Trump ashinda tena Nevada, aelekea kuteuliwa Republican

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,597
1,072
Donald Trump ameshinda tena katika jimbo la Nevada. Ni mfulilizo wa kushinda katika majimbo matatu na hivyo kuwa kidedea kwa chama chake cha Republicans akiashiria kuteuliwa na chama hicho kuwa mgombea wake wa kiti cha uraisi.

Source: CNN
 

(CNN)— It's over. Donald Trump is the Republican nominee.

He just added Nevada to the growing list of caucus primary wins, and while he needs more delegates to clinch it, who the heck can stop him now?

He is leading in national polls and in many state polls; he's succeeded in upending rivals such as Ted Cruz, Jeb Bush and Ben Carson; and there's no one in sight who can stop him. The only question is when will the GOP embrace him?

The answer: no time soon.
 
Hilary atachukua nchi kirahisi kabisa ..... zamu ya mwanamke kutawala USA sasa.... huwez tukana baadhi ya makundi USA ukapata uraisi.... kama wa chicano, blacks, muslims na sasa wakatoliki watakupa kisogo basi ujue huwez kaa ushinde uraisi maana jamii yao inategemeana.... wale pro Trump kuna baadhi watagoma kumpigia sbb ya matamshi yake..... japo li Trump lingeweza
tunyooshea hawa fisi wetu wa africa wanao itisha uchaguzi wa kidemokrasia huku wameshikilia bunduki mkononi mwao kumpiga yeyote atakae wakaribia/ wapinga..... but sorry the guy is so
arrogant....
 
Acha kuuma na kupuliza,wewe si shabiki wa Trump isipokuwa ushaona upepo wa Trump kuukwaa uraisi uko 85%. Wamarekani si kama siasa za CCM za kuzushia watu ugaidi na ukabila ili washinde.
 

 
Nina uhakika Trump hatafanya yale anayoyasema.

Urais wa Marekani ni zaidi ya kuamua. Kutakuwa na watu wengi sana wanaomuongoza.
 
Donald Trump, mgombea wa urais kwa tiketi ya Republican amezidi kujiwekea mazingira mazuri ya kuipeperusha bendera ya Republican katika kinyang'anyiro cha Urais baada ya kujizolea ushindi wa pointi 45 katika jimbo la Nevada na kuwaacha mbali kwa zaidi ya pointi 20 wapinzani wake Marco Rubio mwenyeji wa jimbo la Florida na Tedd Cruz mwenyeji wa jimbo la Texas.
"Tutashangilia kwa muda mrefu usiku kucha", amenena Trump huku akiwa anashangiliwa na wafuasi wake.


DONALD TRUMP AKISHEREHEKEA PAMOJA NA DONALD TRUMP JUNIOR (KUSHOTO) NA ERIC TRUMP (KULIA) HUKO LAS VEGAS, NEVADA.

Kura zilikuwa nyingi huku baadhi ya vituo vikiripotiwa kupungukiwa karatasi za kupigia kura kabla ya tatizo hilo kurekebishwa. Trump aliyeamua kutowekeza kampeni zake kwa raia wenye asili ya Uhispania kutokana na sera yake kuntu ya masuala ya uhamiaji, amepata Uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa raia wenye asili ya ufilipino.
Katika hotuba yake baada ya ushindi, Mkwasi huyo ametanabaisha kwamba awali kuna mdhamini alitaka ajitolee dola za Marekani milioni kumi, lakini alikataa kwa kuwa anajidhamini katika kampeni zake.
Donald Trump amezidi kujiongezea umaarufu katika makundi mbalimbali ya wapiga kura kutokana na misimamo yake ya kuweka Uzalendo na Ukweli mbele hata kama baadhi wanaumizwa na ukweli huo. Ahadi yake ya kulifanya taifa la Marekani kuwa taifa kubwa kwa mara nyingine duniani, imeaminiwa na umma kwa asilimia kubwa.
Hii yaweza kuwa habari mbaya kwa Rais Museveni, Robert Mugabe pamoja na makundi ya itikadi kali duniani kwa maana Trump ametangaza vita dhidi ya makundi hayo.


 
pale marekani hakuna urais wa zamu kama wa ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…