Mwalimu JK Nyerere alikuwa ni wa jinsia ipi kweli, ufumbuzi wa tatizo la rushwa mnalo nyie wenyewe wa TZ, achaneni na ushabiki wa kisiasa.:yuck: especially namba 1 ni Mama wa mafisadi na wala rushwa wote
Jee kama tunataka kupambana na rushwa tunawachague wakuu wa nchi kuwa wanawake. Kwani wanawake wanahistoria ndogo ya ufisadi nchini
nafasi nyeti za kupambana na wahalifu pamoja na rushwa tuwape wanawake walete mageuzi
Bila shaka wewe huwafahamu kabisa wanawake. Tena ni vyema ungeelewa tu kuwa moja ya vichocheo vikubwa sana vya wanaume kuwa mafisadi ni katika harakati za kuwakosha wanawake (ambao WENGI WAO hupenda matanuzi mazito bila kutaka kufahamishwa senti zimetoka wapi-kula bila kuwajibika). :wink1:
Lakini cha muhimu sana ni kwamba rushwa si suala la jinsia au kigezo chochote cha aina ya watu (demography). Ni suala zaidi la mfumo wa uongozi na utawala wa nchi. Bila wananchi kuwa na msukumo wa uhakika kupinga rushwa na kuuadhibu bila kuuonea haya uongozi unaoendekeza ufisadi badala ya kuuzawadia, mtaendelea kuliwa tu hata muweke madarakani vijana, vikongwe, watoto, maalbino, wenye chongo, waandikia mkono wa shoto, n.k. Hamtakuwa tofauti na waendao kutafuta majawabu ya maisha kwa wapiga ramli.
Tuangalie vizuri ama sivyo rushwa inaweza kuwa dini mbadala hapa Tanzania.Baadhi ya watanzania wanaamni na kuitumikia rushwa utadhani ni dini yao. Hii ni mifano michache inothibitisha hoja hii.
Ukipata kazi au cheo mahali penye uwezekano wa kupata fedha haramu watu watakupongeza na kusema UMEULA! Ikiwa katika kazi hiyohiyo wewe unakuwa masikini lakini wengine wanatajirika watasema wewe ni MZEMBE yaani hujui kula. Ndivyo baadhi yawatu wanavyoamini.
Watu wengi wanapenda kazi za masilahi kwa maana kuwa zina nafasi ya rushwa. Hata baadhi ya viongozi wa dini wanawapendelea vizito au vigogo kuliko waumini masikini yaani wanahusudu mali zao japo wanaweza kuwa na mashaka au la kuwa si za halali. Wananchi wanadai bayana kupewa chochote na watangaza nia na kama mtangaza nia ni mgumu kutoa kidogo watamtolea nje. Hii ni imani ya baadhi ya watu.
Watu wengi wanatafuta vyeo vyenye maslahi si kwa ajili ya kutoa utumishi bali kujineemesha. Kwa ujumla matendo haya yamejengeka miongoni mwa watu kadhaa na kuonekana kama imani yao.
Sasa tunaweza kujiuliza swali dogo tu; hivi kweli wote HAWA WANAOOMBA KUCHAGULIWA NIA YAO YA DHATI NI KUITUMIKIA NCHI NA WATU WAKE AU WANATAAWALIWA NA IMANI KUWA WAKIPATA UONGOZI WATAKUWA WAMEULA? JE, KUNA NINI KINAWAKERA AMBACHO WANADHANI WAKIPATA UONGOZI AU CHEO WATAKIONDOA?
Katika imani hii watanzania wanaohusika wamekuzifumbia dini zao macho. Yaani wamevaa ngozi za konndoo kumbe ndani ni mbwa mwitu sorry for that word! Hawa hutoa sadaka nono na kujifanya wako mstari ea mbele katika dini zao. OLE WAO TUMESHAWANGAMUA
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.