Tujifunze kupitia Zelenskyy na vita ya Ukraine

Watanzania ni wajinga sana na uthibitisho ni wewe mleta mada na wachangiaji baadhi wa hili mada. Hivi kwa akili Yako ulitaka Russia alipoingiza jeshi lake Ukraine wasichukue hatua? Hivi wakati crimea inachukuliwa kihuni mlikuwa mmelala? Zelensk Bado ni shujaa na uzuri Bado anapambana kutetea nchi yake. Acheni kuzusha mambo yasiyowahusu, Trump na Musk siyo wasemaji wa mwisho wa Ukraine na hawana mamlaka ya kuiamulia Ukraine Cha kufanya kama hakina masilahi kwa Ukraine. Mleta mada go back to school
Itakuwa na wewe ni Mtz na ni miongoni mwa hao wengi ambao umesema ni wajinga.
Kipindi US anaenda kusimika mitambo yake pale Georgia intelligence ya RUSSIA unadhani haikumpekua Ukraine?
 
Halafu kuna historia ya vita kati ya Urusi na nchi nyingine za Ulaya mfano Russo -Swedish war za tangu miaka ya 1700. Kuna vita ya Uingereza na Urusi, Napoleon na Urusi, n.k. Pia kuna matukio ya karibuni kama vile vita baridi na Cubano Missile crisis. Jinsi nchi za Magharibi zilivyoanzisha vikundi vya kupigana na serikali ya Afghanistan iliyokuwa na mahusiano na jumuiya ya kisovieti.Vikundi hivi baadae ndo vilizaa Taliban na Al Qaeda.Pia kuna matukio baada ya vita baridi ambapo NATO waliendelea kumzunguka Russia mfano kuzikaribisha Sweden na Finland kwenye umoja wa NATO ilihali zinapakana kabisa na Russia. Marekani hawezi kukubali Mexico iwe kwenye uhusiano wa kijeshi na Urusi lakini yéyé kumsogelea Urusi na kuweka silaha zake kwenye mpaka wa Urusi anaona sawa tu.
Hizi porojo zote zinahuisianaje na porojo za kwamba nchi za Magharibi zimekuwa zinataka kuingamiza Urusi? Kwani Urusi ndio nchi pekee kupigana vita na nchi nyingine duniani? Kuna nchi au empire yoyote ya zamani dunia hii ambazo haijawahi kupigana vita?? Genghis Khan aliyeivamia Russia alikuwa mtu wa West? Russia haijawahi kuvamia nchi majirani kabla hata ya uwepo wa NATO?
 
Kwahiyo Putin aliamka tu akapeleka jeshi Ukraine kama kichaa?😂😂😂
Mbona hakupeleka jeshi Georgia. Na kwa taarifa yako, Zelensky kaambiwa asipotoa madini Musk atachukua vifaa vyake vya Star Link. Sasa tuone atapigana vipi bila hivyo vifaa vya Star Link. Angekuwa shujaa asingeingia kwenye vita visivyo na faida. Kapoteza watu, kapoteza ardhi yénye mádini, ana mádeni ambayo yatalipwa hadi na vitukuu vyake, ardhi yénye rutuba aliwakabidhi Black Rocks kitambo. Angekuwa shujaa angekubali sharti la kutojiunga na NATO maisha yaendelee. Kama wewe ni mdogo jua nafasi yako,usikubali kutumiwa kwa maslahi ya wakubwa.
Hitler aliamka tu kama kichaa akaanza kuzivamia nchi nyingine na kuua Wayahudi??
Majambazi huwa wanakurupuka tu kama kichaa kwenda kuibia na kuua watu?
 
Trump na Elon Musk wanamuita Zelensky dikteta,asiye na huruma,asiyependa watu wake, tapeli n.k. Mazungumzo ya kumaliza vita yanafanyika Saudi Arabia bila uwepo wa Ukraine, Zelensky anaambiwa atoe sehemu ya madini yake muhimu kwa Marekani Ili kufidia gharama za vita, Urusi kachukua maeneo muhimu ya Ukraine yénye madini na hayo maeneo hayatarudishwa, mamilioni ya wanaume wa Ukraine wamekufa vitani bure tu. Je sisi tunajifunza nini?

1. Usije kubali kutumiwa na Marekani kugombana na jirani yako. Kamwe usikubali. Ukraine walidanganywa na Marekani na washirika wake tangu mwaka 2014 baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais aliyekuwa na maelewano na Urusi. Wakati wa mapinduzi, maafisa wa CIA walikuwepo nchini Ukraine vilevile Victoria Nuland mama mpenda vita alikuwepo Ukraine na alikuwa anagawa bites kwa waandamanaji waliokuwa wanamshinikiza Rais atoke. Mwisho wa siku, Victoria Nuland hajafa waliokufa ni mamilioni ya askari wa Ukraine. Taiwan sijui wanajifunza au na wenyewe watakubali kutumiwa na Marekani kupigana na China.

2. Usimsikilize Marekani pale anapokuhubiria demokrasia, haki za binadamu n.k. Marekani haijali na wala haijawahi kujali demokrasia. Hizo ni propaganda tu na kupiga midomo. Marekani anajijali yeye hamjali yoyote.

3. Hakuna kitu cha bure. Hata upewe msaada wa kondomu na Marekani, utalipia tu. Msaada ni njia ya kukufanya uwe mtumwa.

4. Kibaraka yoyote wa Marekani hana thamani. Hutupwa kama kinyesi baada ya matumizi. Alitupwa Mobutu na Zelensky atatupwa kwani muda wake wa matumizi umekwisha.

5. Usisikilize propaganda za vyombo vya magharibi. Wakati wa vita ya Urusi na Ukraine, vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vinaipamba Ukraine na kuhubiri kwamba Putin ni mvamizi, muuaji ambaye kavamia nchi ya watu na Ukraine inapaswa kusaidiwa. Kiuhalisia, Putin alikuwa anajilinda. Urusi ni superpower hawezi kukubali Ukraine ajiunge na NATO hata iweje. Huo ndo uhalisia..Ukraine haina haki ya kujiunga na NATO. Lakini vyombo vya magharibi vilikuwa havisemi chanzo cha Urusi kuvamia Ukraine. Kama hadi leo wewe unapenda kusikiliza na kuviamini vyombo hivi vya habari( BBC, DW,VOA,CNN,RFI etc) nakushauri utoke huko utumwani.

6. Tupende kujifunza historia na matukio ya ulimwengu. Tufahamu uhalisia, tufahamu mambo yanakwendaje. Kwa sasa hakuna jipya yote ni marudio. Kama Zelensky angejifunza historia na uhalisia wa Ulimwengu, asingekubali kutumiwa na nchi za Magharibi kupigana na Urusi. Zelensky kasababisha vifo vya Raia wake kwa vita iliyokuwa inaepukika. Ahadi zote za uongo alizojazwa na viongozi wa Magharibi hazijatimizwa hata moja isipokuwa ahadi ya kukopeshwa silaha. Hizi silaha walizokopeshwa zitalipwa hadi senti ya mwisho. Kwenye hii vita aliyepoteza ni Ukraine.

Kapoteza watu, kapoteza maeneo, alichokuwa anapigania hajakipata na ana madeni ya mabilioni ya dóllar lazima alipe. Ukosefu wa hekima ndo umeifikisha hapa Ukraine.Biden na Boris Johnson waliomjaza upepo aingie vitani wamemtelekeza.

Umoja wa Ulaya ulioahidi kumsapoti na wenyewe una haha huko na mambo yao. Raia wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya wamechoka hii vita na viongozi waliokuwa wanaisapoti hii vita kama vile Kansela Olaf Scholz watakosa kura kwenye chaguzi zijazo. Wanasiasa wa mlengo wa kulia wanaoahidi kushirikiana na Urusi na kuleta amani wanapata umaarufu na uungwaji mkono.
Zelensky mwanakulitafuta mwanakulipata.

Asanteni.
 
Watu wengi hawajui historia na chanzo cha hii vita, pia nimeamini vyuo vyetu vinazalisha takataka badala ya wasomi.
Huu mgogoro usingefika hapa Kama Kila mtu angeheshimu makubaliano yaliyofikiwa, wakati USSR inasambaratika au mkataba wa Minsk.
Marekani hataki urusi aweke nyukilia Cuba lakini yeye anataka kumzunguka urusi kwa kuweka majeshi yake, washukuru Urusi ilikuwa Ina kiongozi mwenye busara Ila Kama rais angekuwa Medved Sasa hivi tungekuwa tunapokea wazungu wakimbizi.
Sasa MTU kama Lucas Mwashambwa naye utamuita ni msomi?
 
