ecolizer baba
Member
- Sep 29, 2010
- 88
- 310
Kwanza nianze kwa kuwasalimu.
Pili naomba hiki kilio kiwafikie mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano na waziri wa Fedha na Mpango. Ni kuhusu sisi Wafanyakazi wa YONO AUCTION MART na TARUA hapa Mbeya.
YONO AUCTION MART umeingia kama mkusanyaji wa mapito ya PARKING hapa jijini Mbeya toka December 2018. Na tuliandika barua kuomba ajira na tukafanikiwa kupata wachache takribani watu 40.
Tumefanya hii kazi kwa uaminifu mkubwa. Lakini huu ni mwezi wa tatu sasa waajiri wetu kwa maana ya YONO na TARURA wamegoma kutulipa stahiki zetu. Yaani toka hiyo December hadi January na sasa ni February hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyelipwa.
Tumefuatilia hadi tumechoka maana kila siku majini yanabadilika. Kutokana na hali hii baadhi ya wenzetu wamekata tamaa. Kiufupi ni kwamba TUMEDHULUMIWA.
Naombeni wahusika waingilie kati ili kutusaidia tulipwe hela zetu kwani baadhi yetu tuna familia lakini nahitaji yetu kama mwajiriwa mmoja mmoja. Yaani tunakosa hata hela ya kula na nauli ya kwenda kazini.
Naomba kuwasilisha.