Tathmini ya makabiliano ya CHADEMA na vyombo vya dola tarehe 23 Septemba 2024

Hao vijana watapatikana kwa mfumo upi wa elimu? Kwa sababu vijana wote wanaohitimu vyuo leo wanawaza ufisadi. Wanataka fedha bila kufanya kazi na wanataka anasa!

Mkuu 1961 Nyerere alipokuwa anahamasisha vijana 1954 tulikuwa na elimu? Elimu ni nini? Kwa kiasili binadamu ana elimu ya kutosha, anajua nini ni kitu kizuri nini ni kibaya. Anajua nini ni kuhimu kwa Taifa lake au siyo?
 
Unahitaji upinzani thabiti, serious, usio na udini, ukabila, ukanda, dharau kwa Watanzania ndani yake.
Unafikiri mfano hii CDM ikipata madaraka kesho Lissu, Mbowe, Lema, Mrema ndio viongozi wakuu kutakuwa na tofauti yoyote kwa Mtanzania wa kawaida? JPM alileta tofauti kwa Mtanzania wa kawaida mkampinga, mkamtukana, mkamwita mshamba, dikteka uchwara akaamua kuwa dikteta kamili.

Kiufupi CDM haiwezi kuungwa mkono na Watanzania wengi, watapata support ya watoto wa mjini, makabila, dini kadhaa basi.

Inahitajika upinzani mpya utakaoanzishwa na vijana wote wa Kitanzania. Wakipigia rasilimali zao zitumike vizuri, kuondoa kodi, tozo, kandamizi, uwajibikaji serikalini kwenye kila sekta.
Upinzani upya kutoka wapi ?
 
Mwambieni Samia kama hataki vyama vingi avifute, atawale tu yeye na familia yake mpaka mwisho wa dunia.
relax gentleman 🤣

upende usipende,
umoja, amani na utulivu wa waTanzani, utalindwa kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote ile bila kujali mbambamba za mtu au Taifa lolote Duniani.

Hakuna mzaha, hakuna aibu na hakuna hurumu kwa yeyote atakaethubutu kujaribu kuvuruga au kuhatarisha usalama wa waTanzani 🐒
 
Upinzani upya kutoka wapi ?
Kwa vijano wote wa Kitanzania wasiokuwa na maoni mabovu ya kichama,kidini, kikabila kiukanda. Kama Kenya, Sri Lanka, Bangladeshi, Malema, Nyerere, Mandela,Traore. Huwezi kusikia wanaongelea wasukuma , wanamsifu mtawala kwamba anaupiga mwingi. Wanamchukua kiongozi waliyempinga kuwa kiongozi wao mkuu.
 
Aliyemshauri Samia kutumia staili ile ya jana kuzima maandamano hamtakii mema, amemchafua na kumpa sura ya dikteta katili anayeamini kutatua matatizo kwa kutumia mabavu ya vyombo vya dola.
 
"Tulia RPC Muliro. Kwani shida iko wapi mpaka unikamate? Shida iko wapi? Watu wanatekwa, watu wanateswa. Watu wanaumizwa. Lazima watu wengine tuseme kuwatetea. Lazima tuseme. Lazima tusikike."--Freeman Mbowe, 23 Septemba 2024, Magomeni, Dar es Salam.

Tangu mwaka 2016 Chadema wanalalamikia watukanaji, watekaji, watesaji na wauaji holela wa wafuasi wao, hasa wale wanaoikosoa serikali, ambapo vijana wengi wafuasi wa Chadema wanalengwa na watu wasiojulikana.

Hivyo, hivi karibuni Chadema walifikia hatua ya kuitisha maandamano ya kupaza sauti dhidi ya utekaji, utesaji na uuaji holela ambao sio sehemu ya utamaduni wa Tanzania ya Nyerere unaoheshimu misingi ya utu, kama tunavyosoma katika Katiba ya nchi (1977).

Katika wito wao Chadema walivituhumu vyombo vya ulinzi na usalama kuhusika katika kuasisi na kutekeleza utamaduni wa kumwaga damu ya wapinzani, kwa kuwa wote waliotekwa, kuteswa na/au kuuwawa ni wale waliotamka ama kwa maneno au kwa vitendo kwamba "siitaki CCM na serikali yake."

Vyombo vya ulinzi na usalama vinasimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye anavaa kofia nne kwa mpigo: Ni Mkuu wa serikali, Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa CCM inayopingwa na wanaotekwa, kuteswa na kuuwawa.

