The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Huyu karamagi kwanza ameaibisha kabila langu la wahaya kwa kuwa kwenye list ya mafisadi tena wanayofunga umma wa watanzania kwa mikataba mibovu. Hivi hataki kujifunza kuwa bunge lilimfukuza Zitto likafikiri limemaliza kumbe limezaa akina Zitto kibao pale jangwani, sasa huyu Karamagi atakipata kama ameona wanasheria wenzake wanamzidi mkono anayetetea serikali na ameamua kunyamaza kitakacho mpata atajua mwenyewe pamoja na wanamtandao wenzie wa Chama Cha Mafisadi (CCM)

Sisi tunamtazama Karamagi kama Mtanzania, waziri na kiongozi wa serikali yetu, wewe unamtazama kama Mhaya? Akifanya mema au mabaya unamtazama kwa uhaya wake au kwa kiapo chake? Kwani kuna kabila ambao lina watu wema tu, au wabaya tu?

Pole ndugu yangu, lakini...please, let's think beyond this level!
 
Hii ya kwenda mahakamani ni janja ya kuzima mjadala huu usiendelee hasa kwa magazeti na redio za bongo; watadai eti "suala hili lisijadiliwe hadi kesi itakapoisha"

... na hiyo kesi inaweza chukua zaidi ya miaka 5; tunakumbuka sana yale mabomu ya mrema!
 
Sina tatizo sana na mheshimiwa Karamagi kufungua kesi dhidi ya Dr. Slaa. Ila nina tatizo sana na kesi dhidi ya gazeti lililoripoti tangazo la Dr. Slaa na kampuni inayochapisha gazeti hilo. Makosa yao ni nini, anataka wasitoe taarifa za matukio mbali mbali kama yanavyotokea? Je kazi ya gazeti ni nini? Litafanya kazi kwa kuripoti maneno ya serikali na CCM tu lakini lisiripoti maneno ya vyama vya upinzani?

Kichuguu,

Hizo ndizo sheria ambazo baadhi yetu tunazipinga kila siku. Tunasema zifutwe. Kimsingi, hata kuandika tunayoandika ni kwamba tumeamua kuziasi. Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ndiyo inampa mlalamikaji nguvu ya kushitaki wote hao - wakiwamo wahariri na waandishi wa habari husika. Ipo. Ni miongoni mwa sheria dhalimu 40 ambazo Tume ya Jaji Mkuu Nyalali ilipendekeza zifutwe tangu miaka ya 90. Wamekataa, kwa sababu wanazitumia kutisha vyombo vya habari.

Tulidhani huyu bwana Kasi mpya angeingie na jipya, na walau kusaidia kuzifuta sheria hizi dhalimu. Naona serikali yake inatunga nyingine mpya, hata tusizohitaji.

Kila mara miswada inapelekewa Bungeni. Sheria dhalimu hazifikiriwi. Walipofikiria kuhusu vyombo vya habari, wakaunda muswada mchafu zaidi ya sheria zilizopo - tukaukataa.

Ndiyo maana baadhi yetu tunaamini kwamba Tanzania bado iko utumwani. Tunahitaji kuasi na kujikomboa. Tuliowaweka pale hawaoni haja hiyo, wanatafuta fursa nono kwa ajili yao navizazi vyao.

Jambo ambalo hatujafanikiwa kulifanya ni kupandikiza uasi huu hata kwa vyombo vya habari. Ndiyo maana, kwa kuogpa sheria hiyo na nyingine, na ndani ya kivuli cha 'maadili' vilichapisha stori ya mafisadi bila kuwataja majina. Hiki ndicho walichoogopa.

Mhariri wa MwanaHALISI namjua. Ni mkongwe. Ni kichwa. Ni muasi kwelikweli. Anaendelea kuwanoa vijana wadogo wadogo kama huyo mmiliki mwenyewe wa gazeti kujifunza kwamba uasi kwa ajili ya jamii ni jambo takatifu.

