Tuambie kitu ulichofanyiwa utotoni kikakuletea madhara hadi leo

Baada ya baba yangu kufariki hali ya familia yangu kiuchumi ikawa mbaya sana. Hiyo ikapelekea kunyanyaswa sana na familia ya babu mzaa mama tulivoenda kuishi wakati sisi familia mambo yalipokuwa poa tulikuwa tukiwasaidia bila masimango hiyo imetokea mimi kuichukia familia ya mama yangu hadi leo.
 
Mimi mama yangu na baba yangu walikua wazima na walikua uwezo wakunilea. Sasa cjui kwanini walikua wananipeleka kwa watu tofauti tofauti. Mara mjomba, mama mdogo, binamu shanganzi. Mpaka namaliza la saba nililewa nawatu kama tisa. Nasijui kwanini nimimi tu maana nina ndugu zangu wengine wao walilewa nao. Sasa kitu ambacho kimeniathir kutokua na mapenzi ythati kwa mtu, hata mtu anipende vipi. Huwa namchukulia poua akiwemo mama yanga mme Wangu. Najaribu kuficha hii tabia watu wasigunduwe. Pia baba yangu kafa mwaka juzi ila hata tonne lachoozi hakuna. Watoto wangu najitahidi kuwapenda lakini bado. Maana hata apigwe na house girl naona tu poua. Au mtu akinumiza naona kawaida. Au kunisema vibaya sishituki wala kukasirika.
Pole sana mkuu muombe Mungu akusaidie sana utoke kwenye hiyo hali sio nzuri.
 
Ilikuwaje? Aisee pole sana
Asante chief ilikua ni birthday ya jiran yetu sasa me nilialikwa na huyo mama ambaye mtoto wake ndo ilikua birthday yake bas ni kaenda , mda ulipofika wa kula keki kila mtoto aliwekewa keki yake na yule msichana ambaye ndo birthday yake akaanza kulisha keki ikafika zamu yangu nikalishwa sasa baadaya mda nikaanza kujisikia vibaya, nikatoka nje nikiwa najikokota kwenda home kwa bahati, nzur kuna watu wakaniona na kunipa msaada wakanibeba mpk nyumban nilikua natapika sana nguvu ziliniishia ilibid kwanza na hali inazid kuwa mbaya nikapelekwa hospital (lugalo )cha kwanza walinipa maziwa nikatapika hadi ile keki na baada ya mda nilivopimwa dokta alisema kuwa nimekula chakula kilichokua na sumu
 
Mkuu walitaka kukumaliza hivi hivi?
 
Mimi nilikuwa nikiwapa taarifa ndugu zangu za maendeleo ya shule hata nikiwa wa kwanza walikuwa wananibeza na kuninyima huduma za unform na madaftar nikaanza kujitegemea mwenyewe huduma za shuleni kwa kuuza mapera nikiwa darasa la nne baadaye nikajifunza uchoraji kwa jamaa mmoja hivi kule mbeya mjini kwa kweli sanaa ya uchoraji ikawa inaniingizia kipato na kufanya nidorore kielimu nikiwa darasa la sita sababu hapo nilikuwa nawaza kodi ya chumba vilevile nikiugua niliku cpati huduma ya matibabu sababu maangu alikufa baada ya kutengana na baba nikawa naishi na bibi kuanzia mwaka 1989 nikiwa na miaka miwil kwa kweli ndugu walininyanyapaa sana asante Mungu now wananiona wa maana sana sababu napata vijicent..
Ndugu walivyo nawe wachuniee,,,mi amnae hanijali wala sina muda nae
 
Mimi mama yangu na baba yangu walikua wazima na walikua uwezo wakunilea. Sasa cjui kwanini walikua wananipeleka kwa watu tofauti tofauti. Mara mjomba, mama mdogo, binamu shanganzi. Mpaka namaliza la saba nililewa nawatu kama tisa. Nasijui kwanini nimimi tu maana nina ndugu zangu wengine wao walilewa nao. Sasa kitu ambacho kimeniathir kutokua na mapenzi ythati kwa mtu, hata mtu anipende vipi. Huwa namchukulia poua akiwemo mama yanga mme Wangu. Najaribu kuficha hii tabia watu wasigunduwe. Pia baba yangu kafa mwaka juzi ila hata tonne lachoozi hakuna. Watoto wangu najitahidi kuwapenda lakini bado. Maana hata apigwe na house girl naona tu poua. Au mtu akinumiza naona kawaida. Au kunisema vibaya sishituki wala kukasirika.
duh pole mkuu ni mbaya sana
 
Nililelewa na Mama wa kambo alikuwa mkali sana kitu kidogo tu napigwa,nikiagizwa kitu nimpelekee kama yupo jikoni basi nikimpa tu kama sijarudi nakofi nashukuru Mungu,kutokana na Woga nikawa kila akinituma kitu nimpelekee mikono ikawa inatetemeka haijiamini,kwahiyo mpaka Leo Nina tatizo hilo mikono inatetemeka muda mwingi japokuwa najitahidi kujicontrol watu wasinotice ,pia aliwahi kuniunguza na moto kwenye vidole vya mikono na miguu kwa kosa la kutokufunga bomba la chooni,kwasasa ni MTU mzima Nina kazi yangu nzuri sabab nilijitahidi kusoma ili nifaulu niende shule za mbali niepuke mateso yake,matokeo yake yeye ndo amekuwa tegemezi kwangu,kwani hakubarikiwa kupata Mtoto yoyote na najitahidi kumsaidia kadri ninavyoweza sababu nilikwishaamua kumsamehe!!
Duuu
 
