokea mwaka 1884. Hayo yalitokea karne ya 19. Hayo yalitokea kwa sababu Mangungo hakusoma, hivyo asingeweza kufua dafu mbele ya msomi, Daktari wa Falsafa, Karl Peters.

Baada ya karne zijazo kuna ubaya gani na sisi tukisomwa kama hawa akina Ramazani?

Ebu wasanii badala ya kutengeza move za mapenzi tutengezee move ya zaku elimisha Jamii kama hii mtauza nitanunua copy mbili nimuone Ramazan akipiga fix na kumzunguka Chief.
 
Tofuati ni kwamba, kipindi hicho maeneno yalichukuliwa kibabe sana.

Awamu hii maeneno yanachukuliwa kiulaini kwa akili nyingi sana.
 
"if you Europeans are camellion a'm a fly which you can not catch" Chief Mangungo of Msovero
 
Walitawaliwa au hawakutawaliwa jibu swali acha habari za mbuni kuficha kichwa huku kinyeo kipo wazi we TAGA
Una mawazo mgando sana; unahangaika kushinda mjadala badala ya kchangia mawazo chanya. Mwenzio anazungumza kutawaliwa kwa kutumia mikataba yenye ulaghai lakini wewe unazungumza kutawaliwa kwa kushindwa vita.

Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa. Lile la kwanza la mikataba hata bleo linaweza kutumika wakati hilo la pili la vita halitumiki kirahisi tena katika dunia ya leo labda kwa Urusi na Crimea tu.
 
Walitawaliwa au hawakutawaliwa jibu swali acha habari za mbuni kuficha kichwa huku kinyeo kipo wazi we TAGA
Hoja ni usiri wa mikataba hawa wazee wetu kidogo shule zilikuwa bado kwanini bado tunafanya makosa yaleyale.
 
Wana heri hata peponi akina Chief Mangungo maana hawakujua kusoma wa kuandika Kijerumani. Leo wasomi wetu wamekabidhi kila kitu kwa Dola za Kigeni hadi usimamizi wa misitu yetu na bandari zetu. Kizazi chetu tutachomwa moto hadi tuchakae kwa kutioa rasilimali za wajukuu zetu kwa dola za kigeni hali tukijua kusoma na kuandika.
 
Chief
Walitawaliwa au hawakutawaliwa jibu swali acha habari za mbuni kuficha kichwa huku kinyeo kipo wazi we TAGA
Chief analaumiwa bure tu,wakati ulikiwa umefika hakukuwa na namna Hata Meneliki ii aliyekomaa na kudindda 1935 Ethiopia alikaliwa na Mussolini hadi 1941.Na leo wote tunaburuzwa na wazungu..There was nothing else Mangungo shuold have done.
 
Chief

Chief analaumiwa bure tu,wakati ulikiwa umefika hakukuwa na namna Hata Meneliki ii aliyekomaa na kudindda 1935 Ethiopia alikaliwa na Mussolini hadi 1941.Na leo wote tunaburuzwa na wazungu..There was nothing else Mangungo shuold have done.
Mangungo na wenzake walikubali kuikabidhi nchi kwa Karl Peters na Serikali ya Ujerumani walitusaidia sana. Leo Tanganyika ingekuwa na vinchi vidogo vidogo vingi vya ajabu. Kilosa tu kwa Mangungo kungekuwa na nchi tatu yaani Nchi ya Wasagara, Nchi ya Wakaguru na Nchi ya waliobaki. Kila Kabila ingekuwa nchi.
 
Back
Top Bottom