Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

Kosa kubwa alilofanya ni ile akili ya MTU mweusi ya kufanya Accumulation bila distribution

Yale maeneo potential yote aliyojimilikisha kigamboni Kama angeamua kutoa ghorofa lake moja akawapa wanafunzi wakaishi bure au akawa na programs maalumu za kuwalipia Ada wanafunzi hata wanafunzi 100 kila mwaka .

Tafsiri sahihi ya utajiri ya MTU mweusi huwa inafikirisha Sana .
Hilo la gorofa ndio umebakiziwa wewe sasa ulifanye kwa upande wako
 
Mkuu niliwahi kusema matajiri wakubwa TANZANIA hawana msaada wa moja kwa moja kwa jamii nikatukanwa na kuambiwa nitafute vyangu.
Uoni ata kiongozi wenu anadiliki kuwapa viongozi wa Dini Milioni mia mia lakini kuna watoto yatima wanakosa elimu, hizo bilioni Moja mpaka sasa angewalipia Mayatimq ada na chakula watoto yatima wangeisha mitaani Bilioni moja ingewalipa mpaka elimu ya juu.
 
Kuna kitu inawezekana hatukijui Ila hao unakuta Wana watoto 2 ndani Ila nje wapo 5 hivyo kupanga ni kuchagua
Na hili ni sahihi kabisaaa ukizingatia wake wa maboss kama hao wanapenda sana kudeka hvo na suala la kuzaa watoto wanaonaga ni kama kujichosha na ushamba hvo huishia kuzaa watoto wawili au watatu
 
Kwani ukilia kwa kuzimia ndo nini yaani? Walishalia kidogo inatosha.
Nashangaa ndugu yangu. Bado tuna safari ndefu sana ya mitazano na kuto ku judge wengine . Kila mtu ana aina yake ya kuomboleza , walishalia walishatulizwa kwanza wako kwenye shock- na yaelekea wamekuzwa in a matured manner kuweza kua bsorb mambo. Je tutasema mtu akilia kwa mayowe na kugala gala ndio kipimo cha huzuni, no way? Je huzuni lazma mtu awe mchafu na madera nk no way. Hebu watanzania tuachane na ushamba usio kuwa na maana. Ukuiona kuomboleza ni mayowe good then usimshangae ambaye kuomboleza ni kuwa calm . Ni kama tunataka taifa zima tabakia zama za mawe katika lifestyle.
 
Mungu ndiye anakuza watu
Negative, hizo ni kauli za watu wanaokwepa kufikiri. You want more kids, unaweza kuwakuza at this modern ages?
Look at your financial capacity, else utaishia kuchakaa, na kuwalaumu bure
 
Nipo nacheki hapa msiba wa Ndugulile, kuacha watoto wawili tu, pamoja alikuwa ana uwezo wa kipesa na cheo lakini kaishia kwenye watoto wawili, watoto wawili hawa naona kawakuza na kuwasomesha kwenye shule za gharama inawezekana nje ya nchi maana hata Kiswahili chao ni broken sana wanakuwa kama sio watanzania.

Lawrence Mafuru nae nadhani aliacha watoto wawili tu.

Swali kwa makapuku wenzangu, hivi Sisi maskini tunazaa watoto wengi ili iweje? Na utakuta pengne hata uwezo wa kuwahudumia tuu kikamilifu kwenye elimu na gharama za kila siku hatuwezi, nini maana ya hii?

Nahis NI vizuri kuzaa watoto kulingana na kipato chako, ambao utawamudu vizuri, utakaowapa elimu ya uhakika sio hii ya kuunga unga.

Sisi maskini tunawaza eti tukizaa watoto wengi ndio hao badae watatusaidia, wewe mzazi somesha mtoto, hudumia kwa kadiri ya uwezo wako maana ni jukumu lako, badae akipata maisha mazuri NI yeye sasa atajua atakusaidiaje, ndio ile utakuta wazazi wananunia wakwe zao wanaona kama wao ndio wanafanya wasipewe pesa na mtoto wao.

Tuzae Kwa mahesabu, utakuta mtu ana watoto wanne, halafu kapanga chumba na sebule, sasa jiulize hapo ndani wanaishije, tuwekeze nguvu kwenye kujenga uchumi Kwanza na kuzaa kwa akili.

Tambua kitu kimoja kila mtu anapofanya jambo kunakuwa na sababu,mfano Hao wasomi hawana mda mwingi wakukaa na familia zao tofauti na familia zingine Ambapo watoto ni baraka na faraja kubwa
 
Nipo nacheki hapa msiba wa Ndugulile, kuacha watoto wawili tu, pamoja alikuwa ana uwezo wa kipesa na cheo lakini kaishia kwenye watoto wawili, watoto wawili hawa naona kawakuza na kuwasomesha kwenye shule za gharama inawezekana nje ya nchi maana hata Kiswahili chao ni broken sana wanakuwa kama sio watanzania.

Lawrence Mafuru nae nadhani aliacha watoto wawili tu.

Swali kwa makapuku wenzangu, hivi Sisi maskini tunazaa watoto wengi ili iweje? Na utakuta pengne hata uwezo wa kuwahudumia tuu kikamilifu kwenye elimu na gharama za kila siku hatuwezi, nini maana ya hii?

Nahis NI vizuri kuzaa watoto kulingana na kipato chako, ambao utawamudu vizuri, utakaowapa elimu ya uhakika sio hii ya kuunga unga.

Sisi maskini tunawaza eti tukizaa watoto wengi ndio hao badae watatusaidia, wewe mzazi somesha mtoto, hudumia kwa kadiri ya uwezo wako maana ni jukumu lako, badae akipata maisha mazuri NI yeye sasa atajua atakusaidiaje, ndio ile utakuta wazazi wananunia wakwe zao wanaona kama wao ndio wanafanya wasipewe pesa na mtoto wao.

Tuzae Kwa mahesabu, utakuta mtu ana watoto wanne, halafu kapanga chumba na sebule, sasa jiulize hapo ndani wanaishije, tuwekeze nguvu kwenye kujenga uchumi Kwanza na kuzaa kwa akili.

Wewe ni mpumbavu
 
Back
Top Bottom