TCRA tutaipata wapi tena BBC radio?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,552
Jana niliona taarifa ya kuzinduliwa radio mpya ya ndugu Joseph kusaga na kwamba radio hiyo imepewa frequency zilizikua zikitumiwa na BBC radio na kweli usiku Jana sikuipata BBC radio kwa Mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa ambapo nimekua na kawaida ya kusikiliza tedio hiyo usiku nitokapo kazini.

Ukweli ni kua radio ile ilikua msaada sana kwangu na kwa yeyote anaetaka kujua dunia inaendaje kwa masaa yote tofauti na radio zetu ambao muda huo Wa usiku huwa ni muziki mfululizo na stories zingine.

Ombi kwa TCRA tunaomba tujuzwe ikiwa hawa BBC wanapatikana wapi au watapatikana wapi kwa maana ya masafa kwani kupitia hapa sie hupata habari nyingi na matukio mengi yanayotokea duniani wakati wote.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…