Kumbukeni, mahakamani haipatikani haki, bali mshindi. Ni wazi, kitaaluma na kitaratibu mahakamani ndiko tunakopaswa kupata haki. Lakini katikamisingi hiyo hiyo, tunajua kuwa hata asiye na haki aweza kushinda kesi. Suala la Ditto ni mojawapo ya mambo mapya yanayosisitiza hoja yangu hii. Kwa hiyo, tusishangae kina Ditto wako huru, huku wezi wa kuku wako ndani wanasota.
 
Nakubaliana nawe Ngurumo kwa 99%

Yale mambo ya akina Chonge na Maugwaju katika Tamthiria ya
Tende Hogo iliyoandikwa na ndugu Kaduma,yameanza kujitokeza.

Ilikuwa ni simulizi ya Kidato cha 3 lakini leo hiini kweli inatokea.
 
mwanakijiji,dua,mwafrika,kithuku,
..Kikwete ndiye waziri aliyeasisi sera ya uwekezaji madini Tanzania miaka ya mwisho ya 1990.

..Kikwete ndiye aliyeidhinisha kipengele cha Watanzania kupata 3% royalty.

..Watanzania tunapaswa kuwachunguza vizuri hawa watu kabla ya kuwapa uongozi.

That's why he needs to clean his mess.
 
Eti jamani

Huyu lisu sio mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu chadema? Kwa hiyo ni mwanasiasa?

Asha
 
Keil na Ngurumo.

Nashukuru sana kwa kunifahamisha kuhusu sheria hii isiyokuwa na mantiki. Haiingii akilini mwangu kabisa kuwa gazeti ambalo kazi yake ni kuripoti matukio bila twist yoyote linashitakiwa kwa kuandika habari sahihi kama zilivyotokea. Ingekuwa ni sahihi kama gazeti litathibitika kuandika habari za kutunga tu, lakini hizi ni habari sahihi kabisa zilizotokea, na hata Karamagi anajua kabisa kuwa zilitokea ndiyo maana anamshitaki Dr. Slaa aliyetoa habari hizo.

Kama wanadai kuwa habari zisiandikwe mpaka mwandishi azithibitishe tena kwa main character wa habari hizo, basi Tanzania hatutapata habari zinazotokea sehemu nyingine za dunia kwa vile waandishi wetu hawawezi kufika huko kuthibitisha habari hizo kwa characters wa habari hizo. Vile vile hawatandika habari zinazohusu watu waliokwisha fariki kwa vile hawataweza kudhithibitisha habari hizo na marehemu.

Tuna kazi kweli kweli!! Hivi kweli hii ndiyo Tanzania ya Information Age?
 
Mzee CMB heshima yako

Heshima mbele kwa kutuletea haya mahojiano. Nyuma tuliandika kuwa time will tell. Naona Jamvi linazidi kukunjuka. Kitendo cha Ikulu kukubali hoja ya Zitto aliyoitoa pale Jangwani kuwa Rais hakuwa na taarifa kuhusu kusainiwa kwa huu mkataba kiliashilia kuwepo kwa uvundo ndani ya mkataba wenyewe. Manake Mwalimu alituhasa kwamba Serikali ni timu. Kwamba mkusanyiko wa mawaziri na Rais wao bila mwelekeo huku kila mtu akibutua kivyake hauwezi kuitwa Serikali.

In fact, alichofanya Zitto ni kumwekea Rais wetu mpira juu ya tuta na Rais ametufunga goli kwa kujifanya alikuwa hana taarifa na utiaji saihi wa mkataba wa namna hii. Kwa wadadisi, Rais alijua kuwa ndani ya mkataba kulikuwa na Mzoga. Alichokimbia ni harufu itokanayo na uvundo wa huo mzoga. Alitambua kuwa punde harufu ya Mzoga itachafua hewa safi. Alipopata upenyo akajiengua kimachale.

