TRA, TAKUKURU wamtaja anayeiba mil7-8 kila dakika, huyu hapa..

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hatimaye wametaja mfanyabiashara ambaye alibainishwa na Rais John Magufuli katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Ikulu Dar es Salaam juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Mohammed Mustafa Yusuf Ali anayetuhumiwa kuiibia Serikali matrilioni ya shilingi kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti bandia.

Alisema TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya Sh 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa serikalini na makampuni hayo kwa kipindi hicho.

Alisema kwa sasa wanaendelea na mahojiano naye zaidi ili kuwabaini wote wanaohusika na mfumo huo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA, Alfayo Kidata aliyeambatana na Mlowola katika mkutano huo wa waandishi wa habari, makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za EFDs ambazo hazijasajiliwa.

“Makampuni hayo wakishanunua risiti za manunuzi bandia, hatimaye huzitumia risiti hizo kudai marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na mhusika, kitendo ambacho kinainyima serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya Sh 10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 16,425,703,824 kwa kipindi hicho.

Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited ambayo tangu mwaka 2010 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,930,170,573 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 10,878,564,089.

Pia imo kampuni ya A.M.Steel & Iron Mills Limited ambayo kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 79,016,112 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 131,693,518 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 210,709,630.

Kampuni nyingine ni A.M Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa VAT ya Sh 638,221,034.80 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 1,063,701,724. 00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 1,701,922,758.00.

Alisema baada ya kubaini ukwepaji kodi huo kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya VAT yasiyostahili kwa kuwa mamlaka imejizatiti kuendelea kuwabaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki.

Aidha alisema uchunguzi wa awali pia umebaini kuwepo makampuni hewa 228 na kusisitiza kwamba wameusimamisha mfumo huo bandia na kutoa siku tatu kwa kampuni zote zinazodaiwa kulipa fedha hizo.

“Hakuna yeyote anayekwepa kodi atasalimika, wote ni lazima walipe na sasa tumedhibiti mfumo huo bandia,” alisema.

Juzi Magufuli akizungumza na Ma RC na Ma DC wapya, aliwataka wakasimamie vyema mapato katika maeneo yao kwani kumekuwepo na baadhi ya watu wajanja wanaotumia vibaya taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) TRA kujinufaisha wenyewe na kuliingizia taifa hasara.

Alisema: “Tulikuwa tunafuatilia mashine za EFDs zinazokusanya mapato, yupo mtu mmoja alitengeneza kampuni nyingi zilizokuwa zikimlipa asilimia tano ya VAT na yeye anacheza na TRA halipi asilimia 18 ya kodi hiyo. Alikuwa anaingiza kati ya shilingi milioni saba mpaka nane kwa dakika. Serikali ilipoteza matrilioni ya fedha. Huyu mtu yupo kwenye mikono salama.

Source. Mpekuzi Blog

Katika utawala wa Kikwete majambazi wengi sana walishika sekya nyeti na kufanya maujanja bila kuchukuliwa hatua yeyote. Usikute huyu ni rafiki na Riz alikuwa recruited kuiba for his dad. Jamani tunahitaji Kikwete na Mkapa kuhukumiwa na kutaifishwa.
 
Hizi ni sawa na igizo la LUGUMI,limeisha wanatuwekea SANTULI nyingine,na tulivyo nyumbu tumesahau leoleo Tz ni nchi ya ajabu sana na watu wake.
Kumbe mnajijuwa kuwa ni nyumbu, acheni unyumbu mje kwa hapa kazi tu.
 
Huyu haina haja ya kuzungushana wakati watanzania wanaumia harudishe pesa zetu
Halafu apigwe ndani mvua 20 hadi 30 za mahakama ya mafisadi amabyo inaanza leo. Hii ni baada ya kurudisha pesa zetu na kutaifishwa mali zake. TRA watumie kale kaformula kao kukokotoa malimbikizo ya kodi tangia alipoanza kuiba. Yaani hatabaki na mali huyo.
 
