SoC04 Tuhamasishe unywaji maziwa ili tukuze uchumi

Tanzania Tuitakayo competition threads

fimbo kahema

New Member
Jun 4, 2024
1
0
Nchi ya Tanzania imebarikiwa vivutio vya asili ikiwemo mbuga, mito na kadhalika. sekta ya mifugo ni mojawapo ya sekta ambazo huwa zinachangia kwa kiwango kikubwa sana katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kilimo na chakula duniani(FAO) Tanzania ni ya tatu kwa idadi kubwa ya mifugo barani Afrika ambapo imepitwa na Ethiopia na Sudan kaskazini. Tanzania inamiliki asilimia 1.4% ya Ng'ombe duniani na asilimia 11% ya ng'ombe barani Afrika. Sensa ya kilimo na mifugo iliyofanyika 2019/2020 inaonyesha Tanzania ina jumla ya Ng’ombe milioni 33.9. Sehemu kubwa ya Ng’ombe ambao wapo nchini Tanzania ni Ng’ombe wa asili na sio wale wa kupandikiza mbegu. Kutokana na takwimu za idadi ya mifugo iliyoko nchini Tanzania ni wazi bila ya shaka kwamba kiwango cha uzalishaji maziwa nchini Tanzania ni kikubwa na hivyo uzalishaji maziwa sio tatizo. Tatizo lipo katika kiwango cha unywaji maziwa

Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 inaonyesha kwamba Tanzania ina wakazi ambao ni milioni 61.74 na inaonekana kwamba idadi ya watu hukua kwa asilimia 3.2 kwa kila mwaka. Kwa takwimu hizo inaonyesha kwamba kuna fursa kubwa sana ya soko la ndani la maziwa kama likihamasishwa vizuri.Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 jumla ya wakazi milioni 40,201,425 ambayo ni sawa na asilimia 65.1% wanaishi maeneo ya vijijini na raia wengi wanajishughulisha na shughuli za sekta ya kilimo. Kwa mujibu wa ripoti ya uchumi ya mwaka 2020 inaonyesha kwamba sekta ya mifugo inachangia asilimia 27 ya mchango wa sekta ya kilimo katika pato la taifa.

Ripoti ya shirika la afya duniani(WHO) ya 2022 ilisema kwamba kila mtu anatakiwa anywe lita zisizopungua 200 kila mwaka na anatakiwa anywe glasi moja ya maziwa kila siku.inafahamika kwamba unywaji maziwa una faida mbalimbali kwa wanadamu hususani wanywaji za kiafya.

Serikali katika zoezi la uratibu wa sekta nzima ya maziwa ilianzisha bodi ya maziwa kwa ajili ya kurasimisha sekta ya maziwa na kuisimamia lakini bado mwitikio haujawa mkubwa sana kutokana na ushindani unaoletwa na makampuni ya vinywaji vya bia na soda. Serikali ilianzisha wiki ya maziwa kwa ajili ya kuhamasisha unywaji maziwa. Takwimu zinaonyesha Kwa mwaka 2023 inakadiriwa watanzania walikunywa wastani wa lita 66 za maziwa kwa mwaka na kwa mwaka 2024 kiwango kiliongezeka mpaka lita 67.2 kwa mwaka.

Kwa maoni yangu katika miaka 25 ijayo kama taifa tunatakiwa tuwe na kampeni kubwa za kuhamasisha unywaji maziwa kwa wingi ili kuinua uchumi wa watu mmoja mmoja mpaka wa nchi kwani kwa kutumia rasilimali ya mifugo iliyopo basi kuna uhakika wa kupatikana kwa maziwa mengi sana. Nashauri serikali itumie mbinu zifuatao kwa kuwashirikisha wadau wa sekta ya maziwa ili kukuza unywaji wa maziwa na hatimaye kukuza pato la nchi:

