Teuzi za Magufuli zinadhihirisha hakujiandaa kuwa rais

Kwa maneno yake akiwa mapumzikoni Chato Magufuli alisema alikuwa anajaribu akajishutukia ni rais. Kwa maneno yake alisema "wapiga kura wa Chato mnisamehe, mi nilikuwa nabip tu mkanipokea"

Uteuzi kama wa akina Nape, Kippi Warioba, Masauni, Makonda, Hapi, Makinda, Mwampamba, Pole Pole, Gondwe nk ni uteuzi wa kuwafurahisha Ccm hasa linapokuja suala la kunyimwa uenyekiti. Hakuonekana kada na kama si nguvu ya taasisi ya urais alikuwa anapigwa chini. Unateua mtu kwa sababu alipigwa na spika??? Sehemu nyingine ameteua watu waliotumbuliwa na watendaji wake, mfano wakurugenzi wa Bukoba mjini na Msoma walikuwa wamesimamishwa kazi na wateule wake akawapa u-DC!

Kigezo cha ujana na usomi ni kuficha 'udhaifu'. Kinachotakiwa ni perfomance na uwezo wala si ujana wala usomi. Tukimuuliza Magufuli aliwateua wapi kabla vijana wakaonyesha kukidhi matakwa ya uchapa kazi? Au aliwaona wapi wasomi wakichapa kazi kwa uhakika? Mtu aliyetuaminisha kwamba si mwanasiasa na akasema "mavyama yanatuchelewesha" leo anajaza makada nafasi mbali mbali!
Wateule wote wa Pombe MaGufuli wakikutana pamoja ni kama Kigango
 
Jamaa yetu anasaidia kuimaliza CCM na akiendelea hivi mpaka 2020 basi milioni sita itaruka mpaka millioni 12 watake wasitake na hapo kuiba kura itakuwa ngumu kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano
 
Unatamani kweli ingekuwa hivyo....Lakini wapi....
Kila siku unaomba Rais ashindwe na aonekane ametengwana kuhakikishia utasubiri sana. Tuko nyuma yake wengi tuuu
Labda na wewe ni mteule
 
Iviiiiii
Magufuli kafanya jambo gani zuri embu mniambie
Mana m hata silion naona yote mabaya hakujipanga
 
Hata mkimpinga magufuli yeye ndio Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mpaka 2025,Nadhani hizi kelele za uteuzi mnazipiga tu hata kama angekuja mtawala mwingine angeteua kulingana na vigezo vya kiutendaji, cha msingi na nyie unganeni mfanye kazi kama kigezo cha uteuzi wenu kutoka kwa mungu, Nashangaa mnaongelea na kumlilia lowasa ambae sio Rais na hatakuwa Rais Tanzania hii. Tatizo la pili mko iddle sana hamtaki kwenda mashambani kulima au kufuga walau na wewe uwe na kazi ya kufanya kama hao Dcs walioteuliwa. Tatizo la tatu mliwekeza nguvu na pesa nyingi sana mkitegemea Lowasa atakuwa Rais then atawarudishia fadhila na sasa hazipo na hazitegemewi hata kidogo kuwepo so Loss mlioipata mnaona hakuna namna ya kuirudisha. Hapo ulipo geuka nyuma tafakari baba na mama yako wanataka msaada wa trekta,mbegu,na pembejeo zingine kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo halafu huna hata senti tano unasubili kampeni zije upate fedha. Lets change jamani twendane na wakati utakuwa kila siku unachungulia vijiweni magufuli anasemaje,kamuapisha nani na alieapishwa ana sifa gani...kila siku utakuwa vijiweni tuuu..hatari sana hiyo. Anyway napita tuu nilikuwa nina mda kwa sababu leo sikukuuu...EID ELFITRI...
 