Watu wengi hawajui historia na chanzo cha hii vita, pia nimeamini vyuo vyetu vinazalisha takataka badala ya wasomi.
Huu mgogoro usingefika hapa Kama Kila mtu angeheshimu makubaliano yaliyofikiwa, wakati USSR inasambaratika au mkataba wa Minsk.
Marekani hataki urusi aweke nyukilia Cuba lakini yeye anataka kumzunguka urusi kwa kuweka majeshi yake, washukuru Urusi ilikuwa Ina kiongozi mwenye busara Ila Kama rais angekuwa Medved Sasa hivi tungekuwa tunapokea wazungu wakimbizi.
Medvedev ni mnyama kuliko Putin mkuu.
 
Wewe ndiyo unapaswa kurudi shule ukasome upya!
Fikiria Tanzania tudanganywe tumuondoe Samia harafu tumweke Steve Nyerere au Masanja mkandamizaji ndiyo atutawale tutafika kweli?
Zelensiky hatofautiani na Steve Nyerere au Masanja mkandamizaji aliwekwa tu US ili kuiangamiza Russia lakini wamekuta Putin ni habari nyingine.
Mkuu kuwa mwelewa mgogoro wa Ukraine na urusi haujaanza Jana Wala juzi? Wakati urusi anaivamia Ukraine na kujimegea rasi ya crimea kwa kutumia wahuni wachache wa urusi Zelensk alikuwa Rais? Mbona unakuwa kama boya
 
Watanzania ni wajinga sana na uthibitisho ni wewe mleta mada na wachangiaji baadhi wa hili mada. Hivi kwa akili Yako ulitaka Russia alipoingiza jeshi lake Ukraine wasichukue hatua? Hivi wakati crimea inachukuliwa kihuni mlikuwa mmelala? Zelensk Bado ni shujaa na uzuri Bado anapambana kutetea nchi yake. Acheni kuzusha mambo yasiyowahusu, Trump na Musk siyo wasemaji wa mwisho wa Ukraine na hawana mamlaka ya kuiamulia Ukraine Cha kufanya kama hakina masilahi kwa Ukraine. Mleta mada go back to school
Wapuuzi kama nyie ndio mmesababisha zele na NATO kupokea majonzi pale ukraine
 
Watanzania ni wajinga sana na uthibitisho ni wewe mleta mada na wachangiaji baadhi wa hili mada. Hivi kwa akili Yako ulitaka Russia alipoingiza jeshi lake Ukraine wasichukue hatua? Hivi wakati crimea inachukuliwa kihuni mlikuwa mmelala? Zelensk Bado ni shujaa na uzuri Bado anapambana kutetea nchi yake. Acheni kuzusha mambo yasiyowahusu, Trump na Musk siyo wasemaji wa mwisho wa Ukraine na hawana mamlaka ya kuiamulia Ukraine Cha kufanya kama hakina masilahi kwa Ukraine. Mleta mada go back to school
Mimi sio mtanzania ila kama watanzania wajinga na wewe ndio mwenye akili wao basi kweli nchi yenu imejaa wajinga mana hata wewe unaejiona una akili ni jinga la wajinga

Zelesk amepoteza Kila kitu Ili tu ajiunge na NATO Zelesk nae pia ni mjinga kama nyinyi watanzania

Kwani Zelesk alipungukiwa Nini kuishi bila ya kuwa mwanachama wa NATO
 
Trump ni kichaa lkn Yuko sawa kwa upande Mwingine.

Mosi, Hawawezi kuendelea kuisupport Ukraine Milele.

Sasa Kilichobaki ni kuchagua aendelee kupoteza Watu, Au apoteze Ardhi na Madini
 
Mimi sio mtanzania ila kama watanzania wajinga na wewe ndio mwenye akili wao basi kweli nchi yenu imejaa wajinga mana hata wewe unaejiona una akili ni jinga la wajinga

Zelesk amepoteza Kila kitu Ili tu ajiunge na NATO Zelesk nae pia ni mjinga kama nyinyi watanzania

Kwani Zelesk alipungukiwa Nini kuishi bila ya kuwa mwanachama wa NATO
Wewe huelewi chochote na unaposema Zelensk kapoteza Kila kitu una maana Gani? Unajua maana ya Sovereignity ama unabwabwaja tu? Unahisi Ukraine ni wajinga kama nyie waafrika kuzuiliwa kutumia maji ya ziwa Victoria na Misri na mkanywea
 
Uthibitisho wa haya madai ni upi?

Nitakutafutia video ambayo m'beberu mmoja akiongea na kusema Russia hawezi kukubali military base ya US mpakani mwake kwa kupitia Ukraine 🇺🇦 awe mwanachama wa NATO. Hilo ndiyo hangaiko kubwa la russ
 
Back
Top Bottom