SoC04 Tuisome Katiba yetu ili kuijua nchi yetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Angyelile99

Member
Oct 9, 2023
39
52
Utangulizi. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzia mwaka 1962, wakati Tanganyika ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza. Katiba ya kwanza ya Tanganyika ilipitishwa mwaka 1962 na ilikuwa na mabadiliko kadhaa hadi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulipoundwa mwaka 1964, kubuni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ya mwaka 1977) ilipitishwa baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana kuwa Jamhuri moja ya Muungano wa Tanzania. Katiba hii imefanyiwa marekebisho kadhaa tangu kuanzishwa kwake. Ambapo tunaita amendiment kwa maana ya kwamba maboresho na mabadiliko ya baadhi ya vipengere na sheria ndani ya katiba mama kwa maridhiano ya sheria za kibunge.

20240604_083104.jpg

Source: Google image

Katika kusimamia sheria za nchi kulingana na katiba inavo eleza, wananchi wa Tanzania wana nafasi muhimu sana katika utekerezaji wa masuara mbali mbali na masuara hayo baadhi yake ni kama ifuatavyo;

1. Haki ya Kupiga Kura: Wananchi wanayo haki ya kupiga kura na kuchagua viongozi wao ambao wataunda na kusimamia sheria.

2. Uwajibikaji wa Viongozi: Wananchi wanapaswa kufuatilia na kudai uwajibikaji kutoka kwa viongozi wao kuhusu utekelezaji wa sheria.

3. Kutoa Maoni na Malalamiko: Wananchi wanayo haki ya kutoa maoni na malalamiko yao kuhusu sheria na utekelezaji wake.

4. Kufuata Sheria: Wananchi wanapaswa kuheshimu na kufuata sheria zilizowekwa na mamlaka husika.

5. Kusoma na Kuelimishwa Kuhusu Sheria: Elimu kuhusu sheria inawawezesha wananchi kuelewa haki zao na jinsi ya kusimamia sheria ipasavyo.

6. Kusimamia Misingi ya Kidemokrasia: Wananchi wana jukumu la kusimamia misingi ya kidemokrasia katika nchi yao, ikiwa ni pamoja na kuheshimu mamlaka za serikali.

7. Kupinga Ukiukwaji wa Haki za Binadamu: Wananchi wanayo jukumu la kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu na kushiriki katika juhudi za kurekebisha sheria zinazokiuka haki hizo.

8. Kusaidia Katika Mchakato wa Kufanya Sheria: Wananchi wanaweza kutoa maoni yao na kushiriki katika mchakato wa kufanya sheria ili ziendane na mahitaji ya jamii.

9. Kusaidia Katika Kusimamia Utekelezaji wa Sheria: Wananchi wanaweza kuchangia katika kusimamia utekelezaji wa sheria kwa kushirikiana na mamlaka husika.

10. Kuboresha Sheria: Wananchi wanaweza kuchangia katika kuboresha sheria kwa kutoa mapendekezo na maoni yao kwa mamlaka zinazohusika.

Uhalisia kuhusu mwananchi na katiba
Pamoja na kwamba katiba imeweka wazi nafasi ya mwananchi wa kitanzania katika utekarazaji na ufuatiriaji wa masuara mbali mbali yanayo husu maendeleo na uwajibikaji wa viongozi wao, aidha kutolea maoni na kuhoji pia. Lakini mpaka sasa watanzania wengi ikiweo wasomi wamekua nyuma zaidi katika ufuatiriaji kuhusu masuara haya, ikishinikizwa zaidi na ukosefu wa elimu ya katiba ya nchi na kutojua ni kwa namna gani imewapa nafasi katika masuara mbali mbali kama wanacnhi wa tanzania.

Hivo katiba kubakia kuzungumzwa kwa eneo kubwa na watu wachache ikijumuisha wanasiasa, wanasheria pamoja na wasimamizi wa vyombo vya usarama
Nini kifanyike ili kua na nchi yenye watu wenye kuijua katiba ya nchi na kua na uwezo wa kujisimamia haswa katika masuara ya kuhoji, kujibia ama kutoa maoni kisheria zaidi.

