Tuendelee au nimuache aende zake

Ni miaka 2 Sasa toka nikate mawasiliano na aliyekuwa mchumba wangu. Jmosi iliyopita amenitafuta baada ya hiyo miaka 2! Tulidumu kwenye mahusiano kama miaka 3 na miezi kadhaa kutokana na changamoto za maisha tulikuwa tunakaa Sehemu tofauti.

Baada ya yy kihamia mkoa mwingine mawasiliano yalianza kuwa ya shida.Alikuwa anakaa hata mwezi bila kuongea na mimi.

Hii hali ilikua inaniumiza na nilijaribu Kila namna kurekebisha ila baadae yalikata kabisa!

Nikawa najaribu kumtafuta Hadi kupitia marafiki zake wakawa wanasema watamfikishia taarifa ila hakuwahi kunitafuta! Ni mtu ambae tulikuwa tunaendana kwa vitu vingi na nilimpenda sana!

Wakati wote huo ambao alikuwa hapatikani nlikokuwa ni mtu mwenye mawazo, huzuni, hasira,kulia,kisirani na nikawa mtu wa tofauti kbs!Nikaona kuwa ndio mwisho wetu na tumeshaachana.

Ilininichukua muda sana kukubaliana na hali hali hallisi hadi Kuna wakati niliugua sana na kukonda.Hadi hii juzi ndio amenitafuta baada ya ukimya wa miaka 2! Nilimuuliza kwnn alipotea ghafla alinielezea stori ndefu ila ni kwamba alipata changamoto nyingi na baadae kuhama nchi. Alipata kazi nchi nyingine ( hapa Africa)na Hadi Sasa anafanya kazi huko na amekuja kwa ajili ya likizo' kisha atarudi huko.Ameniomba msamaha na anahitaji turudiane.

Nilimuuliza kuhusu mawasiliano yetu itakuaje akasema atayaboresha na atakuwa anakuja kuniona Kila likizo.

Akili inakuwa ngumu sana kumuamini japokuwa bado nampenda. Nikifikiria hali ngumu niliyopitia Hadi kuwa sawa naona ni ngumu kuamini tena.Katika hii miaka miwili ambayo hatukuwa pamoja,nimekuwa na mahusiano kadhaa ambayo mengine hata mwezi haufiki tunaachana.

Nikubali tuanze upya na kuamini tena? au ni mpasha kiporo nimuache aende zake tu? Nikimuamini af azingue tena mtanisindikiza Mirembe🤌😂) Wadau niamue nini?
UTAISHI NAE KWA MASHAKA HADI LINI, ACHIA NGAZI
 
Back
Top Bottom