All in all, as time goes by, ile misemo ya "win-win situation", na ujinga mwingine unaofanana na huo, inachukuwa sura ya ubabaishaji. At JF we often overlook the strength of the link between the so called large corporations such as Barrick Gold and our Government, and the extent to which both function as instruments of elite rule and are integrally linked. Wakati wa himaya za kikoloni, large corporations functioned as extentions of government power. Lakini sasa hivi our government is acting as extention of corporate power.

Huu utandawazi + corporate money now corrupt our political processes to the point that democracy has become a meaningless charade of all but the very wealthy (mafisadi). Of course, when "Karamangi + Barrick" faced with a conflict between profitability and health of our society, they consistently choose profits. Ni vema kutambua kuwa utandawazi is a legal instrument designed to concentrate economic power without accountability. Utandawazi hauna conscience na wala hauna loyalty to our people. It is inherently both anti-democratic and anti-market. I think the appropriate goal is to end it.

Yote tisa, kumi nimeyasikiliza mahojiano yaliyoendeshwa na Ulimwengu kwa makini. Kumbe ndio maana Barrick walipoambiwa kuwa Waziri Karamagi yuko London wakakimbia kumuwahi hukohuko ili wasaini ule mkataba. Jenerali Ulimwengu anapuuza mantiki ya kusaini mkataba London. Hoja yake ni kuwa hata mkataba ungesainiwa Mpanda, contents ndizo za muhimu zaidi kuliko mahala uliposainiwa.

Lakini msemo wa Kihaya unaelezea hii mantiki vizuri sana. Wanasema kwamba "Omulalu mbali akuela niyo oshabila". Tafsiri isiyo rasmi ni kuwa "Kichaa akikupa unamlala paleple". Usione aibu na kusema ngoja tujifiche kichakani, kwani atabadilisha mawazo. Pale Fire station Dar huwa kuna vichaa wengi wanaotoloka Muhimbili. Akikupea kwenye trafic right za Fire, unakula vitu palepale, ukiona haya kwa kuogopa alaiki ya wapitao njia na ukataka mkajifiche, anabadilisha mawazo. Hii ndiyo "globalization" na hivi ndivyo "large corporations" zinavyoifanya nchi yetu. Mwaka jana hata Mocrosoft aliipatia Serikali ya JK siku tisini pale South Afrika kusaini mkataba wao na wakafanya hivyo. Large corporations zinajulikana kwa ugonjwa wa mfadhaiko wa fedha. Wakikutana na vichaa wanafanya kweli.
 
Mzee Mwanakijiji,
Unajua kwenda mahakamani wengi tunapenda lakini kumbuka mshitaki siku zote ndiye hutakiwa kuwa na ushahidi.. Sasa sielewi kama Karamagi anao ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Dr.Slaa amemzuria maneno ya kumchafua.

Ni yeye atakaye takiwa kuonyesha ukweli wa shutuma hizi kama mshitaka na Dr. Slaa hana haja ya kuonyesha chochote hadi pale itakapo hitajika... na atakacho fanya Dr. Slaa, ni kumshinda Karamagi kwa kusimamisha mashahidi wote waliokuwa ktk deal hizi ambao kisheria watalazimika kusimama kizimbani na kusema ukweli ambao hawakuweza kuusema ktk magazeti yetu. Karamagi hafahamu Dr. Slaa kazipata habari hizi toka wapi? na ni akina nani wanaompa hizi habari!.... kazi kweli kweli!
Sidhani kama Karamagi yuko tayari kuwafumba kinywa wale wote waliohusika na scandal zake!..
Naona kama kesi zote za Rada, IPTL, Richmond, ndege ya rais, BOT zinaweza pata siku yake mahakani!
 
As Karamagi refuses comment on shadowy deal

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi (pictured above) yesterday declined to comment on the latest reports of alleged irregularities in the $400m (approx. 520bn/-) Buzwagi gold mining contract.

Addressing a news conference in Dar es Salaam that he himself convened to express his intention to sue opposition Member of Parliament Dr Wilbrod Slaa (Karatu-CHADEMA) and a tabloid newspaper for alleged defamation, the minister chose to dodge a barrage of questions from journalists specifically on the Buzwagi deal.