Moja kwa moja binafsi naona kunahaja ya uanzishwaji wa somo la katiba kwa ngazi ya sekondari kupitia somo la ulaia kwa ngazi ya O level ama kwa ngazi ya A level katika somo la general studies ama katika soma la historia ya Tanzania. Mchakato huu unaweza kusaidia kua na kizazi cha watu wenye ufahamu zaidi kuhusu katiba ya nchi na mambo yaliyomo ndani yake na nafasi yao kama watanzania.

Utekelezwaji wake
Katika mchakato unao husu mabadiliko ya kimtaala wa elimu ya Tanzania na aina ya maada zinazotakiwa kufundiswa kulingana na kidato kunahaja ya kuzingatia mambo haya katika kuakikisha somo la katiba linafundishwa mashureni.

Moja, kuna haja ya kuondoa mada zinazo weza kujirudia rudia aidha katika vidato tofauti tofauti kwenye somo moja ama katika masomo tofauti tofauti. Kwa mfano kwa ngazi ya A level kuna maada ya mazingira inayo jirudia kwenye somo la geography 1 pamoja na somo la general studies.

Kwa kufanya haya kunaweza kupatikana nafasi ya ufundishaji wa somo hili la katiba bira ya kuathiri mifumo ya ufundishaji wa masomo mengine.

Pili kwa kuanzisha somo hili katika somo mama la historia ya tanzania. Kipengere cha katiba kuibuka kama maja ja maada zinazo weza kupatikana katika somo hilo.

Faida zaidi zinazo weza jitokeza kama mchakato huu ukatekelezwa
1. Kukuza Uelewa wa Wajibu na Haki: Wanafunzi watapata uelewa wa kina kuhusu wajibu na haki zao kama wananchi, na hivyo kusaidia katika kujenga jamii iliyo na ufahamu mkubwa wa misingi ya kidemokrasia.

2. Kuimarisha Demokrasia: Kuelimisha vijana kuhusu Katiba kutawaandaa kuwa raia watakaoshiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na kupiga kura na kushiriki katika utawala wa nchi.

3. Kukuza Utawala Bora: Uelewa wa Katiba utasaidia kujenga utamaduni wa utawala bora kwa kufuata sheria na kanuni za nchi, na hivyo kupunguza rushwa na ubaguzi.

4. Kuchochea Mjadala na Ushirikiano: Kujifunza kuhusu Katiba kunaweza kuchochea mjadala wa kina kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa na kusaidia katika kujenga uelewa mpana na ushirikiano miongoni mwa wanafunzi.

5. Kuimarisha Utambulisho wa Kitaifa: Elimu kuhusu Katiba itasaidia kuimarisha utambulisho wa kitaifa miongoni mwa wanafunzi kwa kuwafahamisha kuhusu historia na misingi ya nchi yao.

6. Kuchochea Ushiriki wa Kiraia: Kuelimisha wanafunzi kuhusu Katiba kutawahamasisha kushiriki katika shughuli za kiraia kama vile maandamano ya amani, kutetea haki za binadamu, na kuhamasisha mabadiliko ya kijamii.

7. Kuwajengea Uwezo wa Kisheria: Wanafunzi watajengewa uwezo wa kisheria ambao utawawezesha kuelewa na kutetea haki zao, pamoja na kuwasaidia kufahamu mchakato wa kisheria na utekelezaji wa sheria.

8. Kuchochea Ubunifu na Uwajibikaji: Elimu kuhusu Katiba itawawezesha wanafunzi kuwa na mtazamo wa ubunifu katika kutatua changamoto za kijamii na kuwa raia wanaozingatia uwajibikaji wao kwa jamii na serikali.

Kuongeza somo la Katiba katika mtaala wa shule za sekondari nchini Tanzania kunaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuandaa kizazi cha vijana wenye ufahamu wa kina kuhusu mifumo ya kisiasa, haki za binadamu na utawala bora.
 
Moja, kuna haja ya kuondoa mada zinazo weza kujirudia rudia aidha katika vidato tofauti tofauti kwenye somo moja ama katika masomo tofauti tofauti. Kwa mfano kwa ngazi ya A level kuna maada ya mazingira inayo jirudia kwenye somo la geography 1 pamoja na somo la general studies.

Kwa kufanya haya kunaweza kupatikana nafasi ya ufundishaji wa somo hili la katiba bira ya kuathiri mifumo ya ufundishaji wa masomo mengine.
Sawa, ya muhimu yote yawekwe kwenye mitaala
 
Back
Top Bottom