OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 54,484
- 123,107
Sarakasi zilizotokea kwenye kumpitisha Samia kuwa mgombea wa CCM kwenye uchaguzi Mkuu ni za kutia aibu kubwa sana.
Lakini nimekuwa najiuliza nini hasa sababu ya CCM kumpitisha bibi harusi huyu mlango wa nyuma? Kwa nini haiwezekani fomu zikatolewa kwa wote wenye nia na kupigiwa kura? Nini sababu ya wao kufanya hivyo. Katika majukwaa inatajwa Samia kufanya makubwa katika utawala wake. Si hayo makubwa yataleta kura za bwerere kabisa?
Nje ya hapo kumekuwa na mambo mengi ya hovyo kabisa kulazimisha kila kitu kiwe cha Samia. Mabango kila mahali, huwezi kufanya sherehe ya kiserikali bila bango la Samia, ajabu mpaka kwenye muhimili wa Mahakama sherehe zao zina mabango ya Samia......Sijui Samia Cup, Samia Urembo, Ndondi Vitasa vya Samia, Goli la Mama Samia, kila kitu kila mahali Samia.
Najiuliza kama mtu umefanya kazi vizuri ikaonekana, haya yote ya nini? Kwa nini unahangaika kiasi hiki kama KUKU MTETEA ANATAKA KUTAGA?