rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,608
- 22,923
Ccm walianza kutinua watu muda. Mrefu kina Baron go , maalim seifu na wenAke walitimuliwa ccm wakati huo hats vyama vingi havijaanza
Wanabodi,
Mimi ni miongoni mwa watu ninaotatizwa sana na ukiukwaji wa haki unaofanyika popote ndani ya JMT na ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kabisa kumuita rais wetu Dr.John Pombe Magufuli kuwa ni dikiteta.
Katika tumbua tumbua majipu ya rais Magufuli niliunga mkono dhana nzima ya utumbuaji na dhima ya utumbuaji ila sikuunga mkono utekelezaji wa utumbuaji huo kutokana na baadhi ya utumbuaji kufanywa kidikiteta kwa chuki, papara na double standards za hali ya juu kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni.
Lakini kwa hii timua timua ya kuwatimua vigogo wa CCM, nimefarijika sana kwa sababu kumbe huu utumbuaji wa kidikiteta sio kwa serikali tuu bali hata kwa CCM. Hii ni plus kwa Magufuli kuwa katika tumbua tumbua, anatumbua tuu bila kumuangalia mtu usoni kuwa nani ni nani, kama mtu kama Sofia Simba ameweza kutumbuliwa, then kiukweli Magufuli sio mchezo! .
Hakuna ubishi kuwa CCM ni chama kikongwe kinafanya mambo yake kiutu uzima. Kwenye katiba yake kinazo taratibu za nidhamu zilizofuatwa ndani kwa ndani, kimya kimya hadi kufikia hatua ya mwisho ya watu kupigwa chini ndipo umma unaambiwa na kupigwa na surprise. Huu ni ukomavu na ndiko kufanya maamuzi makubwa kiutu uzima. Pongezi ziende kwa Mwenyekiti Magufuli. Wapinzani mjifunze kutoka CCM.
Ugomvi wa Baba na Mama.
Mara nyingi watoto huwa hawawezi kufahamua kuwa kumbe baba na mama huwa wanagombana mara mara ugomvi wa kimya kimya chumbani. Mara kwa mara wanawake huwa wanachukia na kuwanyima 'chakula' waume zao, hivyo kuna wanaume kibao hulala njaa na hawasemi. Kuna wanawake kibao hubakwa na waume zao na wengine hupokea hadi vipigo lakini hawasemi. Kuna mara kibao baba na mama wamenuniana ila akija mgeni warajikausha.
Ugomvi ukiwa mkubwa hadi mama kufungasha ndipo hakuna namna lazima watoto watajua. Hiki ndicho kilichofanyika CCM.
Watuhumiwa wote walijadiliwa toka vikao vya chini kimya kimya. Wakapewa barua za mashitaka yao, wakapewa muda wa kujibu tuhuma, wakaitwa kujieleza, wakahojiwa na kupewa muda wa haki ya kusikilizwa na kujitetea, kisha vikao vikafikia maamuzi kimya kimya na hatimaye ndipo vikao vya maamuzi vikatangaza maamuzi yale. Huu ni ukomavu wa hali ya juu na CCM kinastahili pongezi za dhati kwa hili.
Siku Polepole akiongea na media, awahakikishie Watanzania kuwa taratibu zilifuatwa vinginevyo kama ule udikiteta wa kukanyaga katiba ya nchi pia umeikanyaga katiba ya CCM hivyo timua timua ile ni muendelezo wa udikiteta ule ule, CCM kitakuwa ni chama cha kidikiteta na kama kinaongozwa kidikiteta na kiongozi dikiteta, then jiulize taifa letu la Tanzania tunalipeleka wapi? .
Chedema utumieni uzoefu na ukongwe wa CCM katika kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia katiba zenu, niliwahi kuwashauri hivi kuhusu udikiteta katika kuendesha mambo yenu ya ndani.
Fanyeni mambo yenu kimya kimya, jifunzeni kwa CCM ili angalau 2020 Watanzania tuweze kuwafikiria tuwajaribishe vinginevyo tutaendelea kiongozwa na chama kikongwe kilichozeeka mpaka basi lakini kila kinapofanya face lift kama hii, kinarudia ujana hivyo hata hapo mlipo kama mnajidhania mmesimama, angalieni msianguke come 2020.
Hongera sana CCM kwa mabadiliko. Hongera kwa ukomavu.
Jumatatu njema
Paskali.
Hapo ndipo ndugu Paskal anapojiondoa ufahamu na kujifanya hayakumbuki hayo na sasa eti, anaona chama cha magamba chenyewe ndo waasisi wa kutimua wasaliti,, hv kumuunga mkono mwanachama mwenzako na kuonyesha hisia za kumkubali na kuukataa utaratibu fulani wa kibabe leo kwao ni usaliti,,!! Kwani wakati wanaimba tunaimani na mtu fulani kama mwenyekiti wao alivyofafanua na kuonyesha ya kuwa hilo ndo sababu kuu ya kosa lao huyo waliekuwa wanaimani nae alikuwa ni mwanachama wa upinzani kipindi hicho,!!??Mkuu Paskal usijifanye hukumbuki historia ya siasa za Tanzania, CCM wanaiga yaliyokwishafanywa na vyama vya upinzani, CCM walikuwa hawana hulka ya kufukuza walikuwa wanakubembeleza kujiuzulu ref kujivua gamba.
Unakumbuka Chadema iliwatimua madiwani watano (5) wa Arusha kwa mpigo mkaanza kusema si demokrasia, Chadema iliwatimua viongozi waandamizi kina Zitto, Mwigamba na prf Kitila Mkumbo, Arfi aliyekuwa makamu Mkiti akaamua kujitoa umesahau.
CUF nao walishawahi kutimua viongozi waandamizi Mapalala aliyekuwa Mkiti na juzi wamemtimua Mkiti mwingine prf Lipumba. Hali kadhalika NCCR ilishawahi kumtimua Mkiti wake Mrema na viongozi waandamizi.
Ni kweli CCM ni chama kongwe lakini kwa hili walichelewa sana hadi wamejifunza kwa vyama pinzani kuwa kulea wasaliti ni kuua chama.
Huenda waliofukuzwa waliimba wana imani na fulani kwa sauti kubwa na wakipiga makofi juu juu, waliopewa onyo waliimba kwa sauti ndogo wakitazama chini na kwa kujificha, na waliosamehewa wao waliimba kimoyomoyo walionekana wakitingisha vichwa tu. Ni mtazamo wangu tu maana kosa ni moja lakini adhabu tofauti.Wengine mbona mmewaacha?
Asante kwa kumkumbusha mburura huyu aliyetoa postMkuu Paskal usijifanye hukumbuki historia ya siasa za Tanzania, CCM wanaiga yaliyokwishafanywa na vyama vya upinzani, CCM walikuwa hawana hulka ya kufukuza walikuwa wanakubembeleza kujiuzulu ref kujivua gamba.
Unakumbuka Chadema iliwatimua madiwani watano (5) wa Arusha kwa mpigo mkaanza kusema si demokrasia, Chadema iliwatimua viongozi waandamizi kina Zitto, Mwigamba na prf Kitila Mkumbo, Arfi aliyekuwa makamu Mkiti akaamua kujitoa umesahau.
CUF nao walishawahi kutimua viongozi waandamizi Mapalala aliyekuwa Mkiti na juzi wamemtimua Mkiti mwingine prf Lipumba. Hali kadhalika NCCR ilishawahi kumtimua Mkiti wake Mrema na viongozi waandamizi.
Ni kweli CCM ni chama kongwe lakini kwa hili walichelewa sana hadi wamejifunza kwa vyama pinzani kuwa kulea wasaliti ni kuua chama.
Katika hili Paskali amepotea. Àidha sasa umefika wakati Paskali ajiweke wazi kwamba yeye ni Ccm.. Kwanza ccm hawakuwahi kuwa na utaratibu wa kuwajibishana hadi chadema walipokuwa wanachukua hatua kwa wanachama na viongozi wao, ndipo ccm nao wakaiga. Refer isue ya madiwani Bukoba, ambapo walipata kigugumizi wakati vikao vya ngazi ya chini hadi mkoa viliishawafukuza. Leo Paskali anaposema wapinzani wàjifunze toka ccm, ni lipi hilo la kujifunza?..........Watuhumiwa wote walijadiliwa toka vikao vya chini kimya kimya. Wakapewa barua za mashitaka yao, wakapewa muda wa kujibu tuhuma, wakaitwa kujieleza, wakahojiwa na kupewa muda wa haki ya kusikilizwa na kujitetea, kisha vikao vikafikia maamuzi kimya kimya na hatimaye ndipo vikao vya maamuzi vikatangaza maamuzi yale....
Na kisha umma ukatangaziwa wajumbe wote wameunga hoja kwa kishindo,ilihali mambo yalikuwa kimya kimya na hakuna upigaji kura.
Zitto alipotaka kufukuzwa aliitwa na kusomewa mashitaka,japo hakwenda,akapewa barua na muda wa kujibu,akajua makosa yake,akakimbilia mahakamani,ambapo ni kinyume cha katiba!!
Alifukuzwa kwa uwazi kabisa na kwa utaratibu.
Huko ugambani watu wanawekwa selo kwanza ili vikao viendelee,then tunapiga makofi kwa demokrasia na ukomavu!!
Wengi hawajakuelewa mkuu Paskali.Wanabodi,
Mimi ni miongoni mwa watu ninaotatizwa sana na ukiukwaji wa haki unaofanyika popote ndani ya JMT na ni miongoni mwa watu wa mwanzo mwanzo kabisa kumuita rais wetu Dr.John Pombe Magufuli kuwa ni dikiteta.
Katika tumbua tumbua majipu ya rais Magufuli niliunga mkono dhana nzima ya utumbuaji na dhima ya utumbuaji ila sikuunga mkono utekelezaji wa utumbuaji huo kutokana na baadhi ya utumbuaji kufanywa kidikiteta kwa chuki, papara na double standards za hali ya juu kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni.
Lakini kwa hii timua timua ya kuwatimua vigogo wa CCM, nimefarijika sana kwa sababu kumbe huu utumbuaji wa kidikiteta sio kwa serikali tuu bali hata kwa CCM. Hii ni plus kwa Magufuli kuwa katika tumbua tumbua, anatumbua tuu bila kumuangalia mtu usoni kuwa nani ni nani, kama mtu kama Sofia Simba ameweza kutumbuliwa, then kiukweli Magufuli sio mchezo! .
Hakuna ubishi kuwa CCM ni chama kikongwe kinafanya mambo yake kiutu uzima. Kwenye katiba yake kinazo taratibu za nidhamu zilizofuatwa ndani kwa ndani, kimya kimya hadi kufikia hatua ya mwisho ya watu kupigwa chini ndipo umma unaambiwa na kupigwa na surprise. Huu ni ukomavu na ndiko kufanya maamuzi makubwa kiutu uzima. Pongezi ziende kwa Mwenyekiti Magufuli. Wapinzani mjifunze kutoka CCM.
Ugomvi wa Baba na Mama.
Mara nyingi watoto huwa hawawezi kufahamua kuwa kumbe baba na mama huwa wanagombana mara mara ugomvi wa kimya kimya chumbani. Mara kwa mara wanawake huwa wanachukia na kuwanyima 'chakula' waume zao, hivyo kuna wanaume kibao hulala njaa na hawasemi. Kuna wanawake kibao hubakwa na waume zao na wengine hupokea hadi vipigo lakini hawasemi. Kuna mara kibao baba na mama wamenuniana ila akija mgeni warajikausha.
Ugomvi ukiwa mkubwa hadi mama kufungasha ndipo hakuna namna lazima watoto watajua tena hawatajua sababu ya ugomvi ni nini au nani ni mkosaji na amekosa nini.Hiki ndicho kilichofanyika CCM, watu wametimuliwa bila wanachama kuelezwa wamefanya makosa zaidi zaidi ya neno usaliti lakini hakuna taarifa yoyote huku nje nani amefanya nini, hali iliyopelekea watu kuhisi sababu ni ule wimbo wa "Tunaimani na Lowassa...
Oye Oye Oye...
Lowassa kweli...kweli
Kweli...kweli
Kweli kweli Lowassa
Lowassa kweli...kweli
Kweli...kweli
Kweli kweli Lowassa".
Kama kweli hili kosa lao kumsupport Lowassa, then kiukweli kabisa CCM watakuwa ni vichaa fulani kwa sababu kwa mujibu wa katiba ya CCM, kumsupport mtu yoyote wakati wa uchaguzi sio kosa, hivyo hilo sio kosa lao, bali wanamakosa yao ambayo ni mambo yao ya ndani kama ugomvi wa baba na mama chumbani, tumeonyeshwa tuu wakitupiwa virago vyao nje.
Kuhusu mmoja wa watuhumiwa Mama Sofia Simba, mimi niliwahi kumzungumza hapa na kumuita ni ubatili!, Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili!
Ni imani yangu kuwa watuhumiwa wote walijadiliwa toka vikao vya chini kimya kimya. Wakapewa barua za mashitaka yao, wakapewa muda wa kujibu tuhuma, wakaitwa kujieleza, wakahojiwa na kupewa muda wa haki ya kusikilizwa na kujitetea, kisha vikao vikafikia maamuzi kimya kimya na hatimaye ndipo vikao vya maamuzi vikatangaza maamuzi yale. Huu ni ukomavu wa hali ya juu na CCM kinastahili pongezi za dhati kwa hili.
Siku Polepole akiongea na media, awahakikishie Watanzania kuwa taratibu zilifuatwa vinginevyo kama ule udikiteta wa kukanyaga katiba ya nchi pia umeikanyaga katiba ya CCM hivyo timua timua ile ni muendelezo wa udikiteta ule ule, CCM kitakuwa ni chama cha kidikiteta na kama kinaongozwa kidikiteta na kiongozi dikiteta, then jiulize taifa letu la Tanzania tunalipeleka wapi? .
Chedema utumieni uzoefu na ukongwe wa CCM katika kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia katiba zenu, niliwahi kuwashauri hivi kuhusu udikiteta katika kuendesha mambo yenu ya ndani.Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
Wafuasi wa Zitto na Manazi wa CHADEMA: Tunajenga Nyumba Moja, Tunagombea Fito za Nini?
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
Chadema, CUF na NCCR Mageuzi, kukitokea tena utovu wa nidhamu, fanyeni mambo yenu kimya kimya, tumieni kanuni zenu na mamlaka halali za nidhamu, mfano Zitto alipotimuliwa, kikao kilichomtimua ni Kamati Kuu wakati mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu. Msione ugumu kujifunzeni kwa wakongwe kama CCM ili angalau 2020 Watanzania tuweze kuwafikiria tuwajaribishe vinginevyo tutaendelea kiongozwa na chama kikongwe kilichozeeka mpaka basi lakini kila kinapofanya face lift kama hii, kinarudia ujana hivyo hata hapo mlipo kama mnajidhania mmesimama, angalieni 2020 msianguke jumla kwa sababu by that time CCM itakuwa kama kigoli mweupe kwenye Chagulaga, ikimeremeta, kufuatia kazi nzuri ya Magufuli ndio maana tumeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Mabadiliko yoyote yanayoanzia juu kwenda chini bila kujadiliwa na watu wa chini katika ushirikishaji, no matter ni mazuri kiasi gani, pia ni udikiteta, ila kitendo cha CCM kuitisha Mkutano Mkuu kuya ruber stamp ni kufuata katiba yake, hivyo hongera sana CCM kwa mabadiliko, na Hongera kwa ukomavu, vyama vingine igeni mfano.
Jumatatu njema
Paskali.