Tuache maigizo Magazetini, utakamata vipi makontena ambayo yametunzwa hapo kihalali?

Sasa wewe unachotea hapa ni nini?????.......Mbna watanzania sisi ni watu wa ajabu sana????....
Hivi kwa akili yako kabsa unadhani hao WAZUNGU hawatuibii dhahabu zetu???

Ni kweli wazungu wanatuibia, lakini kusema kwamba hayo macontainer yamekamatwa ni upotoshaji na kutafuta kick za kishamba, maana yalikuwa sehemu sahihi na yalifuata njia zote sahihi kuwa hapo yalipokutwa. Wangesema hayo macontainer yanachunguzwa kilicho ndani ingeeleweka na sio kukamatwa.
 
Sasa wewe unachotea hapa ni nini?????.......Mbna watanzania sisi ni watu wa ajabu sana????....
Hivi kwa akili yako kabsa unadhani hao WAZUNGU hawatuibii dhahabu zetu???
Kuhusu kuiba au kutokuiba hilo sijui wanajua wahusika maana serikali ina vyombo husika. maana sijui wanaiba vipi hadi serikali au Wabunge au watu wenye weledi watueleze humu. Ila kama wewe ulikuwa umelima matikiti kisha serikali ikakataza biashara ya matikiti wakati wewe upo na fuso kariakoo. Kesho aje mtu aseme amekamata matikiti yaliyozuiwa kwenye fuso kariakoo wakati iko wazi wakati tunakataza Kuna matikiti yalikuwa shambani, sokoni, njiani, kwenye maghala na pengine yanapakuliwa. Na Pote walitii na kusimamisha....

Kama wanaiba sio tu wazuiwe Bali washtakiwe watulipe fidia. Ila kote haki itendeke na kwa sababu hii ni biashara ya dunia na hata dunia itatuunga mkono ila sio kwa hicho cha Jana. Bado tutasubiri serikali yetu ifuatilie na kutueleza ukweli.
 
Yote hayo uliyo andikwa inawezekana yanatekelezwa, ila kunawatuwamewekwa pale bandarini kunusanusa, na haio ndio walio toa iyo taarifa kwamba uwo mzigo japo una vibalivyote ila tumeibiwa.Ndio maana JPM aliwaweka wamsaidie kunusanusa.
 
Swali langu ni hivi... Kitu kikikamatwa ambacho kipo kinyume cha sheria ina maana hakitakua na nyaraka halali au seal za kutoka mamlaka husika yenyewe dhama ya kufanya hivyo... Lakini yale yalikuwa na seal za TRA...


Sawa yamekamatwa... Kama hayapo hapo kihalali kwa nini yasivunjwe na kufunguliwa?


Just thinking loud....
 
Yote hayo uliyo andikwa inawezekana yanatekelezwa, ila kunawatuwamewekwa pale bandarini kunusanusa, na haio ndio walio toa iyo taarifa kwamba uwo mzigo japo una vibalivyote ila tumeibiwa.Ndio maana JPM aliwaweka wamsaidie kunusanusa.
Kweli mkuu wanatakiwa wawe smart enough kutujulisha wananchi vitu vya kueleweka ili tupate ground Nzuri ya kusifia. Ingetokea imekamatwa meli inatoweka bandarini Jana katika ya ban, hapo tungesifia saana na nadhani hao wenye madini wangefukuzwa kabisa mkuu...
 
Sasa wewe unachotea hapa ni nini?????.......Mbna watanzania sisi ni watu wa ajabu sana????....
Hivi kwa akili yako kabsa unadhani hao WAZUNGU hawatuibii dhahabu zetu???
Je ktk mikataba waliosainiana kipengele cha usafirishaji wa mchanga kikoje? Wamekiuka? Kama wazungu ni wezi na nyie kwa nn mnaficha mikataba isijulikane kwa wote? Sio kulaumu eti wazungu ni wezi! Inshu ni usimamizi mbovu, na rushwa kwa baadhi ya watendaji serekàlini"
Lakini la maana hapa ni kuelewa kuwa smelta zinazochakata huo mchanga kwa hapa afrika hatuna hata moja, duniani zipo kwenye nchi 3 au 4 tu, kama yamelipiwa kodi halali wacha wapige kazi au tuuchukue tukaumwage chato. Tuwakomoe!
 
