TEMBO WAMEKULA MPUNGA WETU LINI SERIKALI ITATULIPA FIDIA?

Kwenye utawala huu sheria zimewekwa mfukon kilicho ni mabavu sheria zilikuwepo kiping cha mkwere

Mkuu.....vipi.....?....mbona unaandika kinyume.......uchagani tunaita kiphuryi......
 
Kuna watu humu ndani huwa wapenda kuchangia kila mada tena kwa dhihaka na kejeli. kama huna cha kuchangia juu ya mada husika ni bora kukaa kimya au kusoma mawazo ya wenzio.
Jamaa kaleta mada ya muhimu mwingine anachangia bila ya kushirikisha ubongo.
Umewahi kutafakari kwa nini ukame uliotekea miaka michache tu iliyopita na kuua ng'ombe wengi mikoa ya Arusha na Manyara na Serikali iliwafidia. kwan Serikali ndo ilileta kiangazi?
Nashauri Mamlaka husika zishughulikie swala hili kwana wananchi hao ndo walinzi wa kwanza wa tembo hao. Pia mazao yanayozalishwa hapo ni faida ya Taifa zima.
Sioni tija kwa Serikali kutumia gharama kubwa kujenga mradi huo alafu wakulima wapate hasara ya kuwekeza vi mitaji vyao na kukata tamaa hivyo kushusha uzalishaji wa chakula nchini.
 
Minaona ni haki Yao kudai serikali iwalipe kwa sababu ukiua tembo unashtakiwa kwa sbb ni Mali ya serikali.
Kwa kawaida kunakuwaga na askar ranger wanaowalinda wanyama ili wasiingie kwenye makaz ya watu. Swali je hao askar walikuwa wapi had wanyama waingie na Kula mpunga?
 
Kwani serikali ndo ilikula mpunga wenu?????????

Kawambieni Tembo wawalipe
 
Katika Kijiji cha Mariwanda tarafa ya Mugeta wilaya Bunda jimbo la Bunda vijiji amboko kuna mradi wa serikali wa kilimo cha umwagiliaji cha mpunga kwa kutumia bwawa. Watu wengi sana wamehasika na kilimo hiki ambacho kwa kweli ni cha uhakika na kinalipa.

Shida kubwa inayowakabili wakulima ni tembo kutoka hifadhi ya Serengeti ambao huja mashambani na kula mazao. Mwezi wa kumi mwaka jana makundi makubwa ya tembo yalivamia mashamba ya mpunga na kuteketeza eka nyingi sana za mpungu. Kwa wakulima wengi tulipata hasira kiasi kwamba mitaji imekatika. Baada tukio hilo tulijaza fomu za madai kupia kwa ofisa kilimo lakini cha ajabu hadi sasa hutujui hatima yetu.

Tunaomba wizara husika ituangalie ili haki zipatikane.
Pole sana. Kilimo cha kisasa kina gharama lakini, kwa hali ya kawaida, unavuna sana. It's high time serikali iangalie jinsi ya kusaidia wakulima pale wanapopoteza mazao kutokana na natural disasters. Endelea kupaza sauti mwishoni watakusikia.
 
Tembo angepotelea kwenye mpunga ndio ingekuwa hoja kuu ndani ya serikali.
 
Wewe upo kwenye focal area yangu ya project. Nitafute au text "0629298812".
Nakujibu: Jana tar 12/1/2016 mheshimiwa Jenister Mhagama, wabunge wote wa bunda (Bulaya, Kange etc) walikuja kihumbu kijiji karibu na mwariwanda, huko kuna wakulima walipiga simu kwamba tembo wamevamia mahindi lakini cha ajabu jana waheshimiwa wanafika wamekuta hali ni ya kawaida sana. ni sawa na kusema mbuzi mmoja amekula mazao. Yameliwa kidogo sana mpaka tukawa tunatafuta wapi alipokula tembo. Ninachojua mm huwa nakuja kuja huko na matatizo ya tembo mmeniambia ni kijiji cha kihumbu, mariwanda na serengeti. na haya matatizo tumeyawasilisha mahali husika majibu ya haraka ni kwamba; hifadhi ya maliasili wametoa askari ambao watakuwa wanalinda ktk miradi ya umwagiliaji ili tembo wasiweze kuharibu mazao, majibu hayo hayakutosha ndpo wakashirikishwa hao wadau waliokuja jana huko. Tatizo lenu linashughurikiwa sana na lipo mbali ktk kutafuta majibu zaidi, hao maafisa kilimo unaowatuhumu tumeshirikiana ktk kutafuta suluhu ya huko. Tulia waheshimiwa hawajatawanyika bado, pia ujue wanatambua sababu za kwanini miradi ya hayo maeneo haifanikiwi kama itarajiwavyo, na sababu mojawapo ni hii ya TEMBO, sababu zingne znatatuliwa kwa urahisi. Pllease nitext nikujibu hatua zaidi zinazochukuliwa kuhusu huko kwenu, ila muwe wawazi msitumie historia kuripoti tatizo bali toeni taarifa sahihi za majira hayo ya tukio
 
Back
Top Bottom