The Radar Scandal: Investigation & Progress

Nafikiri Huu sio uchunguzi, Kigoda na Chenge wameambiwa wa review mkataba usiokuwa na masilahi kwa chama na kutoa mapendekezo ya namna ya kuuboresha. Lakini Chenge na M borongaji Lowassa ni walewale, sijui kama kutakuwa na maboresho hapa.
 
hakuna jipya hapo!nape kadanganya na jk naye anajazia uongo huohuo! kuna kupona hapo kweli???????mimi sielewi hawa ccm wanafanya nini?labda wenzangu mnisaidie,kama wanashindwa kuwa wazi its better wafunge midomo yao wasitushirikishe kwenye "matokonyo" yao,wanakaa kikao na suruali zao vry serous kujadili ******!nina hasira mimi hawajui tu,kila siku wanaanzisha ujinga ambao hawawezi kuutetea na wala kuumaliza,tume tume tume tume tume tume tume mpaka lini mbona ya wao kuongeza vimada na malaya haundi tume?huu ni ******
 
Naona mtoa hoja hajui kamati inayoundwa itafanya nini. Kamati hii siyo ya kuchunguza kama kuna ufisadi katika katika mkataba wa UVCCM. Kamati ya kina Chenge inachunguza kama mkataba huu una maslahi kwa UVCCM. Haya ni mabo mawili tofauti. Kama kuna ufisadi ni Polisi au Takukuru watahusika. Mwenye masiko na asikie!
 
hakuna jipya hapo!nape kadanganya na jk naye anajazia uongo huohuo! kuna kupona hapo kweli???????mimi sielewi hawa ccm wanafanya nini?labda wenzangu mnisaidie,kama wanashindwa kuwa wazi its better wafunge midomo yao wasitushirikishe kwenye "matokonyo" yao,wanakaa kikao na suruali zao vry serous kujadili ******!nina hasira mimi hawajui tu,kila siku wanaanzisha ujinga ambao hawawezi kuutetea na wala kuumaliza,tume tume tume tume tume tume tume mpaka lini mbona ya wao kuongeza vimada na malaya haundi tume?huu ni ******
 
Jamani walishasema kuwa ufisadi wa chenge ni serikalini tu, si katika chama. Kumbukeni kuwa hadi hivi sasa Chenge ndiye mwenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM
 
Chenge, Kigoda kupitia mkataba jengo la UVCCM

2008-09-11 10:55:55
Na Mary Edward, Dodoma na Simon Mhina Dar

Kilio cha Nape Nnauye juu ya mkataba wa jengo jipya la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kimesikika ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho na sasa mkataba huo umeundiwa Timu ya watu watatu kurekebisha kasoro zilizopo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Salehe Feruz, aliiambia Nipashe jana usiku kwamba Timu hiyo itaundwa na wajumbe wa Kamati Kuu, Andrew Chenge, Pindi Chana na Dk. Abdallah Kigoda.

Alisema kazi ya Timu hiyo ni kushirikiana na UVCCM kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika mkataba huo na kuendelea kushauri hatua kwa hatua za utekelezaji wa mradi huo.

Hata hivyo, Feruz alisema Kamati Kuu haitapitia tena mkataba huo, bali itakuwa ikipewa taarifa ya maendeleo yake.

``Kazi ya kusaini mkataba huo ipo ndani ya uwezo wa UVCCM,`` alifafanua.

Alisema suala la kusainiwa kwa mkataba huo liko ndani ya uwezo wa UVCCM na kwamba kilichokuwa kimesainiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini, Edward Lowassa, si mkataba wa ujenzi bali ni makubaliano ya awali (MoU).

Alitaja baadhi ya kasoro zilizogundulika kuwa ni kutokueleza madaraka ya bodi ya wakurugenzi kwa pande zote mbili; kutokuweka wazi mchakato mzima wa uendelezaji wa jengo hatua kwa hatua; na kutokuweka wazi hatua za kusuluhisha migogoro endapo itajitokeza.

Feruz pia alisema mkataba huo hausemi sababu za kuvunjwa kwa mkataba kama ikibidi.

Mkataba huo umekuwa chimbuko la mvutano ndani ya UVCCM kiasi cha kusababisha mwanasiasa kijana na machachari, Nape, kufukuzwa uanachama wa umoja huo Jumapili iliyopita.

Nape alifukuzwa unachama na Baraza Kuu la UVCCM baada ya kutuhumiwa kuvunja kanuni za umoja huo.
Feruz alisema kwamba Timu hiyo itakuwa endelevu kwa ajili ya kushirikiana na UVCCM kushauri maendeleo ya mradi huo.

Pia alisema kwamba Kamati Kuu imegundua kuwa mradi huo una manufaa kwa UVCCM kwa kuwa utaifanya jumuiya hiyo kujitegemea.

Alisema Kamati Kuu imeona ni vema jumuiya hiyo kuingia ubia kwa vile haina uwezo wa kuliendeleza eneo hilo wala kuliendesha. ``Kama hawataingia ubia basi eneo lile lingeendelea kuwa wazi tu bila faida,`` alisema.

Kwa mujibu wa mkataba huo, UVCCM itamiliki asilimia 25 na wabia asilimia 75.

Hapo awali, Nape alionyesha wasiwasi wake kuhusiana na mkataba huo kutokuwa na ukomo na kiasi kidogo cha faida ambayo inatarajiwa kupatikana.

