Tatizo la Makufuli.....

Kuwa makini na vitu mkuu, hilo neno la Watanzania umeliongeza mwenyewe, yeye wala hakutaja jina lolote tofauti na huyu aliyetaja jina
Kwa hiyo aliwaambia Wagagagigikoko au watu gani kama sio Watanzania au wewe ndio hauko makini.
 
Mhhh!Pasco,umewakanganya mno!!Lakini wengine tumekupata vyema hasa sisi vijana wa zamani na ambao tuliowahi kusoma vitabu vya mashairi vya Snow white, tatizo la makufuli yanapokuwa mengi ya aina moja hasa haya ya kichana ni lazima yakuchanganye na hasa haya ya kichina. Tumuombee mungu Mheshimiwa wetu rais Magufuli aendelea na kasi aliyonayo huenda nasi tutafanikiwa kuwa na viwanda vyetu vya kutengeneza makufuli yetu. .
Mkuu Lipijema, asante kwa bandiko hili, kusema la ukweli siku hizi Kiswahili ni kigumu, ndio maana nikaomba kabisa nisiulizwe swali lolote.

Sasa naendelea na uzi wangu kuhusu tatizo la makufuli, ila kabla sijaendelea, naomba kuwaeleza kidogo baadhi vipaji nilivyo zaliwa navyo, ni kipaji cha unajimu, ambao ni uwezo wa kujua mtu anafikiria nini hata kabla hajatamka kitu.

Mfano kwe uzi huu, niliposema tuu kuwa makufuli ni tatizo, kuna wengi walikimbilia kuufungua uzi huu na makasoma kwa macho yao, nimeandika kabisa makufuli, lakini wao mawazo yao yakawatuma kuwa nilimaanisha Magufuli!. Mimi nazungumzia makufuli tena yote mawili na sio Magufuli.

Hivyo naomba sasa nianze kwa tafriri kwa
1. kufuli (wingi makufuli)-kifaa cha madini kinachotumiwa kufungia milango, sanduku, kabati, au kufungia kitu chochote kwa kutumia funguo!. kufuli=padlock kufuli na ufunguo=Padlock and Key
kufuli moja=one padlock
kufuli mbili = two padlocks
wingi wa Kufuli sio makufuli ni Kufuli=plural of kufuli is Kufuli not makufuli

2. Msemo wa kisasa kumaanisha nguo ya ndani.

Hivyo makufuli kwa maana zote mbili kwa siku hizi ni shida. Makufuli ya zamani yalikuwa yanadumu sana, makufuli ya siku hizi hayadumu.

Na yale makufuli mengine ya kisasa nayo ni shida. Makufuli ya zamani ni cotton, ya siku hizi ni plastiki, motokeo yake na hili joto la tropiki ni shida!.

Zamani kufuli ni vazi la heshima, mtu hawezi kuvaa hata mstai tuu wa kufuli kuonekana, siku hizi haswa dada zetu, wanativalia nguo nyepesi kwa makusudi kabisa ili tuone....Wengine kutokana na hili joto, wanavaa zile za mikanda tuu, G-String hivyo kudhania mtu hajavaa kabisa!.

Hivyo kiukweli mambo ya makufuli siku hizi ni shida, na taabu tupu, au sio kweli?!.

Asanteni na Jumamosi njema!.

Pasco

Sasa tukiwa tunamsubiri mkuu Pasco mimi ngoja nichokoze zaidi.

Neno lililotumiwa kwenye facebook kama utusi ni neno "BWEGE".

Hili neno katika kamusi ya TUKI lina maana "good for nothing, simpleton, oaf, lemon" au kwa kifupi mtu dhaifu katika maamuzi.

Kwa mfano: Kama mtu atanichokoza mtaani ili tupigane lakini mimi nikiwa mpole kuepusha shari basi kuna wale watakaoniona kuwa -
  • nina busara kubwa ya kuepusha ugomvi
  • na kuna wale watakaoniona "BWEGE", sina ujasiri wa kumzaba makofi, n.k.
Hivyo basi kuitwa bwege sio utusi bali ni maono (opinion) ya mtu kuhusu ujasiri wa huyo aitwae bwege.

Tusubiri mahakama itasemaje.

Tunaitana na kutukanana matusi ya nguoni humu na tunaachilia mbali tu. Raisi, kwa upande mwengine anapaswa kuheshimiwa na kutovumilia utusi kwake. Hii ni kwa sababu kumtusi raisi sio kumtusi Mh. Magufuli pekeyake kama John, bali kuitusi taasisi nzima ya URAISI (Presidency).

LAKINI, kwa matumizi ya hili neno "bwege" sidhani kumefikia kiwango hicho cha utusi.

Haya niliotoa ni maoni yangu tu. Niko tayari kuswekwa kizimbani kujieleza.
 
Wanabodi,

Nina tatizo kubwa na makufuli na mambo ya makufuli au kwa lugha nzuri zaidi, makufuli ni tatizo.....

Sasa kabla sijaeleza tatizo langu na makufuli, na hayo mambo ya makufuli, lakini kufuatia taarifa ya uwepo wa mtu aliyefikishwa mahakamani jana na kushitakiwa kwa kosa la kutumia lugha isiyo faa na isiyo ya staha kwa Mkuu wa Nchi kule facebook, hivyo kabla sijaumalizia uzi huu kuelezea tatizo langu na makufuli, naomba mnipe muda kidogo, niifutilie hiyo kesi, ndipo niendelee na uzi huu, haswa kwa kuzingatia uwezekano wa kutokea mkanganyiko wa kimatamshi kuhusiana na mambo ya makufuli.

Wakati nikijiandaa, naomba na wewe unaesoma hapa, kuwa mvumilivu japo kidogo tuu, kwa kutokuniuliza jambo lolote kuhusiana na uzi huu, mpaka nitakaporejea kuwaeleza tatizo la makufuli!.

Nawatakia subira njema na Jumamosi njema, ila kiukweli makufuli ni shida, makufuli ni tatizo!.

Ni shida gani, na ni tatizo gani?, nisubirie nitarejea....

Pasco

Nimerejea....

Mkuu Lipijema, asante kwa bandiko hili, kusema la ukweli siku hizi Kiswahili ni kigumu, ndio maana nikaomba kabisa nisiulizwe swali lolote.

Sasa naendelea na uzi wangu kuhusu tatizo la makufuli, ila kabla sijaendelea, naomba kuwaeleza kidogo baadhi vipaji nilivyo zaliwa navyo, ni kipaji cha unajimu, ambao ni uwezo wa kujua mtu anafikiria nini hata kabla hajatamka kitu.

Mfano kwe uzi huu, niliposema tuu kuwa makufuli ni tatizo, kuna wengi walikimbilia kuufungua uzi huu na makasoma kwa macho yao, nimeandika kabisa makufuli, lakini wao mawazo yao yakawatuma kuwa nilimaanisha Magufuli!. Mimi nazungumzia makufuli tena yote mawili na sio Magufuli.

Hivyo naomba sasa nianze kwa tafriri kwa
1. kufuli (wingi makufuli)-kifaa cha madini kinachotumiwa kufungia milango, sanduku, kabati, au kufungia kitu chochote kwa kutumia funguo!. kufuli=padlock kufuli na ufunguo=Padlock and Key
kufuli moja=one padlock
kufuli mbili = two padlocks
wingi wa Kufuli sio makufuli ni Kufuli=plural of kufuli is Kufuli not makufuli

2. Msemo wa kisasa kumaanisha nguo ya ndani.

Hivyo makufuli kwa maana zote mbili kwa siku hizi ni shida. Makufuli ya zamani yalikuwa yanadumu sana, makufuli ya siku hizi hayadumu.

Na yale makufuli mengine ya kisasa nayo ni shida. Makufuli ya zamani ni cotton, ya siku hizi ni plastiki, motokeo yake na hili joto la tropiki ni shida!.

Zamani kufuli ni vazi la heshima, mtu hawezi kuvaa hata mstai tuu wa kufuli kuonekana, siku hizi haswa dada zetu, wanativalia nguo nyepesi kwa makusudi kabisa ili tuone....Wengine kutokana na hili joto, wanavaa zile za mikanda tuu, G-String hivyo kudhania mtu hajavaa kabisa!.

Hivyo kiukweli mambo ya makufuli siku hizi ni shida, na taabu tupu, au sio kweli?!.

Haya wale wote mliondani ninamzungumzia Magufuli, hadi kunidhania nimekosea, niombeni msamaha, na ninawashauri next time kuweni makini kusoma kilichoandikwa na sio kilichomo ndani ya mawazo yenu.

Jee kwenye unajimu wangu, nimepatia, niliposema makufuli, wewe mawazo yako yakaenda kwa Magufuli?!. Kama ni ndio, then mimi ni mnajimu wa kweli, nimefungua ofisi kama ya Sheikh Yahya ila ya kwangu ni online, tayari pesa, njoo inbox nikutabirrie maisha yako yote, pia nina dawa ya kupata pesa na kukufanya kuwa tajiri!.

Asanteni na Jumamosi njema!.

Pasco
Ng'wanangwa utatumbuliwa!! Mimi simo, wenzio siku hizi hawachelewi kutafsiri kwamba unamsema Rais!
 
Back
Top Bottom