TCRA Polisi wako wapi watu wanaibiwa kupitia hii mikopo mtandaoni? Jerry Silaa msaidie Rais

Doslamari

New Member
Jun 21, 2024
4
1,498
Kuna wimbi kubwa sana la matapeli likitumia majina ya watu maarufu km Mohamed Dewji(MO), Tulia Ackson, Jokate Mwegelo n.k. Hawa watu ni matapeli na wana mtandao mkubwa, unakuta kwenye comments wanashukuru kuwa wamepata mikopo kumbe ulaghai ili uiingie mkenge. Namna ya kukuingiza mkenge watakuambia weka akiba au lipia riba kabla, hv kwanza wanaelewa maana ya riba? Ukiwatumia hiyo hela watakuambia watumie hela ya kufungua akaunti ambayo ni kubwa zaidi ya ht hiyo riba. Kwa ufupi ni majambazi. Mtu akiwa na dharura kweli huingia mkenge, hawana huruma. Nauliza nani wa kuwalinda wananchi? Kumbukeni shida haina adabu. TCRA wanashindwa kuwabaini na ht kufunga haya maujinga yao? Wanatumia sana facebook.
Kuna hawa wengine kazi yao kudhalilisha watu, mtu hujui chochote unapigiwa simu kuwa unadaiwa au kuna mtu umemdhamini kwa hiyo mlipie, wana namba za simu nyingi sana mfano wanajiita PesaPlus, PesaX, FiniLoan, RocketLoan n.k. Hizi namba TCRA hawazioni? Mtu moja anawezaje kumiliki line nyingi hivi? TCRA na Police kitengo cha Cyber wako likizo au wamelala? Au wanashirikiana ns hawa wezi? Lini wataamka usingizini au ni mpk lini watanzania waibiwe? Mh. Rais we ndio mlinzi wa raia wa nchi, naomba wasaidie wananchi wako. Jerry Silaa tunajua we ni jembe uko wapi umsaidie mh. Rais?
 
Wapo bize kudhibiti maandamano na vikao vya chadema
.
Umeibiwa mara Moja tu ndo upige kelele nchi nzima?

SI ungesubiri uibiwe hata mara sita ndo uje ulalamike?
 
Hili nalo ni tatizo kubwa sema limezidiwa uzito na tatizo la kupotea kwa watu na mauaji, ikiwa wataanza kushughulikia basi waanze la mauaji. Uhai ni bora kuliko pesa.
Tukimaliza kule tutakuja huku kuwa na subra mwananchi mwenzangu, mana si unajua nchi yetu.
 
Polisi watakwambia wao sio regulator wa mikopo, hvyo nenda BOT
huko bot nao wamesahau wajibu wao wapo kmya kwa kukwepa majukumu
 
Back
Top Bottom