Tuache maigizo Magazetini, utakamata vipi makontena ambayo yametunzwa hapo kihalali?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Magazeti yetu nayo yaanze kufanya mambo kisomi. Baada yule jamaa Jana kutumia lugha wamekamata kila anayejua na mwenye idea kidogo ya mchakato mzima wa usafirishaji wa hayo madini yanayokwenda kuchenjuliwa ujerumani /Japan /China alishangaa.

Nilitegemea hata waandishi nao waumize kichwa kidogo naona nao wameanguka humohumo.
Inashangaza kutumia lugha ya kukamata kitu ambacho kimelipiwa kodi, kitu ambacho, kilikuwa kiko katika safari halali kabla ya katazo la mkuu wa nchi. Hivi hawa wawekezaji wakiitangazia dunia uhalisia Nani atapenda kuja kuwekeza katika mazingira ya fitna kama haya.
Nilitegemea kusikia serikali imegundua madini zaidi ya hayo walioandikishana ndani ya makontena yaani gold, copper na silver ili wananchi tushirikiane kumsurubu muwekezaji dhalimu badala yake wanaleta vitu vya visivyo na mashiko.

Tuliite koleo koleo na sio kijiko.
 

Attachments

  • 20170326_045929.jpg
    41.8 KB · Views: 64
Tuna waandishi wakibashite sana.
Makontena yapo wiki kadhaa hapo bandari Kavu, kila kitu kikiwa halali na wazi kabisa, tatizo pekee lililoibuka ni kauli ya Rais kuzuia ghafla usafirishaji wa hayo makontena kwenda nje ya nchi.
Sasa ghafla watu wanakuja na kusema wamekamata Makontena!!!
Haya ni maigizo sawa sawa na yale ya kukamata Sukari, Viroba.
 
Sasa wewe unachotea hapa ni nini?????.......Mbna watanzania sisi ni watu wa ajabu sana????....
Hivi kwa akili yako kabsa unadhani hao WAZUNGU hawatuibii dhahabu zetu???

Kichwa Maandazi kweli wewe

CCM na Serikali yao ndio walisaini mikataba feki

Pili: Tunaongelea habari inavyotolewa....Soma comment za wengine...wameelezea

Tatu: China na CCM wana Harusi ya kuwaibia Tanzania ili China iwasaidie CCM kuiba kura na kubaki madarakani

Rejea Bomba la gesi na gharama zake...Wachina wezi
 
Huwezi kusafirisha madini bila kibari kutoka wizara ya nishati na madini,na kisha lazima kisainiwe na afisa madini wa kanda ambayo madini hayo yametoka,na unapo pita barabarani kuna check point ambazo wanakagua vibari vya madini yote mpaka mchanga,na huwezi ingiza mzigo bandarin bila document halali za mzigo husika,na kabla mzigo hauja safirishwa lazima tra waje wafanye makadirio ya kodi yao kisha ulipie,ndio utaratibu wa kusafirisha huanza,na ifahamike mzigo bandaran hausafirishwi kama matenga ya kuku,lazima ufanye booking kwenye shipping line na wakupe muda wa kusubir meli,kwaiyo huo mzigo inawezekana upo hapo bandarin kabla zuio halija tolewa,na tra tayar wamesha chukua chao ndio maana wakaweka seal.
 
Izo taratibu ili mzigousafiri ndio zimesitishwa, kwasasa iyo mizigo ipokwenye kundi la kuzuiwa kusafiri na si kusafirishwa. Kwahiyo mizigo imezuiwa/ kamatwa.
 

Bravo

Excellent Explanation
 
Izo taratibu ili mzigousafiri ndio zimesitishwa, kwasasa iyo mizigo ipokwenye kundi la kuzuiwa kusafiri na si kusafirishwa. Kwahiyo mizigo imezuiwa/ kamatwa.

Wewe, acha kukurupuka

Mizigo ilishafika Bandarini kabla ya Katazo la Rais na TRA walishachukua kodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…