hivi tunaposikia watazamaji wameingia bure huwa tunaelewaje?..Mkuu, ningekubaliana na wewe ikiwa Yanga walifanya hivyo ili kujinufaisha (financial gan). Huwezi kulinganisha kuingiza watazamaji bure na kampuni mbili kuuziana kitu kwa bei ya chini isiyo halisi katika suala la transfer pricing. Kwa kuuziana kitu kwa bei ya chini lengo inakuwa ni kuongeza faida na kukwepa kodi - financial gain objectives. Sasa kuingiza mashabiki bure, kuna financial gain objectives gani kwa timu kiasi kwamba wawe penalized? Huwezi kusema lazima kuwe na penalty ya kuikosesha serikali mapato - kwa sabau ukisema hivyo, basi mie ile fedha yangu nyingi niliyoiweka benki kwenye current account ambayo haina interest, badala ya ku-invest, ninatakiwa niwe penalized kwa kuikosesha nchi mapato.
Yes, nchi yetu inapitia kipindi cha uongozi wa "kihisia", na hili litatia ndani maamuzi mengine ya TRA.
Je Yanga wana rasilimali uwanja wao ambao wana nguvu ya kufanya hivyo au wanaulupia uwanja mwingine kwa idadi ya ujazo wa uwanja?
Na kama wanalipia watazamaji..hapo tayari kuna biashara imefanyika na kodi lazima ilipwe