Tanzania ya VIWANDA: Tuko wapi,tunaenda wapi na tutafikaje??

Kuhusu suala la skilled labour kama ilivyosemwa na msemaji hapo juu sio kweli kwamba hakuna skilled labour, wapo wengi sana.

Kuna fani chache sana oil, gas and mineral processing ndio wapo wachache the rest of the skills wapo, fanya research yako vizuri utaona.

Mwaka mmoja baadae, World Bank inasema Tanzania haina skilled labor.

Ni kujidanganya kuamini Tanzania ina skilled labor
 
Tunatoka katika KILIMO KWANZA japo bado hatujafanikiwa sana, Tunaelekea TANZANIA YA VIWANDA.

Hii ni kitu ninayoiunga mkono 100%. Ni aibu kuimport nguo za mitumba,stick,maziwa ya unga, vyuma,Furniture, na bidhaa kibao huku tuna rasilimali watu,chuma (madini,), makaa ya mawe, mazao ya kilimo na vitu vingi ya kututoa huko.

Unadhani Rais JPM afanye nini ili Mapinduzi ya Viwanda Tanzania yawe halisi. Je unaona spidi hii iko sawa?Watu wamjiandaa kufungua viwanda hata vidogo?Je watu wako tayari kununua bidhaa za ndani? Miundo mbinu na masoko yanaandaliwa kwa kasi inayotakiwa?

unaweza ongeza thamani kwa taifa kwa kutoa suluisho au nini kifanyike ili mpando hii uwe halisi kwa kila mtanzania.

Kwanza rais angeunda tume au chombo kitakachofanya utafiti wa kina na kubainisha ni jinsi gani nchi yetu inaweza kuingia kwenye uchumi wa viwanda. Tume au chombo kije na majibu sahihi katika kila kona na namna ya kusaidia, kuhamasisha, kuboresha na kulinda uchumi wa viwanda..tusikurupuke tu kama alivyofanya Nyerere, alikuwa na mawazo mazuri lakini hakujua jinsi ya kutekeleza kwa vitendo, matokeo yake alikwama na kishia kuendesha viwanda na mashirika siyo kibiashara bali kwa ruzuku toka serikalini.
 
Back
Top Bottom