The power within, niliingia ndani ya msingi wa nyumba Kwa kudhamiria tu

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,199
31,832
Salaam, shalom!!

INTRODUCTION.

Tuendelee na mada za wakubwa,

Naamini Hadi sasa Kila mtu ajua kuwa,

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Nimekuwa nikifanya majaribio mengi ya kutumia uwezo wangu ndani yangu na nimekuwa nilipata matokeo mazuri.

Kudhamiria, au kuweka Nia au kutamani kujua jambo Fulani linalokutatiza Kwa kuiambia Roho Yako ifanye uchunguzi ni jambo linalowezekana kabisa.

MADA: JINSI YA KUTUMIA DHAMIRA/ SHAUKU/ WILL KUPATA UFUMBUZI WA SWALI AU JAMBO LINALOKUTATIZA.

Soma simulizi hii fupi.

Siku Moja nilisafiri nikaenda mji Fulani, nilipofika mji Ule, katika tembea tembea zangu,

Nilikutana na nyumba Moja, kilichonifanya nisimame kuiangalia nyumba Ile ni mchwa, mchwa walionekana kutoboa Tundu mwanzo wa msingi wa nyumba Ile kwenye maungio ya msingi na ukuta. Niliangalia nyumba Ile nzuri na kushangaa iweje mchwa wajitokeze haraka kiasi hicho na kuanza uharibifu mapema hivyo, mchwa walionekana kuleta juu udongo japo haukuwa mwingi.

Baada ya kusimama Kwa sekunde kadhaa, nilitamani kujua athari ambazo mchwa wale wamesababisha ndani ya msingi wa nyumba Ile nzuri, nilitamani kujua uharibifu walioufanya ni Kwa kiasi Gani, sasa Kwa kuwa nisingeweza kuingia ndani ya msingi Ule kuona Kwa macho bila kuchimbua au kubomoa Kwa sururu, nilidhamiria kifuatacho,

Niliiambia Roho yangu, nikisema na mtu halisi wa ndani ambaye ndiye niliyevaa mwili huu wa nyama niliiambia yafuatayo,

" Napenda niingie ndani ya msingi huu wa nyumba Kisha nijue ni Kwa kiasi Gani mchwa Hawa wamefanya uharibifu".

Baada ya kusema/ kuweka dhamira/ wish / will hiyo, niliendelea na safari yangu.

Nilipolala usiku, baada ya muda kupita, nilijukuta nimesimama pale pale nilipokuwa nimesimama mchana.

Kilichonishangaza ni uwezo niliokuwa nao wakati huu wa mara ya pili, macho yangu yaliona bila kikomo, niliweza kuona Kila sehemu za ndani ya msingi Ule, niliweza pia kuingia Hadi ndani na kutembea ndani ya msingi na kuona mashimo ya mchwa na mchwa na uharibifu Walio fanya mchwa wale , jambo ambalo mchana sikuweza kufanya.

Nilipoamka asubuhi, nilijishangaa,nilipata kujua kumbe ninao uwezo mkubwa sana ndani yangu nisioutumia Bado.

FUNZO.

1. Tumia dhamira, make a wish, Sema na wewe mwenyewe mtu wa ndani, mpe mtu huyo wa ndani task ya kufanya Kwa mambo ambayo katika mwili yanakutatiza au huna majibu nayo.

Ni hayo tu Kwa Leo.

Karibuni 🙏
 
Ewe MTU wa ndani Yangu, nakutuma unifunulie hao watekaji ni akina Nani na kwa nini Wapinzani Tu ndio wawe wahanga?
Nilipoangalia picha Moja ya Hawa viongozi, nikiona yafuatayo,

Mimi na wenzangu kadhaa, tulikuwa tumejificha ndani ya nyumba ambayo Kwa nje ilionekana kama maliwato, ndani ya maliwato Ile, palikuwa na vyumba vya Siri tulimokuwa tumejificha. Na maliwato Ile ilikuwa ya JINSIA me.

Dhumuni la kujificha, ilikuwa ni kuepuka Hali ya hatari ambayo ilikuwa ikileta HOFU mtaani,

Sasa mtu yule tulimdhania ndiye kiongozi mwenye kutumia watu wale waletao sintofahamu Kwa wasio na hatia. Jambo Moja lilinishangaza nilkabadili msimamo wangu juu ya kiongozi yule.