Hata hivyo, Feruz alisema Kamati Kuu imeridhia mkataba huo kuwa endelevu kwa ubia kwa pande zote mbili.

Kuhusu suala la Nape kufukuzwa uanachama wa UVCCM, alisema Kamati Kuu imesema kwamba haiwezi kuingilia maamuzi ya Baraza Kuu la UVCCM, lakini Nape ana uhuru wa kukata rufaa kwa umoja huo au hata CCM kama hakuridhika na maamuzi.

* SOURCE: Nipashe
 
Hawa CCM nao ni mabwege sana. Huyu Chenge ni mmoja wa watu ambaye amewapaka matope kwa questionable integrity na kwa umbumbumbu wake wa Sheria ameiingiza nchi kwenye matatizo makubwa sana na Kuifanya CCM ionekane ni ya MAfisadi leo wanampa kazi ya kupitia Mktaba wa UVCCM na mwekezaji; kwa utaalamu gani wa sheria alionao wakati kazi yake Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali WAKATI WA AWAMU YA 3 aliprove hana utaalamu wowote?

Nachoka kabisa
 
Kuchunguza kama kuna maslahi ndani ya huo mradi ni (subset) lakini (Super set) yake ni ufisadi hivyo basi vitu hivi vinaenda pamoja kuna janja ya nyani imetumika hapa huoni badala ya kuiita Tume wameiita Kamati? hivyo Chenge ambae ni mwenyekiti wa Maadili ndani ya CCM na ambae anatuhumiwa kwa ufisadi Serikalini hakupaswa kushughulikia hili!!! kwa sababu bila hata kufikiri sana mheshimiwa huyu ni Fisadi aliyekubuhu.
 
Umumuuuuuuuuuuuuuuuuuu! hapa nachoka. Labda wanamsafisha aje agombee uraisi ili awakomeshe wote waliomzodoa. te! te! te! teeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
Jamani naomba kuuliza hivi mwizi anaweza kumuhukumu mwizi mwenzie?

Hii inanikumbusha Mafarisayo waliompelekea Yesu mwanamke aliyefumaniwa kwenye uzinzi: Yesu akawaambia asiye na dhambi na awe wakwanza kumrushia jiwe yule mwanamke aliyefumaniwa.
 
Waungwana genge la wana-CCM ni hatari kweli kweli inahitaji kiongozi aliye tayari hata kufa kwa ajili ya nchi yake ili mabadiliko ya kweli yatokee, lakini sidhani kama Kikwete yuko tayari kwa hilo....otherwise tutaendelea kushuhudia vituko tu.

Lingine ni kama mchangiaji borntown alivyosema hapo juu, ni kuwa wanajuana wote madhambi yao kwa hiyo ni vigumu kuchukua hatua zidi ya wengine kama wewe mwenyewe sio msafi......kwa ufupi ni blackmailing of one another ndio nguvu ya wana-CCM kwa sasa....kwa hiyo sio ajabu tusipoona hatua zikichukuliwa.
 
Hawa CCM nao ni mabwege sana. Huyu Chenge ni mmoja wa watu ambaye amewapaka matope kwa questionable integrity na kwa umbumbumbu wake wa Sheria ameiingiza nchi kwenye matatizo makubwa sana na Kuifanya CCM ionekane ni ya MAfisadi leo wanampa kazi ya kupitia Mktaba wa UVCCM na mwekezaji; kwa utaalamu gani wa sheria alionao wakati kazi yake Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali WAKATI WA AWAMU YA 3 aliprove hana utaalamu wowote?

Nachoka kabisa
...Ibra, Hao ndio Chi CHi eM wanajaribu kutusahaulisha kuwa Chenge ni fisadi aliyekubuhu na ndio maana wamemuweka kwenye hiyo tume ni njia ya kumrudisha kundini..Ufisadi hauwezi kwisha kwa njia hii jamaa anaendelea kujitafunia tujisenti twake kiulainiiiiiiiiii
 
Daaaaaa. Pia jamani Chenge alimfadhili kikwete kwenye kampani za kuwania urahisi kwa hivyo ni ngumu kumtosa.
 
Jamani kama chege huyu huyu ndiye aliyeshiriki kwenye mikataba mibovu tangu enzi za BM, sasa ianluwaje tena ndugu zangu wanasisiem wenzangu ateuliwe kuwa kwenye kamati ya kuchunguza udhalihu wa EL, kama ndio hivyo kwanini mkuu wao RA hakuteuliwa, hawaoni kwa kufanya huvyo ni kumbagua? Nape usife vijana wote upinzani na ccm tupo pamoja nawe.

Makamba `mzee wa kupopoka` kuwa mwangalifu sana na mdomo wako jasije kukuta kama yale ya jamaa wa mchinga.
 
CCM kwisha habari yao..wanalindana hata vitu vya kijinga..ule mkataba hautakiwi hata kuundiwa tume...wala nini...ni sawa na EPA report ipo unaunda tume ya nini???JK chama kimekushinda ....Serikali imekushinda...ungejuzulu ningekuheshimu sana......ingekuwa rahisi kuomba Rais mwingine toka nje TZ aje atusaidie..ningependekeza Kagame...JK angeona wanaume wa shoka wanavypogiga mzigoo...sio siasa hata kwenye utendaji...aibu sana....
 
Back
Top Bottom