Kwa maneno yake akiwa mapumzikoni Chato Magufuli alisema alikuwa anajaribu akajishutukia ni rais. Kwa maneno yake alisema "wapiga kura wa Chato mnisamehe, mi nilikuwa nabip tu mkanipokea"

Uteuzi kama wa akina Nape, Kippi Warioba, Masauni, Makonda, Hapi, Makinda, Mwampamba, Pole Pole, Gondwe nk ni uteuzi wa kuwafurahisha Ccm hasa linapokuja suala la kunyimwa uenyekiti. Hakuonekana kada na kama si nguvu ya taasisi ya urais alikuwa anapigwa chini. Unateua mtu kwa sababu alipigwa na spika??? Sehemu nyingine ameteua watu waliotumbuliwa na watendaji wake, mfano wakurugenzi wa Bukoba mjini na Msoma walikuwa wamesimamishwa kazi na wateule wake akawapa u-DC!

Kigezo cha ujana na usomi ni kuficha 'udhaifu'. Kinachotakiwa ni perfomance na uwezo wala si ujana wala usomi. Tukimuuliza Magufuli aliwateua wapi kabla vijana wakaonyesha kukidhi matakwa ya uchapa kazi? Au aliwaona wapi wasomi wakichapa kazi kwa uhakika? Mtu aliyetuaminisha kwamba si mwanasiasa na akasema "mavyama yanatuchelewesha" leo anajaza makada nafasi mbali mbali!
Hili swali la aliwaona wapi kabla ya kuwateua na uchapakazi wao aliujuaje ulishwahi kuhoji Katibu wetu wa chama pendwa alionekana wapi na uchapakazi wake ulionekana wapi mpaka akapewa hicho cheo akiwaacha waliokuwa wakitabiriwa kwa miezi kadhaa?
 
Ukitaka kuteuliwa na magufuli jitahiidi uwe na mashamba matatu ya ekali 200, kiwanda cha kusindika mazao yako uliolima,Kampuni ya kusafilisha bidhaa iliotokana na kiwanda chako, Lazima JPM akuteue lakini kama ndio unapiga story mtaani,unazunguka kwenye mitandao ya jamii,kila siku uko kwenye vilabu .hatari kweli hata mzazi wako hawezi kukuteua kuwa mshika mikoba baada ya yeye kustaafu au kuzeeka
 
Hakujiandaa na amekuwa rais hajiamn na haelewi afanye kip kwa watanzania sukar bei imemshinda lugumi imekwama mita ya mafuta imefukiwa anarukaruka tu
 
Mlivyomteua Lowasa kugombea huko ukawa na nyinyi mlikuwa mmejiandaa?, vyama vinne vilikuwa vinasubiria hatima ya uchaguzi ccm, mkaishia kudondokea pale, mlijiandaa kushika dola nyinyi?
 
Hivi Amon Mpanju amewahi kuwa mtumishi wa umma!? Mbona uteuzi wake kuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya sheria na katiba haukupigiwa kelele namna hii!? Ni nani asiyejua kuwa Mpanju ni mwanaCCM mtiifu na alishiriki kwenye mchakato wa kura za maoni katika kuusaka ubunge jimbo la Kawe kupitia tiketi ya CCM. Tuache double standards.
hata hivyo hongera sana mkuu kwa kupata uDAS,muombe Mungu jamaa wasijishtukie,wazibe masikio la sivyo watakutengua.Makosa yaliyofanywa kwa Amoni hajawezi kuhalalisha makosa ktk uteuzi wako.Usitulaumu sisi,laumu kanuni na sheria
 
Magufuli ameonesha kuanguka katika uongozi
Ila halionekani kwasababu hapendi kukosolewa
Of course ameanguka maana utendaji kazi serekalini umeboreka, kodi zimeongezeka, mgawo wa pesa za maendeleo umeongezeka, watoto kukaa chini I marufuku na imewezekana baada ya kushindikana Zaidi ya miaka 30! Ni kweli ameshindwa!
 
Back
Top Bottom