Tapeli anatafutwa, zawadi nono mpaka million 10 kutolewa

WAKUU HIZI NI DETAILS ZA ISSUE NZIMA,
angu
1. kwanza kabisa issue ya jina la JANJA PORI isiwasumbue kwakuwa ni mtu ameomba tu ID yangu kutumia kupost habari yake, lakini ni mtu wa karibu yangu kapigwa, ila mimi hadi kupewa jina hilo mjue kabisa niko makini na ni Janja wa TOWN
2. Huyu aliyetapeliwa alikuwa anataka fanya biashara ya madini kununua kwa madalai na kusafirisha nje, sasa rafiki yake alikuwa ni huyo Felix.
2. Huyo Felix walisema wana kampuni Mbezi na mpigwaji alienda kabisa ofisini akaona GOLD na akaona ofisi imesetiwa vizuri (nadhani these guys they are very trained) badae akalipia kilo moja na nusu kama test.
3. Akafunga mzigo wake vizuri na akalipia kilo na nusu, sasa huyo dogo akasema wao kama kampuni watafanya process zote za document, huwezi amini tuna evidance ya document zote TRA, WIZARANI, etc( nadhani huu mchezo watu wa huko wanahusika sana sana maana documents zote ni kama za kweli na mihuri ya kweli) .
4. Huyu feleix alitumia kampuni ya usafirishaji inaitwa Umoja logistic express, nao wakaenda Swiss Cargo (japo mpaka sasa Swiss Cargo wanasema waybill iliyotumika ni fake, na TRA tin number zilizotumika ni fake japo zina mihuri ya serikali)
5. baada ya kuambiwa mzigo uko njiani dogo alirequest mteja wake yani Mpigwaji alipie additonal 3.5 kilo ili ziwe tano, wakiwa na lengo na kupata certificate flani.
6. Huyu dogo ana mtandao mkubwa, wengne sitapenda kuwataja mpaka mbeleni upelelezi ukikamilika
Naombeni wana JF muwe makini na makampuni fake mjini hapa.
Ntaleta details zaidi badae kwa lengo la kusaidia watanzania wenzangu msipigwe ka alivopigwa mpigwaji

Mkubwa,
Funguka, maana sasa maelezo yanazidi kujichanganya. kuwa wazi kama gazeti la Jamhuri ili na JamiiForums heshima yake iendelee.
 
Unachosema ni ukweli mkuu hawa vijana wa town wala bata ni matapeli wengi wao na sasa vinawageuka" ndio hao wananakufa kwenye maajali wakiwa na magari yao yaliyotokana ma mali za utapeli. Huyo Chief FEMO aliyemtapeli jamaa pia dogo aliyevuta Juzi kati Kaloosh Jimmy aliyevuta last year kina Hydary na wengne weng ni clique moja.
Huyu tapeli mbna kma ameshapatikana yani jamaa akitembeza hela kidogo kwa wajanja wa kino n sinza anampata kirahisi.....na dawa yke sio kumpeleka police ni kibano cha kimyakimya ataje wote waliokula hiyo pesa then wakamatwe
 
Kweli kabisa, mji huu wezi wanajulikana,wapigaji wa viwanja,nyumba wanajulikana,wapigaji wa madini wanajulikana
cku hizi utapeli umehamia kwa wauza sura mjini....huyo jamaa walimuwahi mana huo mchezo ni wa kizamani sana
 
Unaweza kunithibitishia vipi hio 10m nikikusaidia kumpata? Huyo anafanya michezo ya watu.......michezo hio wenyewe wanawapiga foreigners baadae wanawatumia polisi wanawa haraass kuingia nchini as visitors lakini wanafanyabiashara haramu ya madini,as a result foreigner anakimbia nchi watu wanagawana hela....sasa huyu dogo anampiga mzalendo mwenzie?

Si ndio hapo nimemshangaa sanaa huyu dogo na akidakwa lazima wana wampige pipe.
 
Hapa mie naona vimebakia vitu viwili,badala ya kumsaidia.
-Hatimae watu waanza kupeana number za wachawi na washirikina,wengine wanachangia kumbe wanatafuta linki za wachawi
-Hapa mleta uzi kuna mtego ataingizwa tu wa kupigwa tena pesa.

Miaka ya nyuma watu kutoga mkoani ndio walionekana kupigwa saana kwenye utapeli,ila sasa ni wajanja saaana.Na imegeuka kuwa wa mjini ndio wanalizwa kizembe saaana.

Ukweli utapeli huu umefanyika kizembe mno,hayam ambo ya kutaka njia za mkato ndio hupelekea hali kuwa namna hii.
Halafu mleta uzi analeta kiujanja ujanjaaaa,ikimaanisha kwamba kuna sehem aliingia kizembe zaidi,na ninaamini alikuwa anajua kabisaa kwamba kuna part ana play illegal,sasa huu wepesi na watu ndio wakapitia hapo hapo.
Ku trace Kampuni ni rahisi mno,withing 30 minutes unajua kila kitu.Halafu huu wizi mbona wa zamani saaaana
Yaani unaenda kufuatilia kampuni wakati umeishatapeliwa?

Halafu baada ya kutapeliwa ndio unakuja JF?
Wakati huo ungeingia humu JF na kuuliza kampuni bora kwa biashara hiyo au kuulizia kampuni hiyo basi wala usingefikia kutoa hela in 15 minutes watu wangekupa data zooote.Humu kiboko.

