Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 168
- 442
Trump na Elon Musk wanamuita Zelensky dikteta,asiye na huruma,asiyependa watu wake, tapeli n.k. Mazungumzo ya kumaliza vita yanafanyika Saudi Arabia bila uwepo wa Ukraine, Zelensky anaambiwa atoe sehemu ya madini yake muhimu kwa Marekani Ili kufidia gharama za vita, Urusi kachukua maeneo muhimu ya Ukraine yénye madini na hayo maeneo hayatarudishwa, mamilioni ya wanaume wa Ukraine wamekufa vitani bure tu. Je sisi tunajifunza nini?
1. Usije kubali kutumiwa na Marekani kugombana na jirani yako. Kamwe usikubali. Ukraine walidanganywa na Marekani na washirika wake tangu mwaka 2014 baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais aliyekuwa na maelewano na Urusi. Wakati wa mapinduzi, maafisa wa CIA walikuwepo nchini Ukraine vilevile Victoria Nuland mama mpenda vita alikuwepo Ukraine na alikuwa anagawa bites kwa waandamanaji waliokuwa wanamshinikiza Rais atoke. Mwisho wa siku, Victoria Nuland hajafa waliokufa ni mamilioni ya askari wa Ukraine. Taiwan sijui wanajifunza au na wenyewe watakubali kutumiwa na Marekani kupigana na China.
2. Usimsikilize Marekani pale anapokuhubiria demokrasia, haki za binadamu n.k. Marekani haijali na wala haijawahi kujali demokrasia. Hizo ni propaganda tu na kupiga midomo. Marekani anajijali yeye hamjali yoyote.
3. Hakuna kitu cha bure. Hata upewe msaada wa kondomu na Marekani, utalipia tu. Msaada ni njia ya kukufanya uwe mtumwa.
4. Kibaraka yoyote wa Marekani hana thamani. Hutupwa kama kinyesi baada ya matumizi. Alitupwa Mobutu na Zelensky atatupwa kwani muda wake wa matumizi umekwisha.
5. Usisikilize propaganda za vyombo vya magharibi. Wakati wa vita ya Urusi na Ukraine, vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa vinaipamba Ukraine na kuhubiri kwamba Putin ni mvamizi, muuaji ambaye kavamia nchi ya watu na Ukraine inapaswa kusaidiwa. Kiuhalisia, Putin alikuwa anajilinda. Urusi ni superpower hawezi kukubali Ukraine ajiunge na NATO hata iweje. Huo ndo uhalisia..Ukraine haina haki ya kujiunga na NATO. Lakini vyombo vya magharibi vilikuwa havisemi chanzo cha Urusi kuvamia Ukraine. Kama hadi leo wewe unapenda kusikiliza na kuviamini vyombo hivi vya habari( BBC, DW,VOA,CNN,RFI etc) nakushauri utoke huko utumwani.
6. Tupende kujifunza historia na matukio ya ulimwengu. Tufahamu uhalisia, tufahamu mambo yanakwendaje. Kwa sasa hakuna jipya yote ni marudio. Kama Zelensky angejifunza historia na uhalisia wa Ulimwengu, asingekubali kutumiwa na nchi za Magharibi kupigana na Urusi. Zelensky kasababisha vifo vya Raia wake kwa vita iliyokuwa inaepukika. Ahadi zote za uongo alizojazwa na viongozi wa Magharibi hazijatimizwa hata moja isipokuwa ahadi ya kukopeshwa silaha. Hizi silaha walizokopeshwa zitalipwa hadi senti ya mwisho. Kwenye hii vita aliyepoteza ni Ukraine.
Kapoteza watu, kapoteza maeneo, alichokuwa anapigania hajakipata na ana madeni ya mabilioni ya dóllar lazima alipe. Ukosefu wa hekima ndo umeifikisha hapa Ukraine.Biden na Boris Johnson waliomjaza upepo aingie vitani wamemtelekeza.
Umoja wa Ulaya ulioahidi kumsapoti na wenyewe una haha huko na mambo yao. Raia wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya wamechoka hii vita na viongozi waliokuwa wanaisapoti hii vita kama vile Kansela Olaf Scholz watakosa kura kwenye chaguzi zijazo. Wanasiasa wa mlengo wa kulia wanaoahidi kushirikiana na Urusi na kuleta amani wanapata umaarufu na uungwaji mkono.
Zelensky mwanakulitafuta mwanakulipata.
Asanteni.