Usiji limit, binaadam tuna capacity kubwa sana na vya kuvifanyia homework ni vile usivyovijuwa tu, si vyote. Maana ikiwa mada zaidi ya 100 kama usemavyo na zote huzijui, itakuwa ni matatizo mazito.
Hii tabia ya homework ikilelewa humu watu watakuwa wanaweka heading tu,halafu tukafanye homework.
Mifano:
Ajali mbaya imetokea Singida,kwa taarifa kafanye homework.
Rais aongea na wakulima leo,kafanye homework.
Mada zote zikiwa za aina hii siku hiyo,wewe unayejua kila kitu niambie kama zinajitosheleza bila kufanya homework.
Wewe usiyeji-limit una muda wa kufanya homeworks 100 za aina hii kila siku?
Hata kama kutetea ni hobby,kuna vitu vingi tu vya kutetea siyo hili.
Nadhani solution kubwa ni kwenda kwenye hizo nchi na kujifunza wanachofanya na sisi tuje kufanya.
Wewe umewekewa majina ya nchi ambazo zinafanya vizuri katika utalii sasa ukitaka kuelewa zaidi kuwa zimefanya nini mpaka zikafaulu basi inabidi ukafanye homework yako.
Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
Ukitaka yote kijana inabidi uiname na kuupinda mgongo.
Akiri= Akili"UBABAISHAJI ni kitendo cha akiri ndogo kutaka kutawala akiri kubwa" hebu usilete ubabaishaji hapa, toa maoni yako sasa wafanye nini sio unakosoa tu
Una akili sana Bi mkubwa...yaani sijui kwanini watz ni wavivu sana kuchanganua mambo na kuzishuhulisha akili zetu.Kakuwekea majina ya nchi tatu, fanya homework yako kuzitazama zinafanya nini hasa ili ujifunze mbinu zao.
Mkuu The Boss kama wewe ni mfuatiliaji vizuri wa wizara hii utagundua kuwa Utalii wa Tz ulianza kuharibikia wakati wa Zakhia Meghji kutokana na poor advertisements haswa nje ya Tz,ni wakati ule ndio wakenya walitangaza huko uingereza na marekani kuwa the foot of Mt.Kilimanjaro is in Amboseli NP na mpaka leo vitabu vipo na vinasomwa dunia nzima.Wewe umenielewa mkuu
wakati fulani Zakhia Meghji aliwahi kuanzisha 'utalii wa ku target Rich class zaidi'
alipoondoka ikafa hiyo policy
sasa ni 'mass tourism' ambayo nayo hatujui tuifanyaje....mradi vurugu tu
mkuu umenikumbusha Dan hostel hapa Copenhagen na euro hostel HelsinkiThe Boss,
Asante kwa thread yako nzuri ambayo inamfanya mtu afikiri mara mbilimbili. Ni kweli uliyoyaandika.
Nchi hizo zote ulizozitangaza kuwa zina watalii wengi, zina vitu kadhaa vinalingana.
1. Mashirika ya ndege: Wote wana mashirika ya ndege na huyatumia zaidi mashirika yao makubwa ya ndege kutangaza Nchi na Miji yao na haswa sehemu ilipo HQ ya shirika la ndege hilo.
- Mfano mzuri ni Abu Dhabi. Hawa jamaa wamejitangaza sana kwenye mitandao na michezo kama kwenye Formula 1 ambapo ukiacha kuwa ni waandaaji wa mashindano hayo ambayo mwaka huu ndiyo yatafunga mwaka, pia walishajitangaza sana kwenye magari hayo kwa kuweka majina ya kampuni zao.
Abu Dhabi pia kwa kutumia jina la ETIHAD, wamekuwa wakijitangaza kwa njia nyingi hadi kufikia kuinunua timu ya Manchester City na uwanja kuuita Etihad ambayo kwa tafasiri ni UMOJA NA NGUVU (kama sikosei).
Pamoja na kujitangaza huko, Dubai ndiyo anasifika zaidi katika hizo EMIRATE saba zinazounda nchi ya UAE au Emirates (United Arab Emirates).
Ukiangalia sana utagundua kuwa Air EMIRATES ndiyo inachangia sana kukuwa kwa utalii huko
Ushahidi huu tutauona hivi karibuni baada ya ETIHAD nao kuanza kuwekeza kwa nguvu kwenye shirika lao la ndege la Etihad Airways. Hawa jamaa kwa sasa tayari wamevamia nchi nyingi za Asia, Ulaya na Africa. Kama wakijipanga vema basi Abu Dhabi itakuwa maarufu kama ilivyo Dubai, Istanbul(Inauzidi hata mji mkuu Ankara), Zurich(inauzidi pia mji mkuu) nk.
2. HOTELI za kitalii: Ukiacha kuwa na ndege nyingi ambazo zitafanya watu waje kwa wingi, Tanzania tunadhani kila Mtalii ni mtu tajiri. Tunadhani kuwa hotel za watalii ni zile za bei ya juu peke yake. Ukifika hata Berlin leo, kuna hostel za bei nafuu hadi chini ya Euro 30 kwa siku ila ndiyo utakuta watu ndani mnalala kama bweni yaani chumba kina vitanda vya ghorofa na ndani ya chumba kimoja waweza kukuta vitanda 2, 3,....8 nk.
