Toyota Ipsum au Wish? Tumeweka maoni yetu

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
May 17, 2018
358
670
TOYOTA WISH AU IPSUM?- Kama alivyouliza mdau kwenye group

Na KIMOMWE MOTORS (T) Ltd- Waagizaji Magari

Ipsum za zamani zimeadimika, hivyo ntaongelea ile mpya kuanzia miaka ya 2001.

Toyota Ipsum inakuja na injini kubwa iitwayo 2AZ (Cc2400) yenye Vvti ambayo pia inapatikana kwenye Harrier Old na New, Kluger, Vanguard na Rav 4. Inakadiriwa kwenda mpaka km 11/L, pia ni moja ya gari nzuri za familia japo mafumizi yake ya mafuta ni juu kiliko wish. Uzuri wa ipsum ni nafasi kubwa zaidi ndani, balance nzuri zaidi kwenye mwendo na kutoegemea upande wa nyuma inapokua na mzigo mzito. Pia ni tulivu kwenye safari ndefu kuliko wish sababu ya uzito. Vifaa vinapatikana kwa wingi kwa gharama nafuu. Kuagiza Ipsum inaanzia 14m.

Toyota Wish tuongelee injini maarufu ya 1ZZ (Cc 1800) pia ina Vvti ambapo injini hii pia inapatikana kwenye Voltz, Rav 4 Kill Time, Isis, Spacio, Premio na Allion. Hii inatumia mafuta chini zaidi kiasi cha km 16/L. Ni nzuri pia kwa familia japo inapobeba watu au mizigo mizito nyuma inachuchumaa kuliko Ipsum. Pia balance yake kwenye mwendo mkali sio kubwa kama Ipsum sababu ina bodi jepesi kidogo. Vifaa vinapatikana kwa gharama nafuu. Kuagiza wish inaanzia 12.5m

Hivyo bajeti yako ya kuagiza pamoja na uwezo wa mafuta vitaamua uchukue ipi lakini kwa ujumla zote ni nzuri haswa hii kubwa yaani Ipsum

Zaidi piga 0746 267740 au fika ofisi za Dar au Mbeya

VideoCollagePG_1627898044706.jpg
 
Ahsante sana kiongozi kwa ufafanuzi mzuri.

Naomba niulize hv vvti ni nini kwenye engine na manufaa yake
VVti, ni ufupisho wa teknolojia ya Toyota inayowezesha gari zake kua fanisi zaidi kwenye mafuta na upunguza mungurumo wa gari...injini inakua kubwa ila inatumia mafuta kidogo, mfano 2AZ ya Kluger ina Vvti inatumia chini kidogo wakati Alphard Haina Vvti hivyo kutumia juu...Pia wana teknolojia mpya iitwayo Valvematic (kama sikumbumbi vibaya).

Mitsubishi ana GDi na MIVEC, Volkswagen ana TSi....Makumpuni mengine mengi yana hizi teknolojia sababu ya kuona kwamba soko linataka gari zenye ahueni ha mafuta na sasa kuna ile bora zaidi inaitwa HYBRID ambayo hutumia umeme zaidi malengo yakiwa ni kulinda mazingira na madhara ya moshi wa magari
 
Nimepata somo zuri sana kiongozi
 
TOYOTA WISH AU IPSUM?- Kama alivyouliza mdau kwenye group

Na KIMOMWE MOTORS (T) Ltd- Waagizaji Magari

Ipsum za zamani zimeadimika, hivyo ntaongelea ile mpya kuanzia miaka ya 2001.

Toyota Ipsum inakuja na injini kubwa iitwayo 2AZ (Cc2400) yenye Vvti ambayo pia inapatikana kwenye Harrier Old na New, Kluger, Vanguard na Rav 4. Inakadiriwa kwenda mpaka km 11/L, pia ni moja ya gari nzuri za familia japo mafumizi yake ya mafuta ni juu kiliko wish. Uzuri wa ipsum ni nafasi kubwa zaidi ndani, balance nzuri zaidi kwenye mwendo na kutoegemea upande wa nyuma inapokua na mzigo mzito. Pia ni tulivu kwenye safari ndefu kuliko wish sababu ya uzito. Vifaa vinapatikana kwa wingi kwa gharama nafuu. Kuagiza Ipsum inaanzia 14m.

Toyota Wish tuongelee injini maarufu ya 1ZZ (Cc 1800) pia ina Vvti ambapo injini hii pia inapatikana kwenye Voltz, Rav 4 Kill Time, Isis, Spacio, Premio na Allion. Hii inatumia mafuta chini zaidi kiasi cha km 16/L. Ni nzuri pia kwa familia japo inapobeba watu au mizigo mizito nyuma inachuchumaa kuliko Ipsum. Pia balance yake kwenye mwendo mkali sio kubwa kama Ipsum sababu ina bodi jepesi kidogo. Vifaa vinapatikana kwa gharama nafuu. Kuagiza wish inaanzia 12.5m

Hivyo bajeti yako ya kuagiza pamoja na uwezo wa mafuta vitaamua uchukue ipi lakini kwa ujumla zote ni nzuri haswa hii kubwa yaani Ipsum

Zaidi piga 0746 267740 au fika ofisi za Dar au Mbeya

View attachment 1877274
Toyota WiLL VS mbona hujaiongelea hapa mkuu?
 
Back
Top Bottom