TRA yakusanya Trilioni 7.27 kwa kipindi cha miezi 6

Naona Kuna watu hawajafurahishwa na hii taarifa ususani wale wanaofikiria kuferi kwa serikali ya CCM.. Basi wahathirika ni wamalawi
 
Watanzani bana yani mnasikitisha,elimu yenu ndogo ndio maana ccm wanatumia mwanya kuwalaghai,
Hakuna cha makusanyo ya matilioni wala nini,ni mbinu ya serikali kuwaondoa kwenye mjadala wa njaa,TRA inatumika tu kutuondoa ili tujadili makusanyo na tusahau mijadala ya njaa,shame on u ccm.
 
Wanazipeleka wapi sasa?
 
Kama kuna moto wa jehamamu kayombo anastahili kwa kutoa kwa maksudi takwimu za uwongo kuogopa kutumbuliwa. Analeta hadithi ya mapato fake
 
[UOTE="ishiveti, post: 19341882, member: 293312"]hivi na faini za magari zinaingiaga humu au,,,naomba kueleweshwa[/QUOTE]Q

huwa ni kodi tu ndugu, faini haziingii kabisa labda hizi za kuchelewa kulipia ada ya mwaka ya gari, kuchelewa kuwasilisha ritani na kulipa kodi stahiki N.K. faini za barabarani za Traffic haziingii.
 
Halafu wanang'ang'ana kukopa 2.1 Trilion ili iweje ? Hawajanipata hata kwa bunduki .
 
mm huwa sikubaliani na hiyo logic ya kupika data, maana namba hazidanganyi hata kidogo, yani wakidanganya ni shida kwao zaidi.
m naona wamepiga kazi sana coz mim binafsi sikutegemea kama wangefikia hapo. Wenzetu wakifanya kazi nzuri tuwapongeze jmn sio kila kitu kuwa negative tu coz wakikusanya kidogo bado hasara ipo kwetu.
NAMBA HAZIDANGANYI.....HAWAWEZI KUFODGE DATA.
 
Tofauti ya Decemba 2016 na December 2015 ni ndogo...inaonyesha December ni mwezi wa mapato kwa TRA sijui sababu...maana 2015 ilikuwa 1.4 na 2016 1.4
 
Watadanganya vipi wakati bunge litajadili mapato na matumizi?
 
Ongezeko si la kuridhisha ukitilia maanani kuwa kwa sasa TRA inakusanya kodi ya majengo ambayo ilikuwa inakusanywa na halmashauri za miji na majiji. Vile vile ukilinganisha na budget iliyopitishwa kuna gap kubwa mno. Serekali inatakiwa kujipanga upya na kuacha matamko yasiyowapa confidence wafanya biashara wa ndani na nje. Vile vile washirika wetu wa maendeleo siyo watu wa kubeza kwa vile kiwango chetu cha utegemezi hakiwezi kuisha kwa usiku mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…