Unavyojipanga kupokea Watalii basi fikiri sana hawa wa kima cha kati na chini kwani wao ndiyo wengi.
Hapa ndipo naona Abu Dhabi itamchukua muda kumfikia Dubai kwa watalii kwani Emir wa Dubai wamejipanga sana kimajengo na leo hii pale kuna hotel za bei ya $10,000 kwa siku hadi chini ya Us $30 kwa siku.
Kuwepo kwa hoteli za bei ya kati na chini huleta wimbi kubwa la watalii.
Sasa tuje kwa sisi Tanzania, hotel zetu nyingi zinalenga watu wenye kipato au akiba kubwa ya fedha. Zingelijengwa sehemu mbalimbali kama kulivyo nchi zinazoongoza kwa kitalii hoteli za bei tofauti huku ukiweka usalama wa kutosha kwa kila aina ya hoteli za watalii wanapofikia.
Pia kuanzishwa kwa shirika la ndege kubwa kwa Tanzania kutafanya wasafiri wengi kufika kwa kupenda au bila kupenda wakiwa safarini. Hao huwa watangazaji wazuri sana wa utalii kuliko hata ukiwapa Manchester City kuvaa jina la Tanzania kifuani. Ndege ni chombo ambacho unapotangaza Fly by AIR TANZANIA basi unatangaza shirika na nchi.
Wazo la Rais Magufuli kununua ndege na kuanzisha upya shirika la ndege ya Taifa, hata kama shirika linakuwa linaleta hasara, ila mwisho wa siku linatangaza utalii. Kenya ni mfano mdogo na hapo ndipo wanatuacha kwa mbaali ukiacha Ethiopia na South Africa.
Kutangaza utalii ni muhimu. Ila hiyo iwe kama nyongeza. Kama nchi inajipanga kutangaza utalii basi kabla haijaanza, tuanze kwanza kwenye hoteli za kima cha chini na cha kati kwa wingi na tumalizie kwenye shirika la ndege.
Kwa sasa nchi nyingi wanatumia pia APARTMENTS yaani mtu anakuwa kama yupo kwake kwani ile inakuwa nyumba ya mtu ya kupangisha kwa muda. Ndani unakuta kila kitu kwa mtu kuanza maisha. Wengine huweka hadi sukari na majani ya chai pamoja na kahawa.
Ila hiki ni kitengo cha watu binafsi ambacho sisi Watanzania tusaidie.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kuna nchi serikali zinawalipia wafanyakazi wa umma ku take vacations
tunaweza jifunza haya...kwa humu humu nchini
ikipitishwa sheria mfano kwa makampuni yenye uwezo
ya binafsi na ya umma kulipia utaali wa ndani wa wafanyakazi wao
tuta boost sana utalii wa ndani...
Toka sakata la Rose Odinga na Olduvai kitu kimoja nimegundua ni kuwa
watanzania wengi tuna tabia ya 'ujuaji' na 'kurahisisha mambo'
Ghafla kila mtanzania kawa 'mtaalamu' wa 'namna ya kutangaza nchi'
na kila mtu kuanzia wanasiasa hadi watu wa kawaida analaumu hiki na kile
ndo sababu nchi 'haitangazwi'
Nimemsikia Zitto akisema mifano ya ku promote 'ma star wetu' kina Samatta na wengine
ili 'eti kutangaza nchi' na hivyo kuvutia watalii
Wengine wakishauri watanzania wa nje wafanye hiki na kile....'eti kutangaza nchi'
Kuna maswali mepesi tu yanaweza kutusaidia kidogo...
tujiulize nchi kama tatu Dubai,Singapore na Malaysia ambazo zote
zinapokea watalii kwa mamilioni...zaidi ya milioni 20
kulinganisha na sisi tunaopokea watalii laki 8...
Je nchi hizo zina 'wasanii maarufu' au 'watu maarufu' wa nchi hizo
waliozitangaza?
unamjua msanii gani wa Dubai au Singapore?
Tukubali tu hili la kusema sijui tuwapromoti wasanii au watanzania wetu maarufu
ni 'kuhangaika tu' na 'tatizo la kujitangaza au kutangaza nchi..
Hivi Messi ni maarufu kiasi gani? mbona Argentina inaachwa na nchi hizo tatu
kwa idadi ya watalii kwa mbali?
Watalii wanao tembelea Argentina hawajawahi kufika milioni 6
na wala husikii sana wakisema sijui Messi atangaze nchi au kile au kile..
mwaka jana tu peke yake Utruki imepokea wataliii zaidi ya mara sita ya Argentina
na Urusi pia imepokea watalii wengi kuliko Brazil.Argentina na nchi nyingi tu...
Najaribu kusema tu kuwa 'kuna mbinu za kitaalam za kutangaza utalii'
na nchi zilizo fanikiwa kwenye utalii zimefanya 'yanayotakiwa' kufanywa
hadi zikafika hapo...
sio suala la kila mtu kuja na wazo lake tu...
'biashara ya utalii iko kuubwa sana'
na 'biashara ya kutangaza nchi zipate watalii' nayo ni kubwa kupita kiasi
yenye 'wanataaluma wake'
tukitaka kufika huko hakuna 'short cuts'
lazima tufanye hatua moja hadi 100.........Hata hao Wa Kenya tunaowaona 'wanatuzidi'
'wanacheza tu makida makida' kwenye utalii.....
tujifunze