Aliingia ndani ya maliwato Ile ambamo tulikuwa tumejificha, na aliingia pekeake na hakujua Kuna watu wamejificha mle, na mwonekano wake ulikuwa kama wa mtu aliyechanganyikiwa hivi,

Alikuwa na nywele zimevurugika, anaongea pekeake na kurusha mikono kama vile analaumu.jambo Fulani,

Sisi tukiwa gizani tumejificha, tulimwona vizuri ila Yeye hakutuona, maana maliwato Ile, ilikuwa na pango la Siri na Mahali salama kujificha.

Sasa wenzangu wakaniambia, nenda kamshambulie maana kajileta mwenyewe, Mimi niliwazuia niliwambia Si sawa kufanya hivyo, niliwambia wamtizame alivyo mwonekano wake kama mtu aliyetok ktk state nzuri ya akili ya kawaida. Tuliendelea kukaa bila kufanya chochote.

Sasa baada ya kuingia mle ndani, haukupita muda, wakaingia walinzi ambao walikagua vyumba vya ndani na kufanikiwa kututia nguvuni wakidai tulidhamiria kumduru kiongozi yule,

Tulijitetea kuwa sie hatukuwa na dhamira ovu juu yake maana aliingia muda mrefu tena pekeake na hatukumdhuru.

Sasa wale walinzi waliomba ushauri Kwa kiongozi yule juu ya hatua Gani zichukuliwe dhidi yetu,

Cha kushangaza, kiongozi yule hakujua nini Cha kufanya, hakusema chochote Wala kuamua chochote,

Sasa walinzi wale baada ya kuona vile, walituachia tukaenda zetu Kwa Amani.

FUNZO.

Tulipo hivi sasa, ndege Haina rubani, inajiendea yenyewe, waiongozao ndege ni wengine kabisa na mbaya zaidi Kila Mmoja anabonyeza rimoti kivyake atakavyo.

Tuendelee na maombi Ili ndege itue salama.
 
Wengi tulizaliwa tukiwa roho,nafsi na mwili ila hilo sio kusudi la Muumba.

Maana ukiwa roho ilikuwa ni kuugua tu kwa mujibu wa warumi 8:23

Na ukiwa nafsi ni kubeba uchafu tu,uzinzi,ulevi,uongo,uasherati,wizi,dhuluma na kadhalika.

Na ukiwa mwili ilikuwa ni uadui na Muumba wako kwa mujibu wa
Warumi 8:7
Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

Hayo yote yalitokea baada ya uumbaji kuwa chini ya ubatili
Warumi 8:20
Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;

Je kusudi ni nini?
Muumba alitukusudia tuwe MOYO yaani mema na mazuri tu,Muonekano wako wote huo ni Moyo, ndo maana akasema katika

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Hapo ndipo kuna umilele tuliokusudiwa

Mhuburi 3:11
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
 
Moyo KAZI yake ni kusukuma Damu,

Moyo huo wenye utambuzi uliotajwa hapo Muhubiri 3:11 ni NAFSI.

Ni hapo palipo center iunganishayo Roho na mwili.

Katika NAFSI ndipo penye akili, hisia na uwezo wa kufanya maamuzi.
 
Sio moyo huo unaoenda kupasuliwa india.

Mhubiri 10:2
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
 
Sio moyo huo unaoenda kupasuliwa india.

Mhubiri 10:2
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
Ndio huo moyo usioonekana,

Ndiyo NAFSI hiyo hiyo Kwa lugha ingine.
 
Hii mada nzuri sana, ila natamani uelezee hatua kwa hatua unavyoanza kusema na mtu wa ndani mpaka ukilala unaota ndoto. Yaani hatua ya kwanza ni nini, unakuwa umekaa, umelala, unamuita mtu wa ndani kwamba njoo tuzungumze au? Yaani ule mtiririko ukoje
 
Hapa kuwa na hatua yoyote,

Nilionyesha tu kutamani kuona kilicho ndani ya msingi Ule na kusema ndani Kwa ndani dhamira na kusudi la kuona wish yangu inatokea.

Ni kama tu mtu apotee au kukuta mtu aneuwawa Kisha ujisemee ndani ya moyo kuwa unapenda kuwajua watekaji.

Labda naweza Sema nilifanya maombi ya bila Kutoa sauti.

Na ninajua Kwa HAKIKA ndani yangu anakaa Roho mtakatifu hivyo naamini alisaidia kufanikisha Hilo.
 
Oh sawa mkuu, kwa hiyo ni suala la kiimani zaidi. Yaani lazima imani itumike kukamilisha mchakato.
 
Back
Top Bottom