  • Kuasisi vilabu vya unywaji maziwa mashuleni. Vilabu hivyo viwe vinapeana elimu juu ya fursa ambazo zinapatikana katika mnyororo wa thamani wa mifugo pamoja na umuhimu wa kunywa maziwa na faida zake mwilini. Kwa kufanya hivyo wanafunzi wataanza kuhamasika kunywa maziwa na pia kuwahamasisha wenzao wanywe maziwa.
  • Kuhamasisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutunga nyimbo za kusifia/kutukuza unywaji maziwa. Wasanii watapewa semina za kuwaelewesha juu ya umuhimu wa kunywa maziwa na pia waambiwe faida za kiuchumi ambazo watakuwa wamesaidia nchi kwa kuhamasisha raia wanywe maziwa kupitia nyimbo zao. Licha ya kwamba hakuna takwimu rasmi lakini wimbo kama “bia tamu” umesaidia kuongeza mapato ambayo yatokanayo na unywaji pombe nchini na kama wasanii wakatumia ubunifu wao kuhamasisha unywaji maziwa basi pato litokanalo na unywaji maziwa litaongezeka.
  • Mashindano ya michezo yenye kuhamasisha unywaji maziwa
  • Kuhamasisha utengenezwaji wa filamu ambazo zitahamasisha unywaji maziwa. Katika filamu na tamthilia zetu bodi ya filamu iwahamasishe watengenezaji maudhui ya filamu waweke matukio ambayo yatakuwa yana maudhui ya kuhamasisha unywaji maziwa kwa wingi sana.
  • Kuhamasisha riwaya zenye kuhamasisha unywaji maziwa. Katika riwaya na fasihi andishi kwa ujumla ambazo zinapatikana mashuleni zinatakiwa ziwe na maudhui ambayo itahamasisha watu wanywe maziwa kwa wingi.
  • Kuweka mabango kwenye maeneo ya umma yenye kuhamasisha unywaji maziwa. Mabango hayo yawekwe kwenye barabara kubwa na pia yawekwe kwenye mitandao ya kijamii ambapo yahamasishe watu wanywe maziwa kwa wingi.
  • Kuwatumia viongozi wa dini kuhamasisha unywaji maziwa. Viongozi wa dini watumie ushawishi wao kwa waumini kuwasomea maandiko yenye kuhamasisha unywaji maziwa kwa wingi huku wakitumia lugha zenye ubunifu mkubwa.
  • Kuweka masharti rafiki kwa wawekezaji wa maziwa. Masharti ya kuwekeza kwenye biashara ya kuuza maziwa yawe ni rafiki ambayo yatawavutia watu wengi kufungua migahawa ya kuuza maziwa ambapo upatikanaji wake utakuwa kwa wingi Zaidi na hivyo bei za maziwa kushuka kutokana na kuwa na wingi wake.
Mkakati ukitekelezwa ipasavyo basi pato la wafugaji na mpaka makusanyo ya serikali kupitia sekta hiyo yataongezeka. Mpango huu utainua soko la ndani la maziwa na utainua hali za maisha za wakazi wa vijijini na hivyo kupunguza ongezeko la watu wanaohamia maeneo ya mijini kwa ajili ya kutafuta fursa za maisha.

Nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa maziwa ni pamoja na India, Marekani, Pakistan, Brazil, Ujerumani, Urusi, Ufaransa, Uturuki, pamoja na New Zealand. India ndio taifa ambalo linaloongoza katika uzalishaji wa maziwa duniani soko lake kubwa la wanywaji wa maziwa linaanzia kwa raia wake wa nchi hiyo ambao wamehamasika kunywa maziwa kwa kiwango kikubwa sana na hali hiyo inawezekana nchini Tanzania. Nchi ya pili ambayo ni Marekani ilianza kupata mporomoko ya idadi ya wanywaji maziwa nchini humo tokea miaka ya 1950 lakini ilipofika mnamo mwaka 1993 bodi ya maziwa ya jimbo la California ikaanzisha kampeni maalumu ya kuhamasisha unywaji maziwa nchini katika jimbo hilo ambayo iliitwa “Got Milk?” Baada ya miaka 20 kampeni hii ilizaa matunda makubwa sana na ilichangia watu wengi kujenga mtindo wa maisha wa kunywa maziwa na hatimaye hali hiyo kuhamia majimbo mengine. Naamini kama mpango huo nliosema utatekelezwa basi itafika hatua raia wa kawaida akitembelewa na mgeni ataenda dukani kuagiza mgeni aletewe maziwa na wala sio soda ama bia na hivyo kukuza uchumi kwa kiwango cha juu.
 
Back
Top Bottom