Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Pole sana mleta mada.
Umeamua kuja kujifariji hapa JF.
Zama za Magufuli zilishakwisha, na Magufuli hayupo tena, ni mfu.

Usilazimishe mambo, soma alama za nyakati, wewe jua tu mtawala wa sasa ni mama Samia Suluhu. Ndio rais wa sasa, tutake au tusitake tutaucheza muziki wake.
Mbona unasema ninachosema mimi; au labda kimekuchanganya kichwa cha habari?
 
Nakukumbusha hapa kuwa hata magu tilimtaka asifanye ya JK, huku tukimmwagia sifa kedekede
Watajifanya hawalielewi hilo bandiko wako bize na kumshauri mh. Rais Samia suluhu Hassan
 
MwanaKijiji anatuambia Malkia Elizabeth akifa UK wakawa na Mfalme Charles eti itakuwa UK ya Elizabeth! Ndugu yangu Leo sijui kaamkia wapi. Enzi huisha na mpya huingia. Sasa ni enzi za Samia. She has her own agenda.
 
Unatakiwa kuonesha "upumbavu" wangu; ila sijawahi kujali "kuvunjiwa" heshima. Inabidi unioneshe werevu wako ili nikupe heshima unayostahili.
Upumbavu wako ni pale unalazimisha watu wampinge samia ata kama kafanya jambo jema . Upinzani upo kwajili ya kukosoa pale penye makosa na kama pana mazuri wanaunga mkono pia upumbavu wako mwingne rais ni wa wananch wote co wa chama wew ulizoea jpm alivokua mchama ukaisi ni sahihi rais hatakiwi kuwa upande wowote ktk utendaj wake na wananch tunamuona ni rais wetu wote
 
Tatizo ni njaa
Watu wameumizwa sana kipindi cha JPM, kila mtu mzima anaelewa hili, si wafanyabiashara, si wafanyakazi wa serikalini,si wa sekta binafsi, si NGOs, si wawekezaje, si wapinzani, kila kundi liliguswa mpaka viongozi wa dini wameonja joto la Jiwe. Asililimia kubwa ya watanzania wameambulia maumivu ya kutosha. Ni the elites wachache tu ndo wamekula shushu mwanzo mwisho wa utawala wake mpaka mauti yalipomkuta. We need reconciliation na hiki ndicho kilio cha Mama Samia. We need to come together, forget the past and move forward. Yeyote anayepingana na hili ni mchumia tumbo na lengo lake ni kusabogate juhudi za mama Samia za kuliunganisha tena taifa lililogawanyika. Hatuwezi kuwavumilia tena nyie pro Magufuli, muda wenu umekwisha, kaeni pembeni.
 
Mkuu hii ndio makala yenyewe au ni sehemu ya makala? Angalau kwa hotuba ya leo SSH sio JPM hata kwenye matamshi mfano tutaongeza wigo,tu(ni)
Ni kweli SSH ni ccm kama alivokuwa JPM ila kumsifia leo haimaanishi hatokosolewa kesho!
ni utangulizi tu; wa makala kadhaa zijazo. Lakini tatizo siyo kumsifia; ni kumfikiria. Kuna watu wanamfikiria na kutaka awe tofauti na ajenda iliyomuingiza madarakani. Ni kuwa wapo wanaotaka angeingia madarakani bila ya Magufuli na kuwa aionee aibu na kuikana ajenda "yao". Ndio lengo la kuwakumbusha watu tu.
 
Mbona sijasema hivyo; siwezi kuthubutu kusema hivyo.

..mbona hukuwahi kusema kwamba " Tanzania ya Magufuli bado ni ya Kikwete..."?

..Kuna ugumu gani kwako kuitambua awamu hii, na serikali yake, kuwa ni ya Mama Samia Hassan Suluhu?

..Ulivyoandika ni kama vile Uraisi wa Samia Suluhu Hassan, siyo kamili, bali ni Uraisi wa ubia na mtangulizi wake.
 
Sasa kama Tanzania ya Samia ni ya Magufuli, sisi tufanyeje?

Mbona nyie watu wa CCM na hasa chawa wa The late Magu mnajishtukia sana? Shida ni nini?

Kubalini mambo yamebadilika, mkiweza hamishieni tu pambio kwa Bi. Mdashi.

Kakoko si aliteuliwa na Magu, hata kwenye ubadhirifu wa mwaka jana kwenye report ya CAG ilionekana? Alichukuliwa hatua gani? Huyu Jaffo si muda wote akiwa kwenye maziara kila baada ya maneno 10 anataja Magufuli!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Wanajaribu kujifariji baada ya mshituko na mfadhaiko sababu hata wao hawajui hali itakuwaje huko mbele, lakini wajue kuwa huyo mama ni Mzanzibar na mwislam safi hatakubali michezo yao, na pia atatumia nafasi hii kuonyesha kuwa mwanamke anaweza.
 
Mimi nilichofurahi maneno ya kunya yatapungua tu.

Huko kwingine sitegemei mabadiliko makubwa, lakini yale maneno ya kunya kutoka kwa rais wa Tanzania kupungua tu ni jambo la kushukuru kwangu binafsi.

Not that niliombea Magufuli afe ili mqneno ya kunya yaishe. Ila maadam lishatokea lililotokea, naangalia upande mzuri wa matokeo ni kwamba maneno ya kunya yale ya "si mbaki na mavi yenu tumboni majumbani kwenu" yatapungua.

Zaidi ya hapo, napenda kujadili hoja na sera zaidi ya kujadili watu.
 
Wanajaribu kujifariji baada ya mshituko na mfadhaiko sababu hata wao hawajui hali itakuwaje huko mbele, lakini wajue kuwa huyo mama ni Mzanzibar na mwislam safi hatakubali michezo yao, na pia atatumia nafasi hii kuonyesha kuwa mwanamke anaweza.

..binafsi nitamkubali Mama Samia Hassan kama akiweza kukomesha dhuluma, unyama, na ukatili, wa genge la WASIOJULIKANA.
 
Mimi nilichofurahi maneno ya kunya yatapungua tu.

Huko kwingine sitegemei mabadiliko makubwa, lakini yale maneno ya kunya kutoka kwa rais wa Tanzania kupungua tu ni jambo la kushukuru kwangu binafsi.

Not that niliombea Magufuli afe ili mqneno ya kunya yaishe. Ila maadam lishatokea lililotokea, naangalia upande mzuri wa matokeo ni kwamba maneno ya kunya yale ya "si mbaki na mavi yenu tumboni majumbani kwenu" yatapungua.

Zaidi ya hapo, napenda kujadili hoja na sera zaidi ya kujadili watu.
Sawasawa; na nadhani (niseme najua) kuna watu ambao walipenda ajenda ya Magufuli ili hawakupenda jinsi alivyokuwa anaiendesha maana ni kama alikuwa anajigongelea misumari miguuni huku akijaribu kukimbia...
 
Tatizo lako unadhani Magufuli alichukiwa na wapinzani pekee. Na usijitoe ufahamu kuwa Magufuli alilazimishwa tu kuwa na Mama Samia kama mgombea mwenza na hatimaye Makamu wake.

Najua unajua vema nini Magufuli alimfanyia Mama Samia kwa kumtumia Makonda 2016. Ndo maana narudia: usijitoe ufahamu.

Magufuli alituongopea kuwa ATCL ilikuwa inapata faida, leo Mama Samia hana hata wiki Ikulu kawezesha ukweli kuwekwa hadharani kuwa bombadia zimeleta hasara mfululizo kwa miaka mitano. Na tumeambiwa kwa mara ya kwanza kuwa ATCL imetengeneza hasara ya bilioni 60.

Lakini Mama Samia amekwenda mbali zaidi. Amemtimua mtu wa Magufuli pale bandarini.

Najua huu ni wakati mgumu kwa mliojikomba kwa Magufuli na hamna njia zaidi ya kujitoa ufahamu kuwa mtaendelea kuonekana wa maana. Hizi ni zama mpya. Zenu zimekuwa rasmi na kuzikwa Chato. Poleni
 
..binafsi nitamkubali Mama Samia Hassan kama akiweza kukomesha dhuluma, unyama, na ukatili, wa genge la WASIOJULIKANA.
mbona hawa "hawakuanza" wakati wa Magufuli; na sidhani kama kuna serikali duniani imefanikiwa kuwaondoa hawa... wengine imechukua miongo kadhaa kuwafikia (rejea mfano wa Cambodia na Chile)...
 
Back
Top Bottom