chrissleon
Senior Member
- Jul 22, 2015
- 147
- 89
Mkuu haututakii mema, yani upo tayali kabisa kututoa ndugu zako kafara kwa Al-shababi? tena wengine wakiangalia sura zetu ni kisu tu moja kwa moja hawata kuwa na haja ya kuuliza majina au kuleta Quran ili kujua kama si waislam. (kiuhalisia kenya kiusalama ni hatari na umakini unahitajika katika vyombo vyao vya usalama hasa kwa watu muhimu kwa Taifa kama madaktari, swala la usalama si kwamakundi ya kigaidi tu ila hata wenyewe kwa wenyewe hasa kipindi hichi kenya inapoelikea kwenye uchaguzi mkuu maana kenya wasipokuwa makini katika hili wanaweza wakasababisha matatizo ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili).Dr changamkia fursaa
ila hili swala serikali haikupaswa kukurupuka najua kuna kiasi ambacho serikali huwa kina ingiza kila wanapo toa wataalamu wake kwenda kusaidia sehemu mbalimbali ila jambo hili Muheshimiwa hakupaswa kulitolea maamuzi, badala yake angeliacha chini ya wizara husika na baraza la madaktari. kwa mambo kama haya ndio tunapo ona madhala ya siasa inapo ingizwa kwenye mambo ya kitaaluma.