''I have called you here in my personal capacity as Nazir Karamagi - not as a cabinet minister of this government,'' he declared, although the news conference was conducted at the headquarters of the Ministry of Energy and Minerals in the city.

Asked directly to comment to the media reports outlining details of the controversial Buzwagi pact and his own role in it, an evasive Karamagi responded with the refrain: ''Please don't ask me anything about the Buzwagi contract today?I am here to speak about my defamation in person and not in my capacity as a minister.''

Instead, he concentrated on announcing that he had instructed his lawyers to immediately begin civil litigation proceedings against Dr Slaa, the Kiswahili weekly tabloid MwanaHalisi, and the private newspaper printing firm Printech.

Karamagi said the pending lawsuit against Dr Slaa is in response to the inclusion of his name in a list of top government and public leaders alleged to have been involved in various shady monetary deals in recent years, unveiled by the legislator at a public rally in Dar es Salaam.

Asked if he also planned to sue another CHADEMA MP, Zitto Kabwe (Kigoma North), for first raising the Buzwagi contract issue both in and out of parliament, Karamagi said his lawsuit will zero in on Dr Slaa.

''I didn't hear Zitto making any serious allegations against me at the Mwembeyanga public rally (in Temeke District, Dar es Salaam). So, he won't be in my lawsuit,'' said the beleaguered minister.

According to Karamagi, Dr Slaa made the alleged defamatory remarks at the public rally on September 15 this year, which is also where he produced his now-famous 'List of Shame'.

Still, most journalists at the media conference appeared more interested in the Buzwagi contract and less in the planned lawsuit, and continued to try to pin down the minister on the matter.

Asked by one journalist to explain why the agreement had to be signed in London, he remarked: ''It seems you don't realize that I didn?t travel to London to sign the (Buzwagi) contract.''

More questions were thrown at him as he left the conference room on the fifth floor of the ministry's headquarters building, including whether or not he would step down over the allegations. But he remained tight-lipped.
 
Nilikuwa ninapitia orodha ya mafisadi kama ilivyowekwa na Mzee FMES lakini orodha hiyo imeishia namba 8, bado kuna majina matatu hayaonekani na majina hayo ni ya UTATU BADHIRIFU a.k.a Mtandao Founders. Naomba aliye na details za tuhuma za Karamagi aziweke ili tuone kama ana hoja ya kwenda Mahakamani. Kama hoja ya mkataba wa Buzwagi itakuwa ni moja ya vitu alivyotuhumiwa navyo basi nina uhakika kwamba hawezi kwenda mahakamani, na kinachofanyika ni kupoza makali. Naomba mwenye tuhuma dhidi ya hao watu 3 wa mwisho aziweke hapa ili tupate upande wa pili wa shilingi na tuone kama NK ana hoja au anatapata!
 
Karamagi, Buzwagi, na Mkate wa Siagi...

soon utakuwa mkate wa shubiri.The guy anatapatapa kama mmemsikiliza vyema alikuwa na shaking tone kwenye voice yake wakati anajiumauma akisema NAAMINI MIMI NI MUADILIFU. Body language yake could tell it all, hata vidole vyake vilikuwa vikichezacheza katika meza. Poor him kwa kujidhalilisha.
 
soon utakuwa mkate wa shubiri.The guy anatapatapa kama mmemsikiliza vyema alikuwa na shaking tone kwenye voice yake wakati anajiumauma akisema NAAMINI MIMI NI MUADILIFU. Body language yake could tell it all, hata vidole vyake vilikuwa vikichezacheza katika meza. Poor him kwa kujidhalilisha.

Hata siku alipokuwa akijibu hoja ya Zitto nilimuona alikuwa kama alikuwa anatetemeka na alipata nguvu pale wabunge wa CCM walipokuwa wakipiga makofi na kujifanya anasisitiza na kuomba kurudia maneno aliyokuwa anasema. Akumbuke kwamba mahakamani siyo kule kwenye kijiwe cha soga cha CCM chini ya Anko Six ambako ushabiki wa kiitikadi unaweza kukupa 'confo' na kukufanya uonekane shujaa. Yetu macho na masikio na soon tutasikia nini kinaendelea.
 
Kinyau asante maana sikuisoma vizuri hiyo taarifa yake. Anasema "naamini mimi ni mwadilifu". Unajua mambo ya imani mabaya sana.. kuna wakati mimi naamini kuwa natoka sayari ya Zuhura. Na wakati mwingine naamini vitu vya ajabu ajabu kweli. Sasa kwa vile hajui kuwa yeye ni mwadilifu, naona amebakia kuwa na imani tu.. tatizo wakati mwingine imani inakuwa ni imani potofu isiyo na msingi wa ukweli!
 
Huyu bwana anawaletea wenzake balaa. Huyu ndio ameanzisha hili sokomoko lote la kina Zitto na Slaa na upinzani. Sasa huko mahakamani kitakachotokea ni mikataba yote kutakiwa kuwekwa hadharani ili kuona kama hakukuwa na rushwa. Hapo itakuwa balaa kubwa zaidi. Naanza kuamini maneno ya MKJJ kwamba hakuna cha mahakamani wala nini. Natabiri pia kwamba kuna mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri yanakuja. Let's wait and see his reaction when Muungwana atakapofika bongo
 
Tanzania government miss critical thinkers. I guess huyu Karamangi hajui anything concern contracts law. Probably anadhani hii mikataba ni sawa na mikataba ya Nyumba, kwamba unaweza kumsainisha mtu, kisha ukamfukuza siku ukijisikia na hakuna atakaye kubabaisha. He is missing the point kwamba as soon alipo angusha sign yake, we was bound into it. He trap us in the long time tragedy, hatuwezi kubleach hizi contract sababu WTO will be all over the place.

Wanaojua sheria za Tanzania, kuna any way wananchi wanaweza kumshitaki kiongozi kama huyu karamangi kwa kututrap in this mess, thats the only way we can do as a pay back. Hatuna other option zaidi ya kumfunga, au kuvunja mkataba kisha tukaanza kubishana na WTO and all other big fishes.
 
ha,ha ha nimecheka sana. Mimi nahisi aliandikiwa ile hotuba sasa alipofika kwenye hayo maneno "naamini mimi na muadilifu" akajishauri kweli ayaseme haya matamshi hadharani, hivyo dhamira yake ilikuwa inamsuta. Tusubiri kama mahakama itakubaliana na hiyo IMANI yake ya uadilifu au la.
 
Naamini hathubutu kwenda mahakamani. Anatishia tu kama JK alivyotishia wakati ule alipoandikwa kwamba amepokea $20 milioni toka Iran. Aling'aka "Nitakwenda mahakamani!" Thubutu! Ukweli zaidi ungetoka!

Karamagi ataelezwa (kwani inaelekea mwenyewe hana uwezo wa kuona mambo vizuri) kwamba ukienda mahakamani basi wakili wa Dr. Slaa atataka apewe mkataba wa Buzwagi. Akienda mahakamani ataulizwa details zote za kwa nini aliusaini hotelini, nani alikuwepo, mihuri alikuwa nayo mfukoni au vipi, kwa nini ilibidi viongozi wa Barrick watoke Dar wamfuate London, n.k.

Naungana na Mzee Mwanakijiji kusema haendi mtu mahakamani. Amekurupuka baada ya kusikia wengi wanauliza kwa nini walioshutumiwa hawendi mahakamani. WANAOGOPA!

Kuna mmoja ameuliza kwenye kurasa za nyuma kama kesi ya Nyari iliamuliwa na Jaji. Jibu ni ndiyo. Aliachiwa huru na Jaji Othman Chande wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Inatisha kweli!
 
Back
Top Bottom