TRA yavuka lengo la ukasanyaji kodi kwa mwaka wa fedha 2015/2016, wazungumzia mapato ya bandari

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969

Mamlaka ya mapato Tanzania imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2015/2016 kwa kukusanya kodi ya shilingi trilioni 13.371 sawa na asilimia 100.04% ya lengo lilipoangiwa na serikali kwa Tanzania bara na Zanzibar
Kamishna wa mapato Tanzania amesema mapato hayo ni ongezeko la asilimia 23.70 ukilinganisha na mapato ya mwaka wa fedha 2014/2015
Akizungumzia suala la bandari amesema pamoja na mizigo kupunga bado wanakusanya kodi kubwa ya zaidi ya bilioni 400 hadi 500 kwa mwezi ukilinganisha na wastani wa bilioni 200 hadi 300 kwa mwezi waliokuwa wanakusanya kabla na sasa bandari haitumiki kama uchochoro wa kupitishia bidhaa kama ilivyokuwa mwanzo
Pia wamezungumzia suala la kodi ya VAT na kusema kodi hiyo itakatwa kwa watoa huduma na sio wananchi
 
Kwa lugha rahisi TRA wamekiri wazi tena hadharani kwamba, Bandari ya Daresalama ilikua ikitumia kama uchochoro kwa wakwepa kodi na wapiga kodi. Na hilo ongezeko la sasa pia lilikua likiliwa na wajanja wachache kwa miaka yooote toka kwa shamba la Bibi.
Baba Janeti please weka hawa watu nyuma ya nondo, na kisha wafikishwe mahakamani wahusika wote watakao bainika aiseeee...
 
Hayo mapato ya mwaka 2014/2015 kuyashinda ya mwaka juu 2015/2016 yamezingatia thamani ya dola au shilingi yetu?
Maana 1000 ya mwaka jana naona ni sawa na 1300 ya sasaa
 
Sasa hela zaenda wapi maana hakuna hela
Kwa huo wastani je bajeti yetu hii itatekelezwa?
 
Hao wanaweweseka wenyewe! Mara Bandari mara TRA mara watasema TCRA! Shauri yao sisi tunajua mapato yameshuka! Wamekubali meli zimepungua na mizigo hamna! Sasa mapato yameongezeka maruhani? Au? Waache upuuzi wao!! Hakuna kitu hapo!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…