Ila kama ukiisaliti JF basi ujue utakuwa asusa wa wapigaji mjini.
Na inawezekana kuna usanii kuanzia hatua za mwanzo kabisaa za upatikanaji wa hiyo dhahabu.
Nakushauri,usitumie muda mwingi saana kufuatilia huyo mtu,maana itakutoka pesa kibaooo,na unawezakukuta watu na marafiki zako wakakugeuza tena mradi kwa lengo la kumsaka jamaa.Hilo inatakiwa liwe somo tosha kwako.RB ya polisi inatosha,ila kumtafuta kwa pesa hiyo ni ngum saana.La sivyo ulishie pesa kibaooo,na hapo unabahatisha
 
Unaweza kunithibitishia vipi hio 10m nikikusaidia kumpata? Huyo anafanya michezo ya watu.......michezo hio wenyewe wanawapiga foreigners baadae wanawatumia polisi wanawa haraass kuingia nchini as visitors lakini wanafanyabiashara haramu ya madini,as a result foreigner anakimbia nchi watu wanagawana hela....sasa huyu dogo anampiga mzalendo mwenzie?
Mkuu uhakika upo, and that is real. nipigie kwa number hiyo we met tuongee
 
Mkuu Milioni 10 wala hao Private investigator huhitaji unachokihitaji kwa huyu jamaa ni sajili namba mpya ya simu weka picha ya kimada mkali sana.Tafuta rafiki wa kike halafu aonge na huyu tapeli ajifanye kamzimia kwa sana. Akitokea kumuulizia kapata wapi namba yake amwabie alimuona club flani akampa namba mwenyewe mwezi jana.Waachie waongee kama siku mbili tatu halafu mwambie apange wakutane sehemu ya faraha hapo ndio kuwa na polisi kwenye gari ya tint akitokeza tu unamkamata. Ukimkamataa kwa mtego huu nataka hela yangu ya bia tu;):D
mkuu huu ushauri ni mzuri ila ingefaa zaidi kama ungem-PM
just imagine Mimi ndo muhusika sina escape kimtindo
 
Huyu 'jamaa/tapeli wako' atakachofanya atatafuta mtu ajifanye amemkamata halafu wewe utampa huyo mtu 10m kwa kukukamatia 'jamaa' halafu 'jamaa' atakutaka radhi na kukurudishia 68.7m yako. Mwisho wa siku unaona isiwe issue maana pesa kashakurudishia so unamwachia 'jamaa' na anaenda kugawana ile 10m na mtu wake.Unakuwa umelwa tena hiyo 10m.

Pole sana bro lakini kuwa makini na yeyote atakayesema amempata 'jamaa'
Mkuu upo sayari ya ngapi aisee yaani jamaa arudishe mtonyo wa M68 kwa mtego wa 10M???
Ni bora ungemtahadharisha kutapeliwa tena hiyo 10M asipozidisha umakini.
Binafsi naahidi kumsaidia jamaa endapo huyu tapeli atakuwa "anakula bata" hapa mji kasoro bahari!
Kingine mhimu kabisa jamaa aongeze agents kwenye miji mhimu kama MWANZA, DOM, MSA CHUGA na kwingineko mbona hatachomoka!
 
Mkuu upo sayari ya ngapi aisee yaani jamaa arudishe mtonyo wa M68 kwa mtego wa 10M???
Ni bora ungemtahadharisha kutapeliwa tena hiyo 10M asipozidisha umakini.
Binafsi naahidi kumsaidia jamaa endapo huyu tapeli atakuwa "anakula bata" hapa mji kasoro bahari!
Kingine mhimu kabisa jamaa aongeze agents kwenye miji mhimu kama MWANZA, DOM, MSA CHUGA na kwingineko mbona hatachomoka!
Na wewe unaihitaji hiyo 10m kumbe!
Nilikuwa nampa tahadhari tu.
Ila angetaka with 10m mapolisi wanaweza kuhakikisha wanampata.Polisi wana resources nyingi mno wanachohitaji ni pesa tu.
 
Na wewe unaihitaji hiyo 10m kumbe!
Nilikuwa nampa tahadhari tu.
Ila angetaka with 10m mapolisi wanaweza kuhakikisha wanampata.Polisi wana resources nyingi mno wanachohitaji ni pesa tu.
Mkuu rudia kusoma nilichoandika.
Kibongo bongo hata hao polisi ni wakuangaliwa kwa jicho la tatu! Ukiwafinance watamtafta jamaa wakimpata wanaweza gawana mpunga wote alobakiwa nao nakuendelea kukupiga danadana za "uchunguzi bado unaendelea" refer KASUSULA scandal polisi kibao walivuna mkwanja ule b4 hajatiwa nguvuni.
 
Mkuu rudia kusoma nilichoandika.
Kibongo bongo hata hao polisi ni wakuangaliwa kwa jicho la tatu! Ukiwafinance watamtafta jamaa wakimpata wanaweza gawana mpunga wote alobakiwa nao nakuendelea kukupiga danadana za "uchunguzi bado unaendelea" refer KASUSULA scandal polisi kibao walivuna mkwanja ule b4 hajatiwa nguvuni.
Aisee umenikumbusha. Wezi walinikomba siku moja hapa kwangu, kwenda polisi wakanichangamkia mno wakawapigia informers wao.Wakaniambia nisiwe na wasiwasi vitapatikana. Sikuwahi kuwasikia tena aisee. Nikaamua kupotezea tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom