TIGO: Wanaomiliki simu feki kupewa nyingine bure

Habari wanabodi.

Kampuni ya Tigo Tanzania inakualika wewe mtanzania unayemiliki simu feki kufika katika duka lolote la Tigo hapo utabadilisha simu yako feki na kupatiwa halisi/original bureee aina ya Itel 21100 pamoja na ofa za dakika na meseji pamoja na data bila kulipa chochote.

Wahi sasa.

Chanzo: Clouds Fm
Pengine hukulisikia tangazo vizuri ni lazima ununue kifurushi cha 22,000....
 
Ngoja nihamishe line ya airtel hapa kwenye simu feki niweke line ya tigo nikapate tambarare ya simu
 
Du hivi ni kweli IQ zetu ni ndogo hivi.

Hivi ukiambiwa nunua bia moja [2,500] na kupewa mbili bure ni sawa na kuzinunua?

Unachonunua ni muda wako wa maongezi tu kisha simu bure. Ukitaka kuona utofauti wake nenda duka la simu nunua simu mpya 22,0000(kama ipo) kisha uone kama itakua na muda wa maaongezi na airtime yenye thamani sawa na simu yako
 
Mkuu bei ya hizo itel 2100 ni elfu 25 kwenye maduka ya kawaida hivyo ni danganya toto tu.
Kwa jinsi watu tunavyopenda vya bure maduka yatafurika bila kujali hicho kifurushi tunachonunua 22,000
 
Back
Top Bottom