Tofauti kubwa kati ya mwerevu na mjinga, tajiri na maskini

Kwema Wakuu!

Tofauti kubwa ya mwerevu na mjinga ni kuwa Mwerevu anaweza kujifanya, kuigiza kuwa ni Mjinga ila Mjinga hawezi kujifanya wala kuigiza kuwa ni mwerevu

Vile vile Tajiri huweza kujifanya au kuigiza ni Maskini lakini Kamwe Maskini hana uwezo wa kujifanya wala kuigiza yeye ni Tajiri.

Naweka Maiki chini
Kupitia mitandao ya kijamii watu wengi wanaweza kuigiza kuwa matajiri. Rudia kufanya utafiti wako bwashee.
 
Mada imekaa kimtazamo sana, naona njia nyingi za kubisha.

Mfano tajiri anaweza kujifanya maskini kwa kitomiliki vitu vya bei ghali, ili aonekane mnyenyekevu.
Maskini anaweza kujifanya tajiri kwa kuvaa visuti na kushika vi iphone ili ajitutumue kwa watu...
 
Hakuna mwerevu wa kila kitu
Hakuna mjinga wa kila kitu
Kila mtu ana umuhimu wake?

Utakuwa doctor lakini utaenda msikitini au kanisani kuhubiriwa na darasa la 7

Upo Sahihi kabisa
Lakini hoja inabaki palepale Mjinga hawezi kuigiza NI Mwerevu

Kûna àmbao walijaribu wakaumbuka
Mfano wanasiasa mara kadhaa wamekuwa wakijaribu kuwa werevu hata kwèñye mambo ya dini ndîo unasikia madesa yakivurugwa. Rejea ishu ya Spika ndugai na hadithi yake kumhusu Yesu
 
Mada imekaa kimtazamo sana, naona njia nyingi za kubisha.

Mfano tajiri anaweza kujifanya maskini kwa kitomiliki vitu vya bei ghali, ili aonekane mnyenyekevu.
Maskini anaweza kujifanya tajiri kwa kuvaa visuti na kushika vi iphone ili ajitutumue kwa watu...

Maskini hawezi kufanya hayo unayosema,
Unazungumzia kundi jingine.
 
Ata mwerevu alikua mjinga ila akaelimika halikadhalika tajiri naye alikua masikini kabla ya kuwa tajiri. Uwerevu ni stage ya juu ya kuukimbia ujinga na utajiri pia ni stage ya juu ya kuuukimbia umasikini

Lakini kuigiza Maskini hawezi kuigiza utajiri Kwa sababu hajawahi kuwa tajiri ila Maskini anaweza Kwa sababu umaskini NI Jambo rahisi àmbalo Mwanadamu yeyote anaweza kulipata íwe Kwa kusudi au Bahati mbaya (Mikosi)
Halikadhalika na Mjinga Vs mwerevu
 
Back
Top Bottom