Taratibu naona watanzania wanarejesha matumaini yao kwa CHADEMA

Si siri mlianza na Mungu lakini pale mmoja wenu alipodai ni lazima tuing'oe ccm hata kwa kumtumia shetani, Mungu aliwaacha. Sasa hivi mmepagawa na hamjui kilichowapata. Poleni.
Kama ni kweli tulichukua shetani kiuondoa Ccm jiulize yalibaki mashetani mangapi kwenu?
 
Huwezi chekelea nchi ikipelekwa kule Zimbabwe ya Mugabe iliko.
 
Msingi wa uwajibikaji au accountability ni kufuata sheria, kama rais hafuati sheria huwezi sema anawajibika

Well, nianze kwa kusema mimi ni mwanachama wa CHADEMA. Katika hili la kuwa Rais hafuati sharia, Yes nakubaliana nalo kwa baadhi ya mambo madogo madogo ambayo tumeya shuhudia hivi karibuni tangu Nov 2015. Na katika hili sioni ni kwa nini Rais hakufuata ama hakupewa ushauri na wataalam wake hata kwa mambo madogo madgo ambayo angefuata taratibu zilizopo ni rahisi tu kutekelezwa na angeweza kufikia malengo yake bila kuchelewa. Pamoja na hilo, nita mpongeza kwa yale mazuri anayo fanya kwa masirahi mapana ya mama yetu Tanzania, na nita mkosoa au sita muunga mkono kwa yale anayo yafumbia macho kisa ana uhusika hata kama si wa moja kwa moja. Dawa ya jipu ni kutumbuliwa, usipo fanya hivyo ugongwa utaendelea kuibuka tena na tena sehemu tofauti tofauti mwilini..... Mfano, Lug...umi na wahusika wake, upande wa pili kuna February ukigeuka nyuma kuna bunge live.

Ushauri wa jumla, wapambanaji wetu sijui watachukuliaje mawazo yangu .... Watanzania wanaweza wakapata shida kuelewa malengo hasa ya UKAWA kama tuna kinzana na yale anayo fanya JPM ila niliwahi kusikia kwamba tofauti inakuja katika staili anayotumia Rais kufikia malengo. Binafsi niliwahi kusema kuwa kwa hali tuliyo nayo tunahitaji Rais dikiteta japo kwa kiasi. Hata hivyo mimi siyo mwanasiasa na wala sijasomea sayansi ya siasa, yamkini kama wewe haupo katika serikali inayo tawala na wewe lengo lako ni kupata utawala, sijui ukimuunga mkono anaye tawala huwezi kuaminiwa na wananchi?? Hii ni mada inayo hitaji kudadavuliwa zaidi.

Pamoja na mawazo yangu hayo, kamwe sitabadilika kwa sababu najua ili JPM au CCM yake wawe bora na wafanye kazi nzuri kwa Watanzania LAZIMA kuwepo na Upinzani makini ili anayepata nafasi ya kuongoza ASIBWETEKE!
 
Awamu hii ya kiserikali inaniacha hoi kwa utendaji kazi wao wa kwenye media,hilo tu!
Kila wafanyacho waandishi wa habari wako pembeni!
Sasa kama wanapenda tuone kila kitu bunge linazuiwa kwanini?
 
Kosa kubwa ambalo CHADEMA walifanya ni kumchukua Lowassa na kumfanya mgombea Urais wa Tanzania.

Baadhi ya viongozi na wanachama walidhani baada ya Uchaguzi ataenda Monduli kuchunga ng'ombe lakini kwa sasa amesema anajiandaa kugombea tena kwenye Uchaguzi Mkuu 2020.

Kwa sasa hawana ubavu tena wa kumwambia akae pembeni wakati wanafahamu yuko kwenye njia aliyopitia Augustino Mrema.

Uwepo wa Lowassa ndani ya CHADEMA umewafunga kiitikadi na kifalsafa kiasi kwamba mpaka sasa huwezi kufahamu CHADEMA inasimama kwenye falsafa gani achilia mbali mwenye maamuzi ya mwisho ndani ya CHADEMA.

Kwenye hafla za kichama, Lowassa anaonekana ndiye top dog wakati kiuhalisia ni mwanachama ambaye hana cheo chochote ndani ya CHADEMA. Nilishangaa sana kuona Mbowe ndiye anampokea Lowassa badala ya Lowassa kumpokea Mbowe.
 
Toa mfano wa hao wakosoaji!
Mimi ni mmoja wa wakosoaji! Nilimpenda ila sasa hapana sidhani kama alijipanga kuwa hapo alipo! Nahisi alihitaji seminar! Na kwa style yake nakupa mwaka mmoja tu nchi itakuwa katika hali mbaya sana labda abadilike!
 
Kama ni kweli tulichukua shetani kiuondoa Ccm jiulize yalibaki mashetani mangapi kwenu?
Ha ha ha, jambia la JK lilipokata kile kichwa cha shetani, kilichocki kwetu hakina nguvu tena. Chama sasa kinogile na bado muda kidogo utasikia vigelegele vya m/kiti tingatinga. Atasafisha uchafu uliobaki.
 
Awamu hii ya kiserikali inaniacha hoi kwa utendaji kazi wao wa kwenye media,hilo tu!
Kila wafanyacho waandishi wa habari wako pembeni!
Sasa kama wanapenda tuone kila kitu bunge linazuiwa kwanini?
Ni Kama wanajaribisha kuongoza nchi hawako siliasi.
 
Ukawa ndio watu wenye maoni ya ukweli na ndio maana wamefikia hapo ambapo leo tunwaona na saizi isingekuwa ubabe wa ccm basi saizi lowassa angekuwa ikulu. Mm Sijajua wewe unaongelea maoni gani?
Mpo katika boti moja mkuu,hujamuelewa tu jamaa.
Jaribu kufikiri mara 2.
 
Kuongoza nchi inahitaj akili kubwa sana na c ubabe...mugabe na ubabe wke wte wa kuwafukuza wazungu yuko wap....utumbuaji utumie akl
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom