Tarehe 21-05-1996 Hakika ni Safari isiyosahaulika, Wapumzike Kwa Amani wote Walipoteza Maisha.

Makala yako inajikanganya kuhusu idadi ya waliokuwa kwenye meli na waliokufa. Mwanzo umetaja waliookolewa 114. Waliokufa na maiti kupatikana 319 wasiopatikana 332. Lakini tena ukasema waliokufa ni zaidi ya elfu. Harmonize hizi data
Akili hizi za Kubisha Kila Kitu kama zilivyo ajali nyingine nyingi Tanzania has a za Majini haijajulikana hadi Leo idadi ya waliokua Ndani ya Meli ila Inasemekana ni zaidi ya 1,000.
IMG_20170521_090623_331.jpg
 
MUNGU ampunzishe kwa amani Dada yake na Said Masoud mwanachuo mwenzetu miaka ya 90 Mwanafunzi aliyetoka kufanya mtihani wa kidato cha sita Rugambwa secondary.
ALLAH.. S. W. T... Awarehemu wote... Na mimi pia dada yangu..Zaina musa... Alifariki kwenye Ajali hiyo akitokea shule ya Rugambwa sec. School... Kumaliza mtihani wa kidato cha sita... Inna lilah wainna Ilah Rajiuun....
 
Iparamasa

Hawa jamaa wa Sumatra kusema kweli upande wa usafiri wa majini naona wamelala sana yaani mpaka litokee janga lingine tena ndio wajifanye wanafatilia

Mwezi mmoja uliopita nilienda Zanzibar ila huwezi amini upatikanaji wa tiketi hapa dar ni wa ulanguzi wa hali ya juu na hii mamlaka inajua maana malalamiko ni mengi lakini sijaona wamechukua hatua gani
huu ni mfano mdogo tu wa uwajibikaji kwa mamlaka ikiwa suala la tiketi ni gumu kwao kulifatilia. je kuchunguza hivyo vyombo kama ni salama kwa abiria wanaweza kweli??

Inasikitisha sana likitokea la kutokea ndio unawaona watu wanatoa matamko yasio na maana huku tunakuwa tumeshapoteza wapendwa wetu na nguvu kazi ya taifa


Wito wangu mamlaka ziwajibike ipasavyo waache kukaa maofisini
 
Wallah uko kama mimi,hata nikienda kigamboni tu lile pantoni naogopaje?
Sitaki mimi usafiri wa majini...imagine meli ipo katikati ya bahari huko,aaarrrgghh nitakufa mie kwa hofu.
Mie ujanja wangu wote kigambon naisikia kwenye radio na tv, panton umpandishe nani
 
KIUKWELI tarehe kama ya leo miaka 20 iliyopita haitoweza kusahaulika kirahisi kwenye mioyo ya Watanzania na Ulimwenguni kote, kwani usiku wa kuamkia Mei 21, 1996, meli ya MV Bukoba ikiwa na abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37 ilizama majini kwenye Ziwa Victoria mwambao wa Bwiru Jijini Mwanza ambapo ilikuwa takribani kilomita 30 kufika nchi kavu.

Meli ya Mv Bukoba ikiwa inazama.

Ripoti ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha hiyo ilieleza kuwa, kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma barabara ya Musoma, nje kidogo ya Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla ya miili 332 haikupatikana.

Kila mwaka, ifikapo Mei 21, viongozi wa dini, wa serikali na wananchi huongozana kwenda eneo la ajali kufanya kumbukumbu.



Mnara wa Kumbukumbu ya Kuzama kwa Meli ya MV Bukoba uliopo Makaburi ya martehemu waliotokana na ajali hiyo, Igoma – Mwanza.

Hakika Mei 21 Mwaka 1996 Taifa la Tanzania liligubikwa na Msiba Mkubwa ambapo kila mmoja kwa nanma yake aliguswa na Msiba huo ambao uliyagharimu Maisha ya Mamia ya Wapendwa Wetu, baada ya Meli ya MV.Bukoba Kuzama hatua chache kabla ya kutia Nanga Mkoani Mwanza ikitokea
Mkoani Kagera.

Meli ya Mv.Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 ilizama katika Maji ya Ziwa Victoria Mkoani Mwanza yapata umbali wa kilomita zipatazo 30 kutoka ufukweni mwa maji na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika Meli hiyo ambayo tangu kuundwa kwake hadi kuzama kwake ilikuwa na umri wa miaka 17. Jambo la butwaa hapa ni Idadi ya vifo na idadi ya abiria waliookolewa ukilinganisha na Uwezo uwezo wa Meli hiyo wa kubeba abiria 430).

Makaburi ya waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Bukoba yaliyopo, Igoma – Mwanza.

Pengine tumezoea kuita kwamba Mei 21 Watanzania tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzama kwa Meli hiyo ambayo iliigeuza taswira ya Mji wa Mwanza, kwani kwa waliokuwa Mwanza Mwaka huo walipigwa na Butwaa baada ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambao mara nyingi hutumika kwa
shughuli za Kimichezo, pale ulipogeuka na ghafla na kutapakaa Maiti za wapendwa wetu, ama hakika inauma sana.

Wakati leo tunakumbuka tukio hili ambalo limeacha simanzi mioyoni mwetu, hebu tujiulize kwa pamoja; Kama ilivyo imani ya watalaamu wa masuala ya usafiri kwamba Usafiri wa Majini ndio usafiri
salama kuliko aina nyingine ya usafiri, Je Kwa Tanzania imani hiyo ina mantiki yoyote kwamba vyombo vyetu vya usafiri wa majini ni salama?.



Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri (Picha zote na Maktaba).

Lakini wakati tunatafakari suala hilo, pia tukumbuke kujiuliza sisi wenyewe bila kusubiri kusukumwa na mtu hususani wale wenye mamlaka ya kuleta matokeo chanya katika kuboresha hali ya usafiri majini Ikiwemo Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA kwamba tulijifunza jambo lolote kutokana na ajali hiyo ya Mv.Bukoba?

Na Kama kuna jambo tulijifunza, je tumefanikiwa kulifanyia kazi ipasavyo jambo hilo? Je kuna hali yoyote ya uwajibikaji (kwa waliopewa dhana ya kusimamia sheria) katika kuzingatia sheria za usafiri na usafirishaji wa majini na nchi kavu? Je, tumekwisha jijengea hali ya kuchukua hatua za uokoaji pale tunapopatwa na majanga ya majini au nchi kavu?.

Lakini pia wapo waliohoji na bado wanaendelea kuhoji juu ya taarifa ama ripoti ya uchunguzi wa ajari hiyo ya Mv.Bukoba kama ulifanyiwa kazi ipasavyo? Lakini pia wakiwa bado wanaendelea kujiuliza ni ajari ngapi za vyombo vya majini zimetokea tangu kuzama kwa meli hiyo? Hapo nadhani nawe unazikumbuka ajali kadhaa ambazo tayari zimekwisha kutokea na kuyagharimu maisha ya Watanzania ikiwemo ile ya mv Spice Ireland iliyotokea Septemba 10 mwaka 2011 katika Mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja Zanzibar.

Lakini yote Tisa, Kumi ni stofahamu iliyoibuka juu ya Chanzo cha ajali hiyo mbaya kuwahi kutokea hapa nchini.Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Wakaguzi wa na Waangalizi kwa maana ya Mamlaka husika, Wapo waliosema ilikuwa ni Uzembe wa Nahodha na Timu yake na wapo waliosema chombo kilikuwa kibovu.

Wapo waliodai chombo hicho kilikuwa kimebeba Mizigo na abiria kuzidi uwezo wake na wapo waliodai kuwa abiria wenyewe walisababisha ajali hiyo kwani walilazimisha kupanda Melini ilihali chombo kilikuwa kimejaa huku mlolongo huo ukihitimishwa na wale waliohusisha ajali hiyo na Imani za Kishirikina.

Mimi nasema sina nia ya kuandika hayo yote kwa lengo la kumtafuta mchawi ila lengo langu ni kuyaweka wazi hayo yote ili kila mmoja kwa namna anavyohusika na anavyoweza kusaidia namna ya kufanya ili kuepukana na ajali kama hiyo ama kama ambavyo wengine husema tusiangalie tulipoanguka bali tuangalie tulipojikwaa.

Wapo wengi waliowapoteza ndugu, jamaa na marafiki zao na mmoja wao ambae alimpoteza mpendwa wake katika maisha yake ni Mwanamitindo maarufu hapa nchini ambae pia anafanya shughuli zake barani Ulaya Flavian Matata ambae yeye alimpoteza Mama yake mzazi pamoja na binamu yake.

Pamoja na watu wengine, Matata amekuwa na desturi ya kukumbuka tukio hilo kwa kufika Mkoani Mwanza katika eneo la Igoma walikohifadhiwa watu waliopeza maisha katika ajali hiyo ya Mv.Bukoba
ambapo pia maadhimisho ya kuwakumbuka hufanyiia kila mwaka, huku akibainisha kuwa ilimchukua miaka mingi hadi kuamini kuwa ni kweli hayuko na mama yake mzazi, kwa kusema kuwa ni miaka michache iliyopita ndiyo ameweza kuamini kama ni kweli hayuko na mama yake tena.

Hakika inauma sana.
Umesimulia vyema sana,hujachomekea leo mambo yako yale ya siasa uchwara.
Ni moja ya tukio nalolikumbuka na kunihuzunisha sana tangu nikiwa mtoto.
Mungu awape faraja wote waliopoteza wapendwa wao.
Mungu awapumzishe kwa amani wapendwa wetu,daima tunawakumbuka na kuwaombea.
 
1495350425189.jpg
Shughuli ndio imeanza baada Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mongela kama mgeni rasmi
 
jiji liyatengeneze haya makaburi yawe kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavya, tuige memorials za wenzetu, utafikiri hatujawahi kutoka kwenye mipaka ya Tz
 
"Usitumie cheo chako kama dhamana ya matakwa yako, usije sababisha ajali kama ya MV Bukoba.....
Poleni sana Watanzania,
Na wale wote walioangamia, Mola aziweke roho zao mahala pema peponi..."
(Justine Kalikawe, 1996).

Baada ya wimbo huu huyu jamaa sikumsikia tena hata wimbo wake ulipotea na sijaupata mpaka leo. Wapumzike kwa amani marehemu wote, Amina.
 
jiji liyatengeneze haya makaburi yawe kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavya, tuige memorials za wenzetu, utafikiri hatujawahi kutoka kwenye mipaka ya Tz


Tanzania Yenyewe Umetembea wapi Ndugu mbona Kuna Makaburi Mengi tuu yametengenezwa Vizuri.
 
Back
Top Bottom