TANZIA: Bi. Asha B. Makame afariki dunia

DSC_5379.JPG

Aliyejitangazia kuwa ni Raisi halali akimsindikiza Bi. "Nchi haitolewi kwa vikaratasi". Mungu amrehemu huko aliko. Mungu ni mwingi wa rehema. Msindikizaji ana cha kutafakari. Kesho au kesho kutwa ni zamu yake.
DSC_5385.JPG

Raisi aliyechaguliwa na wapiga kura wengi na kukwamishwa na CCM na Jecha anamsindikiza ndugu yake na kumtakia safari njema. Huu ni ubinadamu na utu uliotukuka anaouonesha Maalim Seif.
DSC_5388.JPG

Dereva wa mkwamo akijionea mwenyewe hali inayomsubiri kwa kuwasweka Masheikh Korokoroni kwa matamanio ya ulwa.
DSC_5344.JPG


Nimejaribu kuangaza kwenye hizi picha sijamwona Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha. Kwa nini anaitisha "uchaguzi" na nchi haitolewi kwa vikaratasi?

Link ZanziNews : Mazishi ya Marehemu Asha Bakari Makame katika Kijiji cha Kianga Zanzibar
 
Unamkumbuka yule mama wa Zanzibar aliyesema Serikali ya Zanzibar haiwezi kupewa watu waiongoze kwa vikaratasi wakati wa BMK?
Huyo ni bingwa wa mipasho bungeni alikuwa anaitwa Asha Bakari, kwa mujibu wa ITV amefariki dunia huko Dubai.
Apumzishwe kwa amani
sio apumzike kwa amani mi naona ni motoni tu amna namna
 
View attachment 318027

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Zanzibar, Asha Bakari Makame amefariki dunia leo huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa zilizothibitishwa na wanafamilia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo visiwani Zanzibar, Salama Aboud Talib zinasema kiongozi huyo alikuwa ametoka nchini India kwa matibabu.

Naibu Katibu huyo amesema kuwa baada ya Makame kutoka India kwa matibabu, alipitia Dubai kwa mwanae, mahali ambapo mauti ilimkuta mapema leo.

Mbali na wadhifa huo ndani ya UWT, Asha Bakari Makame ameshawahi kuwa Waziri wa Wanawake na Watoto katika serikali ya awamu ya tano visiwani Zanzibar iliyokuwa chini ya Rais Salmin Amour.

Mbali na wadhifa huo, mwanasiasa huyo ameshawahi kuwa mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

View attachment 318124

Huyu mama nakumbuka alitoa lugha chafu sana wakati ule wa Bunge Maalumu la Katiba.

Mungu amuweke pale anapostahili!
 
View attachment 317991

Aliyewai kuwa Mwakilishi wa bunge maalum la katiba na Waziri wa wanawake na watoto Zanzibar na Makamu wa Jumuiya ya wanawake wa CCM ametangulia mbele ya haki huko Dubai baada ya kurejea matibabu yake huko India.

Mwenyeenzi Mungu amsamehe makosa yake na amlaze mahali pema. Amin
Aende kwa Bwana Yesu akajibu huu upumbafu wake aliowafanyia Wa ZnZ
 
Back
Top Bottom