TANZIA: Muigizaji Seth Bosco (Mdogo wa Marehemu Kanumba) amefariki dunia Usiku wa kuamkia leo

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mdogo wa Marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwa Mama Kanumba Kimara, Dar es Salaam alipokuwa akiuguzwa kwa muda sasa baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye uti wa mgongo.

Abela ambaye ni Dada wa Marehemu amethibitisha.

#RIPNduguYetu🙏🏽

FB_IMG_1575690742214.jpg
.
Taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Alipougua ghafla: Mdogo wake Kanumba apooza ghafla
 
Huyu mama wa hawa marehem atakuwa katika hali mbaya. Jaribu kuwaza vijana wako ambao unategemea sasa ule matunda na wakutunze wanafariki nakukuacha, waweza kukufuru.

Lakini tukumbuke kuwa Sote ni wa Mungu tutarejea kwake na kila nafsi itaonja umauti ..Mungu ampe faraja Mama wa marehemu
 
Apumzike kwa amani, pole sana mama Kanumba, najua unapitia wakati mgumu sana kwa sasa ila hayo ndio mapenzi ya Mungu.
 
Hutaelewa kitu mpaka upoteze mtu wako wa karibu. Huyu mama imemkuta hivyo mara mbili.

Yaani sina cha kusema

Wale tunaotaka kufeed na kujiongezea umaarufu kupitia misiba na majanga ya wengine tuvute pumzi tutulie tuache lipite.
 
Watu wengi wanajua huyu Seth ni mtoto wa mama Kanumba, Marehemu ni binamu na Kanumba

Back
Top Bottom