Kulingana na intelijensia za kimataifa, sasa ni wazi kwamba, utamaduni huu mpya unaegemea zaidi katika utamaduni wa umwagaji damu kwa kutumia upanga/jambia uliozoeleka kwenye nchi za Kiarabu na Kiislamu huko Mashariki ya Kati, nchi zenye kusifika zaidfi kwa AUTOCRACY badala ya DEMOCRACY

Kwa wasiojua hili jambo someni Kitabu kilichoambatanishwa, yaani "Democracy in the Arab World: Explaining the deficit."

Kwa mujibu wa kitabu hiki, Waarabu-Waislamu wa Mashariki ya Kati, ambao kwa sasa ni washauri wakuu wa baadhi ya viongozi wetu wakuu, wanaamini yafuatayo kuhusu uhusiano uliopo kati ya demokrasia na autokrasia:
  • "a backward society cannot but produce a backward socialism and cannot but produce a backward democracy. Therefore, priority must begiven to the revolutionary transformation of that society." (p.21)
  • "Giving freedom to the people could lead to the tyranny of the majority, given the multiple pathologies of Arab civil society"(p.22)
Nchi hizi zinaamini katika matumizi ya jambia kama mbinu rasmi ya kueneza imani, sera na mikakati yao kwa kuwatisha, kuwateka, kuwatesa na kuwachinja wote wasiokubaliana na imani, sera na mikakati yao.

Kuna wakati hayati Magufuli alipingwa na umma kwa sababu hii. Bado ni kwa sababi zile zile Chadema wanaipinga serikali ya Rais Samia, lakini sasa kuna ukatili wa ziada umeongezeka chini ya Rais Samia.

Hivyo Chadema waliitisha maandamano kupaza sauti ya kupinga. Lakini vyombo vya dola vikaharakisha kujikusanya Dares Salaam na kukaziba barabara na mitaa yote ya Dar na hatimaye kufanikiwa kuyakwamisha maandamano.

Viongozi wakuu wa Chadema waliojitokeza barabarani wamekamatwa, wamepelekwa polisi, wamefunguliwa majalada, wamedhaminiwa na kuachiwa kwa dhamana.

Lakini bado tatizo liko pale pale maana waliotekwa bado kupatikana na watekaji hawajulikani.

Kwa hiyo, sasa maswali nane ya kimkakati yanazuka na yanapaswa kujadiliwa kwa kina na wajasiriadola wote makini:
  1. Katika mtazamo wa kihistoria sisi Watanzania ni kina nani, sio kina nani na kwa nini sisi ni tofauti na watu baki? (History: Where did we come from?)
  2. Kwa sasa tuko katika mazingira gani kama tukiangalia nguvu, udhaifu, fursa na vitisho dhidi yetu? (current situation analysis: where are we now in terms of strengths, weaknesses, opportunities and threats?)
  3. Tangu mwanzo sisi kama Taifa tulitaka kwenda kwenye bonde la utekaji, utesaji na uuaji au kwenye kilele cha mlima wa uhuru, uzima tele, udugu na ustawi endelevu? (Vision: Where do we want to go?)
  4. Tunawezaje kutoka hapa na kufika tunakotaka kwenda, kwa kuzingatia kuwa kuna aina tatu za mikakati ya kutatua matatizo, yaani: additive problem solving strategy, subtractive/eliminative/substitutive problem solving strategy, na problem resolving strategy? (strategic orientation: While using our strengths to overcome our weaknesses, defeat threats and seize opportunities, what exactly will we do in order to get where we want to go?)
  5. Ni mbinu gani zitatumika kutekeleza mkakati wetu wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali ? (tactics: How will we get our strategy implemented?)
  6. KIna nani wanapaswa kuhusika katika mkakati huu mpya wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali? (division of labour: Who will do what tasks?)
  7. Tunahitaji rasilimali kiasi gani kwa ajili ya kufanikisha mkakati wetu wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali? (budget: How much resources does our journey require?)
  8. Katika mkakati wetu wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali jukumu gani litatekelezwa wakati upi? (time table/work plan: How long will our journey take?)
  9. Tukifika mwisho wa safari yetu tutajuaje? (Key performance indicators: What are the signs of our destination?)
  10. Tukifika mwisho wa safari salama tuchukue tahadhari gani za kiusalama? (Security: What should be our security management strategies in our bid to sustainably defend of success story?)
Tujadili bila jaziba.

Solution= Samia must go
 
bado hatuna kizazi kilicho tayari as a group kupigania haki.. tuna few individuals wenye huo ujasiri.'
chadema iangalie namna ya kujilinda na kuwalinda viongozi wake pamoja na mpango mpya wa kupambana na ccm ila sio kupitia mobilization ya watu, kwa sasa uwoga, umaskini na kukata tamaa vimewatawala wanachi hvyo kupata mafuriko kama ya zama za kina dr slaa na lowassa ni ngumu.
watu warud chimbo wachore raman upya na waliandae taifa kwa hzo movement posibly kuleta mabadiliko chaguzi za 2030 kuendelea. ila 2025 bado hakuna uwezo wa kubadilisha kitu, given condition ya watawala na ya watawaliwa kwa sasa, angalia misimamo ya bunge, ya mahakama zetu, ya jeshi la polisi, na unyonge wa wanachi, uliochochewa na woga, umaskini, pamoja na unafki/uchawa wa kutisha.​
KUHUSU KIZAZI, HAKI na UJASIRI

Kuna namna ya kuziona jamii ni kuzibayanisha ukweli wa sifa, hadhi na ukweli wake, kiutamaduni; namna yenye kina sahihi cha mbegu ya u-JUA-ji.

Demokrasi kwa mfano, ni topografu ya juu juu tu katika kukadirisha kheri ya mapana ya jamii; vivyo hivyo kuzungumza mambo ya tawala, Ujamhuri na siha njema raia/wanajamii--mapelekeo na vina vya tafsiri kuhusiana na HAKI na WAJIBU wa Ki-Ujamhuri.

Uanazuoni wa kileo, 2024, hujikita sana kwenye visomo empirikali vya 'mahusiano ya nguvu' miongoni mwa wanajamii; hili jambo lina umahiri wake--umahiri kimashauri na upeo wa namna fulani ilivyo ni Elimu 1.0; na huku vile vile, kumbe, kukosa 'vina vya tafsiri' vyenye kujinasibu na ukweli wa 'UTU'--UTU na Metafizikia yake.

Japo ni rahisi kwa Wanazuoni kutetea mashauri ya ujuujuu wa wazi wa mambo, wenye kuzungumza hili kwa lugha ya Kiingereza kutaja 'Objectivity', hawa wataepa mengine ya undani wa mambo kwa kudai ni mambo ya kutegemea mtu na mtu, 'Subjectivity', kwa wenye kuzungumza hili hili kwa lugha ya kiingereza...

SASA, mambo ya kuepea misimamo ya UTU na Imani ndiyo 'Pepo ya Wadhalimu' na 'Makafiri'; Ukafiri kiufundi ile nasibu ya UTU usiyo na 'kina cha upeo na mashauri' kupitiliza 'kawaida ya mambo; na basi kawaida ya mambo ni mapana ya jamii ambayo kuna mseto wa 'watu wenye kujua ilivyobora' ama 'watu kutokujua ilivyobora'--pia watu wa kutokujua kabisa/ujinga.

'Pepo ya Wadhalimu' na 'Ukafiri' , ashkum si matusi, ni nasibu ya utu wa ubinafsi, kiburi na kujikweza kijamii kwa kutumia fursa ya 'kawaida ya mambo'. Kwa mintarafu ya hivi, 'kawaida ya mambo' ndiyo mambo ya 'Statusi Kwou'; epitomi ya ule usemi 'Sandakalawe... Mwenyekupata... Mwenyekukosa....' Basi ndiyo yawa, adha zote za tafsiri ya haki, dhuluma vivyo hivyo dhana za 'Uhuru' ama/na 'Amani', vyakadirisha ukweli wa kuwa kwamba huo wote ni utundu wa 'kuwapanga wanajamii' ili wakubaliane ni 'hali ilivyo'/Statusi Kwou...

SASA, siasa ni 'sayansi' ya juu juu ya mambo, inayoweza kutumiwa hata kudanganyia wanajamii/umma kuhusu 'Demokrasi'; na kumbe haya yote ni jamvi la nasibu ya 'Michezo michafu'. Kwa mintarafu ya hili, ni 'Nuru ya Ufahamu' pekee ndiyo ufunguo wa 'Kuwasanua wanajamii' na michezo yao--michezo yao iliyo ndiyo 'Mauti yao'. Kwa nchi yetu ya Tanzania kwa mfano, kuunganisha dhana ya 'Demokrasi' na dhana ya 'Ujamaa' ina ukweli wake wenye kina na kheri; japo hata wasomi na wanazuoni wanaweza kudhania haya ni 'mambo ya siasa' na 'Milengo'--milengo ya kinchi-dola iliyoshindwa ama 'ya kimaskini'; na tena jinamizi baya sana katika harakati zilizopitiwa, kihistoria, katika kulijenga taifa kwa utaasisi wa Nchi-dola ya Kijamaa...

Kwa ELIMU 1.0, na tena kwa udhanifu adilifu, inaweza kufikiriwa nchi inaweza kuongozwa na watu wa maarifa; wawe ni kwa sura rasmi ama isiyorasmi ya kiutendaji. Kwa mintarafu ya hivi, wale watu wanaoweza kuwa katika kujua--kujua mengi hata yasiyojulikana kwa umma/jamii; wanaweza kuongoza serikali ya watu kwa manufaa yao na ya umma huku wakiendelekeza 'utawala wa watu wachache' wenye 'kupangwa/kupangiliwa' kwa 'maslahi ya nchi'. Basi ndiyo yawa, kuna nchi nyingi hili limejaribiwa 'kisiasa za dini' ama hata 'kisiasa za kisayansi jamii' bila mafanikio ya kweli. Tena basi kumbe, Nchi yeyote inaweza kuwa jamvi la 'Michezo'--mchezo kwa wale wenye mbinu, ujuzi na uwezo wa 'kutawala mambo'.

Autokrasia ndiyo 'jina la mchezo' --jina la ule mchezo khasa wa watu wa mbinu za kutawala; ambavyo hata Demokrasi inaweza kuwa 'mchezo' kwa wale wenye ujuzi wa 'siasa za kisayansi-jamii'; Udhamirifu wa 'Demokrasi na Ujamaa' ni 'kupiga pini' nasibu ya hayo yote mawili. Kwa mintarafu ya hivi, dhana ya 'Demokrasi na Ujamaa' ina misingi ya kiroho, maadili na miiko--iwe inajulikana wazi wazi ama imesitirika. Basi ndiyo yawa, kwa mfano, Uhuru-Udugu-Haki-Amani ni mbegu ya u-JUA-ji ya kusudi la kiroho la Jamii Mabadilikoni katika kulijenga taifa la watu wanaojipambanua dhahiri na ulimwengu wa hila ama/na 'ukafiri'.

Maslahi ya Taifa lenye misingi ya Demokrasi na Ujamaa ni mwongozo wa kusisitiza koherensia ya vyombo vyote vya Ustawi wa Jamii ili kukadirisha sura ya miundo na utendaji inayokusudia wanajamii wote wanastahiki tunu za Uhuru, Udugu, Haki na Amani. Kwa mintarafu ya hivi, daima lipo hitaji la kuwakumbusha wadau na watendaji wote miongozo ya Utaasisi wa Kitaifa kwa ajili ya Shabaha ya Maendeleo ya Watu na tena kutafuta muafaka wa uadilifu wa kiutendaji wa shabaha yenyewe. Basi ndiyo yawa, hakuna mwanajamii anayelazimishwa 'kuwa na imani' na Utaifa wake bali 'mazingira rafiki' yanahitajika daima ili kuwawezesha wanajamii 'wajitambue' na 'kunata na biti' ya Uzalendo...

Mazingira rafiki ni fanusi ya 'Usanii' na 'Uongozi/Utendaji wa Kijamii' kwa kuwa 'viongozi/maafisa watendaji ni wasanii'--hawa daima wanaakisi ubora wa jamii yenyewe kiufahamu na kujitambua. Kwa mintarafu ya hivi, mambo kama vile 'Kujitambua' ama/na 'Kutimiza wajibu' ni suala mtambuka kwa taasisi zote za utendaji wa jamii. Basi ndiyo yawa, watu wenye madaraka katika jamii na hata pia raia wote wanaowajibu wa kukumbushana kheri za makusudi mema ya utendaji wa kijamii kwa ajili ya fanaka na furaha ya Taifa; chochote kile kinachofanyika 'Taasisi' katika Utaasisi wa Taifa hakina budi kujinyooshea vema sana na 'Nia ya Kulijenga' pia 'Maslahi ya Taifa'. Tena basi, kupangalanyika kwa jamii huja kutokana na wanajamii wote kupotezana kuhusu 'Maslahi ya Taifa'; kukosa kujiimarisha kitaasisi vile vile 'Kujisahihisha kitaasisi'...

Kiufundi, ikiwa wanajamii wa Kitanzania wataendekeza sana 'Politiki' basi wajue ndiyo wanaicheza 'ngoma ya Ukae'... Mifumo ya Kisiasa, ina mapungufu ikiwa UTU wa wanadamu ni 'Kafiri'. Kwa mintarafu ya hivi, mageuzi na mapinduzi ya kijamii yaliyo ya kweli, na tena ya kutarajiwa, yawa ni 'Kufukuzia Upepo' wa mabatili ya KIUTU. Siasa zote ni danganya toto kula kande mbichi kwa kuwa, daima kwenye ulimwengu wa mwenyekupata na mwenyekukosa, mvuta kamba/muwamba ngoma huvutia kwake. Basi ndiyo yawa, Jamii ya Watanzania kwa mfano, wanahitaji sana namna ya Elimu inayowakomboa Kifkra na KIUTU; na si 'Elimu ya Madarasani' tu. Tena basi Ujasiri upo kwenye kujikomboa kifikra; na si kuaatamishwa kama yai/kifaranga cha Kuku katika 'kambi za fikra za kisiasa' na malengo yenye 'Ukafiri'...

Kiufundi, ikiwa wanajamii wa Kitanzania waterejea kwenye misingi ya Nia na Makusudi ya Taifa basi wanaweza 'KUJISAHIHISHA KITAASISI na MIFUMO'. Kwa mintarafu ya hivi, 'Mwenge wa Uhuru' ni alama ya muamko na ujenzi wa Taifa kwa Mwangaza wa UTU bora. Basi ndiyo yawa, Umoja ni jambo litokanalo na nasibu ya kushiriki kusudi la utaifa na Maendeleo ya UTU--si maendeleo ya vitu; ama maslahi binafsi ya mtu ama kikundi cha watu. Tena basi, Ujamaa ni nasibu ya kushiriki 'Matamanio ya UTU bora' na matunda yake ya Ustawi na Maendeleo.

Kiufundi, ikiwa wanajamii wa Kitanzania watajitambua na kujiongeza kwa kheri kupitia Utaasisi wa 'Mwenge wa Uhuru' kutakuwepo koherensia na sinejia ya miundo na utekelezaji wa mipango kitaasisi na Mifumo. Kwa mintarafu ya hivi, maslahi ya kweli ya Taifa ni jambo linalotakiwa kuzingatiwa na kutetewa na wanajamii wote wenye kujua ilivyobora--si suala la kudhani maendeleo yanaletwa na 'chama' ama 'serikali'. Basi ndiyo yawa, mfumo wa vyama vingi una dosari ya kiufundi inayoweza kupelekea 'taifa changa' kupangalakanyika badala ya kujifuma kiutu Bora. Tena basi, tunu za Uhuru-Udugu-Haki-Amani ni nasibu ya 'Taifa la Kijamaa'; na si taifa la 'Samaki Mkubwa kummeza mdogo'...

Mbali kupita adha ya Ukafiri wa mfumo wa Vyama vingi na 'Miluzi Mingi'; ni kulitekeleza kusudi la azimio la udugu/ujamaa la sisi wanajamii wa Kitanzania. Hili linatekelezeka kwa kufanya bidii katika mawanda ya upeo wa Elimu 2.0 na Elimu 3.0; ili kuondokana na dhana ya sisi kuwa ni 'Wasafiri Kafiri'. Kwa mintarafu ya hili, kujua ilivyobora kuna kuja na uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja na tena kwa kutubidi sana kulikamia hili. Basi yawa, 'kujisahau' kwetu ndiko kunakotuponza 'kuingia majaribuni'. Tena basi hakuna mtu wa kumkomboa mwingine khasa, wala hakuna kikundi fulani cha watu watakaoamua hatma ya wengine ambao 'wamejiziuka'...

Demokrasi ni masikilizano katika utaasisi bora; bila 'UTU BORA' ni mchezo wa kutwanga maji kwenye kinu hadi 'Yesu atapokarudi'. Labda wapo watu wanayoyafahamu haya fika! lakini wanafurahia sana kuona jumuiya ya kimataifa ikijifurahisha na 'dhana hii ama ile ya demokrasi na utaasisi wake' bila mafanikio yoyote ya kudumu; kwa kuwa, Je ni nani wale kofia ni yenye kuwatosha? Waache wao waivae...

Kwa sisi watanzania, kukumbuka na kuzingatia azma ya ujenzi taifa la watu wa Demokrasi na Ujamaa ni kudumu katika nidhamu, adabu na mazoea ya 'utu bora' wenye kuazimia Uhuru-Udugu-Haki na Amani -- wenyekujua ilivyobora waache lawama, visa na vipakazio, kwa kuwa hivi vinaweza kuwa 'Mtego wa Shetani/Ukafiri'. Kwa mintarafu ya hivi, hakuna wa kutukomboa ikiwa tunaendelea kufanya fyongo kwa mawazo, vitendo na kutotimiza wajibu... Basi ndiyo yawa, kila mtu atimize wajibu wake katika makusudi yenye kheri na mengine yatajisawazisha yenyewe...


View: https://www.youtube.com/watch?v=X3lT1CivkLo



 
Mkuu 1961 Nyerere alipokuwa anahamasisha vijana 1954 tulikuwa na elimu? Elimu ni nini? Kwa kiasili binadamu ana elimu ya kutosha, anajua nini ni kitu kizuri nini ni kibaya. Anajua nini ni kuhimu kwa Taifa lake au siyo?
Mfumo wa elimu wa sasa ni wa kibinafsi na kujilimbikizia mali! Mfumo wa mwanzo baada ya kupata uhuru ulikuwa wa kuwajali binadamu wenzako kwanza na uzalendo kwa Taifa.

Hivi sasa hata maprofesa wanataka kujilimbikizia mali kwa hiyo hawajielekezi kwenye taaluma bali wengi wanajielekeza kwenye uchawa! Wanasaka uteuzi ili wanufaike na ufisadi uliotamalaki katika serikali.

Vile vile wanafunzi hawataki elimu ili wakawatumikie wananchi bali kupata michongo ya fedha chafu!

Kwa hiyo itachukuwa muda mrefu kurudi katika mstari ambao maprofesa na wanafunzi watajielejeza katika taaluma na tafiti zitakazokuwa zinatatua au kujibu changamoto zinazowakabili wananchi na Taifa kwa jumla!
 
Mfumo wa elimu wa sasa ni wa kibinafsi na kujilimbikizia mali! Mfumo wa mwanzo baada ya kupata uhuru ulikuwa wa kuwajali binadamu wenzako kwanza na uzalendo kwa Taifa.

Hivi sasa hata maprofesa wanataka kujilimbikizia mali kwa hiyo hawajielekezi kwenye taaluma bali wengi wanajielekeza kwenye uchawa! Wanasaka uteuzi ili wanufaike na ufisadi uliotamalaki katika serikali.

Vile vile wanafunzi hawataki elimu ili wakawatumikie wananchi bali kupata michongo ya fedha chafu!

Kwa hiyo itachukuwa muda mrefu kurudi katika mstari ambao maprofesa na wanafunzi watajielejeza katika taaluma na tafiti zitakazokuwa zinatatua au kujibu changamoto zinazowakabili wananchi na Taifa kwa jumla!

Sidhani kama tutarudi kwenye wakati wananchi wanajali maslahi ya jamii, taifa kuliko maslahi binafsi. Kuwarudisha Watanzania huko unahitaji mkono wa chuma.
 
Sidhani kama tutarudi kwenye wakati wananchi wanajali maslahi ya jamii, taifa kuliko maslahi binafsi. Kuwarudisha Watanzania huko unahitaji mkono wa chuma.
Sioni ugumu wo wote kurudisha uzalendo kwa vijana wetu wajao kwa kuwa tumefika hapa kutokana na aina ya utawala tulionao hivi sasa usio heshimu Katiba wala sheria zilizopo kwa maslahi yao.
 
Kwamba tupo mfumo wa utawala wa kidikteta wa kiarabu alioasisi Mohamad wa mapanga na majambia🤔

Solution hapa ni

1. Kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi itokanayo na Rasimu ya kwanza aliyoiasisi Mzee Warioba na ipatikane kabla ya Uchaguzi wowote.

2. CCM ije na mgombea mpya 2025 wa kuliponya Taifa.

3. Msajili aruhusu chama kingine kubwa kusajiliwa Ili tuwe na vyama vikuu vya upinzani VITATU.

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom