TRA yavuka lengo la ukasanyaji kodi kwa mwaka wa fedha 2015/2016, wazungumzia mapato ya bandari

kivipi weka mapato ya Kikwete na mapato mwinyi mkapa na magufuli tuone.

CQnPIquVAAEYPiY.jpg


swissme
 
Yamepanda kutoka shilingi trilioni 1.31 mwezi Mei hadi shilingi trilioni 1.41 Juni. Hongera sana TRA
Hiyo pesa gawanya kwa 2250 ya dola Leo. Tafuta bei ya dola mwezi juni mwaka Jana, halafu tafakari
 
Yamepanda kutoka shilingi trilioni 1.31 mwezi Mei hadi shilingi trilioni 1.41 Juni. Hongera sana TRA
siku hizi unashinda mitandaoni ili na wewe uchaguliwe kama wenzako lakini wewe elimu yako ni form 4 pale mazengo laki unaweza pata bahati maana magu uchagua watu wasio na vision kama wewe jitahidi.
swissme
 
Naomba taarifa ya TRA. Sihitaji maneno matupu.
Dah! Mkuu? Kwani unatumia kifaa cha aina gani? Mbona link ipo hapo juu unaweza kujipakulia mwenyewe? Haya soma basi hapa chini

IN SUMMARY
Kidata alisema hayo jana baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutoa taarifa kuhusu kushuka kwa zaidi ya asilimia 50 mizigo inayosafirishwa kwenda nchi jirani za DR Congo na Zambia.

Dar es Salaam. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema mapato katika Bandari ya Dar es Salaam yameongezeka katika miezi miwili iliyopita licha ya mizigo inayopitia hapo kupungua.

Kidata alisema hayo jana baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kutoa taarifa kuhusu kushuka kwa zaidi ya asilimia 50 mizigo inayosafirishwa kwenda nchi jirani za DR Congo na Zambia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Kidata alitaja sababu za kupungua kwa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kuwa ni matatizo yaliyopo duniani kote yakichagizwa na kuyumba kwa uchumi wa China hivyo siyo Tanzania pekee iliyoathirika.

Kamishna huyo alisema utafiti walioufanya umebainisha kwamba mizigo imepungua pia katika Bandari za Mombasa, Beira na Durban ya Afrika Kusini. Hata hivyo, alisisitiza kuwa licha ya kupungua kwa mizigo, mapato ya bandarini yameongezeka kwa sababu wameziba mianya ya uingizaji mizigo kwa njia zisizo rasmi na wamejipanga vema kuhakikisha mizigo yote inapita bandarini na kulipiwa kodi stahiki.

“Ni kweli mizigo imepungua bandarini lakini siyo nchini kwetu pekee, hata bandari nyingine. Hapa kwetu limekuwa likizungumzwa sana. China ni nchi kubwa na ya pili kiuchumi duniani, na ndiyo inayoongoza kwa kusafirisha mizigo, wao wameyumba kidogo, hivyo wakapunguza kusafirisha. Lazima na sisi huku tutaathirika pia,” alisema.

Kamishna huyo alisema walikuwa wakikusanya Sh200 bilioni hadi Sh300 bilioni kwa mwezi kutoka katika bandari hiyo lakini baada ya kudhibiti mianya ya uingizaji mizigo, Aprili walikusanya Sh458 bilioni na Juni walikusanya Sh517 bilioni.

Na kuhusu makusanyo ya jumla ya TRA, Kidata alisema kwa Juni makusanyo yameongezeka kufikia Sh1.41 trilioni kutoka lengo la Sh1.31 trilioni. Vilevile, alisema makusanyo kwa mwaka uliokwisha pia yameongezeka kwa wastani wa asilimia 100.04 hadi kufikia Sh13.37 trilioni badala ya Sh13.31 trilioni ya lengo.

Aprili 2, mwaka huu wakati akifunga warsha ya Wahariri wa Habari, Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga alisema kwamba mizigo inayokwenda katika nchi hizo inapitia Bandari ya Beira, Msumbiji.

Mhanga alionyesha hofu yake kwamba huenda hali ikawa mbaya zaidi kwa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli ya kisasa inayoanzia katika Bandari ya Mombasa (Kenya) mpaka DR Congo, kwa kuwa itaongeza unafuu wa usafirishaji wa mizigo katika bandari hiyo shindani kwa Tanzania.

Aidha, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alilieleza Bunge Aprili kuwa kutoka Oktoba 2015 hadi Machi mwaka huu mizigo ilikuwa ikipungua bandarini huku makontena kutoka nchini Congo yakishuka hadi kufikia makontena 4,092 kutoka makontena 5, 529.

Dk Mpango alieleza kuwa mizigo ya kwenda Malawi ilishuka kutoka makontena 337 hadi 265, huku yale Zambia yakishuka kutoka makontena 6,859 hadi kufikia 4,448.

Akifafanua kuhusu kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mizigo, Mtafiti Mwandamizi Mkuu wa TRA, Beldon Chaula alisema Sheria ya VAT hairuhusu mizigo ya kimataifa kutozwa kodi isipokuwa kwa huduma nyingine zitakazofanyika hapa nchini.

Alisema mizigo yote inayosafirishwa ndani ya nchi na kutumiwa ndani, itatozwa kodi ya VAT kama ilivyo kwa bidhaa nyingine. Alisisitiza kwamba hiyo siyo sababu ya kupungua kwa mizigo bandarini kwa sababu mizigo inayotoka nje na inayokwenda nje hailipiwi kodi.

“Mizigo inayotoka nje kwenda bandarini hailipiwi kodi isipokuwa huduma nyingine kama kupakia mizigo, kushusha mizigo au kuhifadhi mizigo ndizo zinatozwa kodi ya VAT,” alisema Chaula.

Kamishna wa Mapato ya Ndani, Elijah Mwandumbya alisema wamejipanga kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wote wanatumia mashine za kielektroniki za EFD na kwamba watapita sehemu mbalimbali kuhakiki kama wanatumia mashine hizo au la.
 
siku hizi unashinda mitandaoni ili na wewe uchaguliwe kama wenzako lakini wewe elimu yako ni form 4 pale mazengo laki unaweza pata bahati maana magu uchagua watu wasio na vision kama wewe jitahidi.
swissme
Mkuu, umenisahau nini? Mbona siku zote tangu 2013 nipo mitandaoni?
 
Mkuu, umenisahau nini? Mbona siku zote tangu 2013 nipo mitandaoni?
jipendekeze elimu yako ya form 4 pale Mazengo ndio inakuaribia unaweza pata bahati maana magu uchagua watu wasio na vision kama wewe jitahidi

swissme
 
Hawasemi kuwa walikopa kwa wafanyabiashara bil 300 kuongezea mapato mwezi uliopita!
 
Hizo takwimi za kwenye magazeti sisi hatuzitaki tunataka kuona maisha yanachange.
 
Back
Top Bottom