Sasa wewe unachotea hapa ni nini?????.......Mbna watanzania sisi ni watu wa ajabu sana????....
Hivi kwa akili yako kabsa unadhani hao WAZUNGU hawatuibii dhahabu zetu???
Leseni ya uchimbaji walipaje?
Kama wanatuibia tuchimbe wenyewe

Hujui kilichopo ardhini wee komaa n kodi wanayokupa.
Kama unahis mkeo anadokoa nyam jikoni.... Ingia upike mwenyewe
 
Huwezi kusafirisha madini bila kibari kutoka wizara ya nishati na madini,na kisha lazima kisainiwe na afisa madini wa kanda ambayo madini hayo yametoka,na unapo pita barabarani kuna check point ambazo wanakagua vibari vya madini yote mpaka mchanga,na huwezi ingiza mzigo bandarin bila document halali za mzigo husika,na kabla mzigo hauja safirishwa lazima tra waje wafanye makadirio ya kodi yao kisha ulipie,ndio utaratibu wa kusafirisha huanza,na ifahamike mzigo bandaran hausafirishwi kama matenga ya kuku,lazima ufanye booking kwenye shipping line na wakupe muda wa kusubir meli,kwaiyo huo mzigo inawezekana upo hapo bandarin kabla zuio halija tolewa,na tra tayar wamesha chukua chao ndio maana wakaweka seal.
Mkuu ndio maana magazeti ya English hawajaiandika au wameandika kwa umakini. Tunapopinga uchochezi wa magazeti haya ya kiswahili pia inabidi watupe taarifa safi sio zenye mkanganyiko hata wakisoma watu wa nje wanatuona tunalishwa makapi.
Uchambuzi wako nimeusoma sana...
 
Hujawai kuona mizigo imelipiwa kodi na inazuiwa?iinatokana na baadhi ya watendaji kutokua waaminifu.Ndio maana ata pale bandarini kuna security camera kama watendaji wangekuaxwazalendo zisingewekwa.
 
Tatizo elimu elimu elimu waandishi hata kuhoji tu unashindwa hayo ni maigizo tu yote nikutaka kuwekwa mbele ya magazeti akuna hatua yoyote hii nchi itakayopiga muda ndio msema kweli atabakia kumalizia viporo vya jk kama ilo daraja la magari kupita juu na miradi mingine lakini jipya hakuna
 
Magazeti yetu nayo yaanze kufanya mambo kisomi. Baada yule jamaa Jana kutumia lugha wamekamata kila anayejua na mwenye idea kidogo ya mchakato mzima wa usafirishaji wa hayo madini yanayokwenda kuchenjuliwa ujerumani /Japan /China alishangaa.

Nilitegemea hata waandishi nao waumize kichwa kidogo naona nao wameanguka humohumo.
Inashangaza kutumia lugha ya kukamata kitu ambacho kimelipiwa kodi, kitu ambacho, kilikuwa kiko katika safari halali kabla ya katazo la mkuu wa nchi. Hivi hawa wawekezaji wakiitangazia dunia uhalisia Nani atapenda kuja kuwekeza katika mazingira ya fitna kama haya.
Nilitegemea kusikia serikali imegundua madini zaidi ya hayo walioandikishana ndani ya makontena yaani gold, copper na silver ili wananchi tushirikiane kumsurubu muwekezaji dhalimu badala yake wanaleta vitu vya visivyo na mashiko.

Tuliite koleo koleo na sio kijiko.
Magazeti nayo mnashangaza sana..tangu muambiwe kuandika habari nzuri kwa taifa, mmejitoa ufahamu hata hamchuji cha kuandika.

Ina maana mmepoteana kiasi hicho?
 
Mkurugenzi wa bandari anasema walipewa taarifa ya kuwapo makasha 20 tu. Baada yakufanya uchunguzi wao wakayakuta 262. Hapa kwa nini wasiseme wamekamata? Wenye mzigo walificha taarifa japo makasha hayo yalifuata taratibu kufika pale. Lengo lao la kutokutoa taarifa awali ni nini?
Kweli hupendi yanayofanywa na serikali hii. Huo ni uhuru wako. Lakini hiki cha kushupaa kupotosha hali halisi kwa malengo yako si sawa na hakileti maendeleo.
 
Hivi hii wizara haina waziri? Na kama yupo yeye anafanya nini? Na kwaninii wizara hii isirudi kwa raisi ambaye anaonekana kuipenda sana na ndicho anachoweza zaidi? Au kwa sababu bandari ipo karibu na magogoni? Akikosa usingizi anakwenda kuvizia mizoga pale? Au ndiyo wizara ya kuombea huruma za wananchi? Au hapo ndipo walipo wapiga kura wengi? Au,......au....
 
f1937462076cf2eef53249045d5b35ef.jpg
 
Ndo maana alisema " watu wa vijijini ndo wanamuelewa sana" kwa sasa wa mjini ni vigumu sana kumuelewa jpm.
 
Back
Top Bottom