Walivyoimba CCM mbele kwa mbele kisha Magufuli akabaki akisisitiza HAPA KAZI TU nadhani hawakumwelewa.
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hatimaye wametaja mfanyabiashara ambaye alibainishwa na Rais John Magufuli katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Ikulu Dar es Salaam juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Mohammed Mustafa Yusuf Ali anayetuhumiwa kuiibia Serikali matrilioni ya shilingi kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti bandia.

Alisema TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya Sh 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa serikalini na makampuni hayo kwa kipindi hicho.

Alisema kwa sasa wanaendelea na mahojiano naye zaidi ili kuwabaini wote wanaohusika na mfumo huo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA, Alfayo Kidata aliyeambatana na Mlowola katika mkutano huo wa waandishi wa habari, makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za EFDs ambazo hazijasajiliwa.

“Makampuni hayo wakishanunua risiti za manunuzi bandia, hatimaye huzitumia risiti hizo kudai marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na mhusika, kitendo ambacho kinainyima serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya Sh 10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 16,425,703,824 kwa kipindi hicho.

Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited ambayo tangu mwaka 2010 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,930,170,573 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 10,878,564,089.

Pia imo kampuni ya A.M.Steel & Iron Mills Limited ambayo kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 79,016,112 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 131,693,518 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 210,709,630.

Kampuni nyingine ni A.M Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa VAT ya Sh 638,221,034.80 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 1,063,701,724. 00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 1,701,922,758.00.

Alisema baada ya kubaini ukwepaji kodi huo kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya VAT yasiyostahili kwa kuwa mamlaka imejizatiti kuendelea kuwabaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki.

Aidha alisema uchunguzi wa awali pia umebaini kuwepo makampuni hewa 228 na kusisitiza kwamba wameusimamisha mfumo huo bandia na kutoa siku tatu kwa kampuni zote zinazodaiwa kulipa fedha hizo.

“Hakuna yeyote anayekwepa kodi atasalimika, wote ni lazima walipe na sasa tumedhibiti mfumo huo bandia,” alisema.

Juzi Magufuli akizungumza na Ma RC na Ma DC wapya, aliwataka wakasimamie vyema mapato katika maeneo yao kwani kumekuwepo na baadhi ya watu wajanja wanaotumia vibaya taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) TRA kujinufaisha wenyewe na kuliingizia taifa hasara.

Alisema: “Tulikuwa tunafuatilia mashine za EFDs zinazokusanya mapato, yupo mtu mmoja alitengeneza kampuni nyingi zilizokuwa zikimlipa asilimia tano ya VAT na yeye anacheza na TRA halipi asilimia 18 ya kodi hiyo. Alikuwa anaingiza kati ya shilingi milioni saba mpaka nane kwa dakika. Serikali ilipoteza matrilioni ya fedha. Huyu mtu yupo kwenye mikono salama.

Source. Mpekuzi Blog

Yaonesha una taarifa, eh wameibia serkali what next wanarudisha pesa na kufilisiwa au vipi? . Maana hizi habari za kuachana hewani na kuelezwa habari hewa hatuitaji na hazitatusaidia wakati pesa za kuleta maendeleo nchini petu zilikuwa zikitumiwa na wajanja. Hawa watu yapasa wachukuliwe hatua stahiki ili mtu yoyote hasiwaze hata kufanya haya mambo tena kwenye ardhi ya TZ.

We need to know, wote waliobanika tangu wale wa majipu wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa.
 
Ujinga wangu ni mzigo unaonielemea wanajamvi; hivi kwa wataalamu wa IT na investments zilizofanyika katika uboreshaji wa mifumo ya komputa ni kweli mtu anaweza kuandikiwa cheki na kulipwa baada ya kuwasilisha nyaraka za bandia (fake)!!!!??
Hapa ni lazima huyu mtu ana mtandao hadi ndani.
 
Ujinga wangu ni mzigo unaonielemea wanajamvi; hivi kwa wataalamu wa IT na investments zilizofanyika katika uboreshaji wa mifumo ya komputa ni kweli mtu anaweza kuandikiwa cheki na kulipwa baada ya kuwasilisha nyaraka za bandia (fake)!!!!??
Huo ni ujinga wetu, hata mimi nina maswali mengi kuliko majibu kwamba TRA ikulipe returns za kufoji? Ngoja tuwasubiri wajuwaji watuelimishe!
 
Yaonesha una taarifa, eh wameibiwa serkali what next wanarudisha pesa na kufilisiwa kama hawarudisha au nini kinaendelea. Maana hizi habari za kuachana hewani na kuelezwa habari hewa hatuitaji na hazitatusaidia.

We need to know, wote waliobanika tangu wameanza na wa majipu wote wamechukuliwa hatua gani mpaka sasa.
Mbona hiyo taarifa iko wazi mkuu kwa kila kitu, au unataka nikusomee na niwe nakuletea kila taarifa ya kila hatua wanazopiga katika kuyashughulikia haya madubwana. Man hebu fanyisha kazi bongo yako.

BTW unaweza anza kwenda kuhudhuria mahakama ya mafisadi kujua ni nini kinaendelea. Leo ndio imeanza rasmi.
 
Hakuna kilichofanyika kwa hawa watu mpaka leo sio wote tunaokubali hadithi tu. Tunahitaji vitendo.
 
Kama kuna mtu ambae hakujenga au kumalizia ujenzi wa nyumba yake utawala wa jk asahau kujenga utawala Pombe aisee! Milango yote imesha banwa
Hizi ndizo akili potofu na tumekuwa brainwashed na hizi division five kutoka kwa waliobuni hili 'game'.
Kuna watu wanatokwa jasho masaa 15 lakini hawana uhakika hata wa mlo mmoja wakati mtu anapewa kazi ya kufunga vifaa vya kutambua alama za vidole na kulipwa mabilioni bila hata kufunga vifaa hivyo alafu unategemea wote wajenge!?
Chukua mfano wa mkulima (kumbuka hakuna mkulima hewa) ambaye baada ya kuwakiwa na jua miezi 7 anauza gunia la viazi kwa 15,000/- huku sokoni likiuzwa 180,000/- na hakuna mechanism yoyote ya kutambua unyonyaji huu alafu tunaishia kusema eti wengine 'Mungu kawajalia' na hawa wavuja jasho eti ni 'watanzania masikini na wanyonge'.
Je, si ni hizi kelele zilizopigwa na wapinzani miaka 10 huku wakibezwa!?
 
NINGEFURAHI KAMA HAKUTAKUWEPO NA "DOUBLE STANDARDS" KATIKA KUSHUGHULIKIA HAYA MAMBO....LUGUMI LIMEISHA VIPI ?
MBONA NAPATA KENGEZA ?

Inashangaza wakati walotokomea gizani na vitita vya fweza wamewashiwa taa nakuambiwa wafanyekazi zao mwangani bila tatizo. Hofu yangu ni hii mahakama ilioanzishwa leo.... wenye mitaji ya kuungaunga tutakomaje??
 
Hakuna kilichofanyika kwa hawa watu mpaka leo sio wote tunaokubali hadithi tu. Tunahitaji vitendo.
Kwa hiyo wewe ulitaka leo leo ndio ianze rasmi kusikiliza kesi?? Akili zingine bhana. Tambua leo ndo officially ndio siku ya kwanza kwa mahakama kuwepo, sasa suala la kuanza kusikiliza mashauri linaweza chukua hata miezi miwili.

Hizi akili zenu naamini Magufuli ndo the right person kuziendesha maana mnapenda porojo na shortcut sana. Sasa ngojeni awapeleke mzobemzobe mpaka wananchi wote muisome namba ndipo akili zenu zitakaaa sawa.
 
Hivi Takukuru waliokuwapo katika utawala uliopita na TRA kwanini W asipangwe mstari wakanyongwa hadharani hicho kizazi kikapita? je JPM atafanya @ Jambo peke yake ataweza? police iruhusu tuandamane kuunga mkono Raisi watu hawa wanyongwe ni majambazi no 2.

Hivi hujagundua kitu kwenye serikali ya mwendokasiiii! Wale Mega investors sio rahisi apigwe chini japo wanakutwa na makosa kibao.
 
Kwa kazi nzuri kama hii bado wapo wanaomkosoa tu,yawezekana wanahusika ndo maana midomo iko juu kumkosoa. Tuzidi kuiombea serikali hii mpya.
 
Back
Top Bottom