Tuache ujinga wa kutaka kuifanya Dodoma iwe kama Dar!

Kumbe na wagogo mna asili ya ubishi?!!! Nilikua najua nyie asili yenu ni omba omba tu
 
Badala ya kutowa lawama kwanini usiwashauri waTanaznia wenzako waende Dodoma kujipatia kutokana na ukweli kuwa Dodoma kuna fursa nyingi?!
 
Ni vizuri leo nawe umeamua kushauri, naunga mkono hoja 100%...

Pia lazima uelewe jukumu letu kama watanzania ni kuona Tanzania ikipaa na kuwa moja ya super power Africa na dunia kiujumla. Pia tunahitaji watanzania wote au asilimia kubwa wawe na nguvu ya kiuchumi maana hili linawezekana kabisa...

Hatuhitaji kusifia watawala maana kutenda ni majukumu yao kazi yetu ni kuwasukuma watende kwa speed na nguvu kubwa, tunalipa kodi, tunafanya kazi kwa bidii...
 
Mbuyu ulianza kama mchicha Mkuu. Mji wa Mwanza si unaona ulivyojengeka? ulianza polepole sio fumba fumbua Dodoma iwe Dsm kamwe haiwezi kuwa ila Ramani ndiyo nyumba yenyewe Mkuu baada ya miaka itakuwa.
 
Badala ya kutowa lawama kwanini usiwashauri waTanaznia wenzako waende Dodoma kujipatia kutokana na ukweli kuwa Dodoma kuna fursa nyingi?!

Ni wapi nimetoa lawama? Nimetoa ushauri kwa jinsi nionavyo hali yetu halisi ya Kiuchumi kwamba hatuna uwezo ya kujenga Mji kama Jinsi watu wanavyofikiria, hivyo Dodoma jinsi ilivyo inatosha kabisa kuwa Mji mkuu wetu wa Utawala!
 
Mbuyu ulianza kama mchicha Mkuu. Mji wa Mwanza si unaona ulivyojengeka? ulianza polepole sio fumba fumbua Dodoma iwe Dsm kamwe haiwezi kuwa ila Ramani ndiyo nyumba yenyewe Mkuu baada ya miaka itakuwa.

Na hapo ndipo ninapotofautiana na wengi kwamba lengo lisiwe hilo kwamba Dododma uwe Mji mkubwa na uliojengeka kama Dar au Mwanza na zaidi, bali uwe tu Mji mdogo makao Makuu ya Utawala wa nchi yetu!
 
Kumbe na wagogo mna asili ya ubishi?!!! Nilikua najua nyie asili yenu ni omba omba tu

Mimi nipo Mwanza nimezaliwa DSM nimesoma Dodoma mpaka chuo sasa nina maisha yangu Mwanza. Dodoma ninaijua, Dsm Ninaijua na Mwanza pia.

So usijali sana Mkuu.
 
Mimi nipo Mwanza nimezaliwa DSM nimesoma Dodoma mpaka chuo sasa nina maisha yangu Mwanza. Dodoma ninaijua, Dsm Ninaijua na Mwanza pia.

So usijali sana Mkuu.
Punguza mihemko ya Dodoma sasa ingawa kuna wagogo walio zaliwa dar na kwa sasa wapo mwanza kama wewe
 
Dar bado sana!!! Ni jiji lkn bado halijapangiliwa au kupangika vizuri,

Inapaswa kuwepo na satellite city pembezoni mwa mji kama kibamba, boko. nk hii kweli itapendezesha jiji litaonekana kweli ni jiji kubwa.

Kwa sasa mwananchi wa kibamba analazimika kwenda Kariakoo au mlimani city kufanya manunuzi hii si swa kwa jiji.

Watu wa mipango miji haswa ktk wilaya mpya kama ya ubungo wapangilie
 
Na hapo ndipo ninapotofautiana na wengi kwamba lengo lisiwe hilo kwamba Dododma uwe Mji mkubwa na uliojengeka kama Dar au Mwanza na zaidi, bali uwe tu Mji mdogo makao Makuu ya Utawala wa nchi yetu!

Upo sawa Mkuu. Watu ninawashangaa kabisa. Kukua kwa miji na kuwa mikubwa si lazima nguvu ya serikali miji mingine inakuwa yenyewe kama Mwanza hakuna nguvu ya serikali hapa. kwa hiyo dodoma kama itakuwa mji mkubwa na ukue tu hofu na wasiwasi ni wa nini? Kwanza walisema haiwezekani na sasa wizara 1 na nyingine wiki hii inahamia dodoma tuwache kama utakuwa kama dsm good na kama sio basi utakuwa kwa kiwango chake.
 
Hujielewi unachozungumza wewe
 
Chuki zako na mkoa wa Dodoma bado hazijaisha?
Siwezi kuichukia sehemu ya nchi yangu ninachotofautiana nawewe ni kwamba hatuna uwezo wa kuijenga Dodoma tunayoitamani wakati Makusanyo yetu ni chini ya Trillion1 kwasasa na wage bill inachukua zaidi ya 70%, hapo bado hujatoa pesa ya matumizi ya kawaida ya nchi nzima yaani OC. Usisahau kwamba tukikopa pesa ya kujenga Reli ya standadigeji tutakua tumeisha chakachua uwezo wetu wa kukopa tena, maana tunachechemea sana katika eneo hili. Kwa uchumi wetu jinsi ulivyo kuijenga Dodoma ni kuchezea pesa, kuna maeneo ya kuyajenga ambayo kweli yana faida kiuchumi kwasasa. by the way ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa pale Chato unaendeleaje? maana pale napo kuna watu wanasema pana tija kuwekeza billions of money
 
Mkuu nahisi hiyo article hata hujaisoma umekurupuka tu kuanzisha uzi.
Article yenyewe inamnukuu jamaa akisema hatutaki Dodoma ije kuwa kama Dar.
Na pia kakwambia bani wanaenda kujenga skyscrapers huko? Dodoma mwisho floor 5 hawaruhusu majengo marefu zaidi ya hapo i think
 
Kuongea kitu usichokijua ni kulimbikiza ujinga!! Dodoma haiwezi kuwa kama Dsm lakini Dodoma ni mkoa ulio planned zaidi ya Dsm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…