Mimi mama yangu na baba yangu walikua wazima na walikua uwezo wakunilea. Sasa cjui kwanini walikua wananipeleka kwa watu tofauti tofauti. Mara mjomba, mama mdogo, binamu shanganzi. Mpaka namaliza la saba nililewa nawatu kama tisa. Nasijui kwanini nimimi tu maana nina ndugu zangu wengine wao walilewa nao. Sasa kitu ambacho kimeniathir kutokua na mapenzi ythati kwa mtu, hata mtu anipende vipi. Huwa namchukulia poua akiwemo mama yanga mme Wangu. Najaribu kuficha hii tabia watu wasigunduwe. Pia baba yangu kafa mwaka juzi ila hata tonne lachoozi hakuna. Watoto wangu najitahidi kuwapenda lakini bado. Maana hata apigwe na house girl naona tu poua. Au mtu akinumiza naona kawaida. Au kunisema vibaya sishituki wala kukasirika.
Dada angu hata mie Nina hilo tatizo, baada ya baba na mama kutengana nililelewa upande wa wajomba na nilikua napokea kipigo haswa sasa saiv Nina roho ngumu ajabu sina huruma hata kidogo kwa wazazi najitahidi lakini wapi?
 
wazazi wangu walinipelkea kwa ndugu kwa lengo la kusoma tution mzee wa ile familia akanibaka na kujaribu kueleza ndugu kwa namna ya kificho na kutoeleweka mabaya zaidi mama ndiyo alikuwa anasisitiza kila likizo niende kwa kisingizo sipendi shule aisee nikifika pale nakuwa kama changudoa nashikwa shikwa makalio na huyo mzee kama anavyotaka si nyonyo huku akinichonganisha kwa wazazi wangu hasa mdingi kuwa sipendi shule kazi yangu kuchekea wanaume , hapo mdingi kwenye swala la shule aisee hana utani .. niakosa wa kumueleza .. bahati nzuri kuna mama zangu wadogo nikajaribu kuwaambia kuwa yule mzee hafanyi fresha duh si wakamfuata acha nigeuziwe kibao kila mtu against me halooo.. nikajipiga ten kumueleza mkewe mama yangu wee kama nimemwagiwa mkaa petrol dadeki kikao semwa sana,.. madhara niliyoyapata nilikuwa mtuu wa kukaa peke yangu muda mwingi sababu kila nikikutana na mtu nasemwa,, hii tabia ikapelekea nikiwa form three kuanza kutumia pombe na sijui ili wazo lilitokea wapi na mpaka leo japo najaribu kupunguza pombe ndiyo kipenzi changu napo kuwa na stress.
pili siamini mtu yeyote duniani kila mtu namwona snitch tu sioni hatari kupoteza uhusiano kwa gharama zozote zile .

napata shida kuchangamana na watu hata mama yangu kipiga naye story hiyo habari sina ,, in short story na watu sina najiona kama hii hali inazidi kuwa mbaya ... naweza kukaa na watu na nikasiliza tu nisicoment chochote na nikaona fresh tu ....
fundisho: wazazi jaribu kuwapa nafasi ya kuwasikiliza watoto , wazazi wangu wangenisikiliza nisingekuwa hivi hii leo,, japo nalaumika huna ushirikiano na ndugu zako naanzaje ?
 
Kitu kinachoniumiza mpaka leo na kujiona tofauti na wengine ni kukosa mapenzi ya baba na mama ,maana walitengana ,nikaishi na mama tu ,baadae kuchukuliwa kulelewaa na bibi
Mpaka leo nikiona watoto au wadada wengine wakiishi na wazazi wao pamoja najiona kama sikupata bahati hivi na kujiona na kasoro,imenifanya sijiamini nikitembelea familia za wengine naona kama kwetu tuna kasoro
Ndugu wa mama kumuona mama yangu hafai ,,nami nishaacha kuwatembelea wala siwapigii simu kila mtu aishi kivyake,nishaona ndugu ni mama yangu na tuliozaliwa nao basi,,,

Ni mengi basi hatukustahili kufanyiwa tukiwa wadogo wanatuharibu sana akili
 
Niliwahi wenda kurina asali na mjomba angu, nikiwa na umri wa miak 12 tu porini mbali sana na tulitembea kwa zaidi ya masaa 16 kwa miguu, huko porini mjomba alipanda mtini na kuniacha peke yangu chini ilihali nikiwa ba umri huo mdogo na kuna wanyama wakali sana, sinto sahau na nakumbuka mpaka leo mjomba alinidhulumu mizinga yangu 11 niliyochonga huko msituni, nakumbuka tulikunywa maji yalichanganyika na kinyes cha wanyama , yaani shida kweli , leo Alhamdulillah ni boss napenda ma dream liners kama sio mimi wa ussoke, maisha safari ndefu sana , na Allah anajua hatma yetu despite shida za mapito
 
Kitu kinachoniumiza mpaka leo na kujiona tofauti na wengine ni kukosa mapenzi ya baba na mama ,maana walitengana ,nikaishi na mama tu ,baadae kuchukuliwa kulelewaa na bibi
Mpaka leo nikiona watoto au wadada wengine wakiishi na wazazi wao pamoja najiona kama sikupata bahati hivi na kujiona na kasoro,imenifanya sijiamini nikitembelea familia za wengine naona kama kwetu tuna kasoro
Ndugu wa mama kumuona mama yangu hafai ,,nami nishaacha kuwatembelea wala siwapigii simu kila mtu aishi kivyake,nishaona ndugu ni mama yangu na tuliozaliwa nao basi,,,

Ni mengi basi hatukustahili kufanyiwa tukiwa wadogo wanatuharibu sana akili
The very same story!!! Life jamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom