laki si pesa.
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 10,003
- 9,754
Sijakuelewa kwa hiyo unakubaliana na ndoto ya Lema?
Kweli inatisha! Kitwanga neno likatimia, RC akaambiwa na neno likatimia. Sasa hatutaki kuamini mpaka litimie?Naona umeogopa kuweka na ile ndoto(Maono) ambayo Lema aliiona.
Kumbuka pia, Lema naye amejariwa kipawa hicho cha kuona mbali, ipo mifano miwili mikubwa alisema 'Ameota' na baada ya muda ikatokea kweli. Alisema kuhusu Kutumbuliwa Kwa Kitwanga, na pia kutumbuliwa kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Uzuri mmoja wa 'ndoto' za Lema huwa zinakupa tahadhali ili muhusika ajirekebishe kabla hazijatokea.
Wanabodi,
Declaration of interest. Mimi ni mwandishi wa kujitegemea, kule newsroom tunaitwa freelance lakini sasa wanatuita wapiga dili za habari!, na kufuatia ukame wa habari, tumepigika kweli kweli hadi tunatunga habari za mayalla (njaa)!.
Kufuatia kupigika sana Januari hii, Usingizi ulinikatikia usiku manane, nimegala gala wee mwisho nimeshuka JF ndio nikakutana na topic iliyonifanya kupandisha uzi huu.
Kiukweli kabisa Tanzania hapa tulipo sipo, tunahitaji nguvu ya Mungu kuweza kutoka,na kufika kule tunakotaka, ndio maana mara kwa mara mnamsikia rais wetu mpendwa Dr.John Pombe Magufuli akituomba Watanzania tumuombee, kuashiria anahitaji nguvu za Mungu ili kuweza kuishinda vita iliyo mbele yake.
Awamu ya Tano ilipoanza kwa kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tuu" ikaanza kwa Mhimili wa Serikali kuisigina katiba, mihimili ya Bunge na Mahakama yenye the role of Checks and Balances under the principle of "the separationseparation of powers" imekaa kimya!. Ukaja mhimili wa Bunge ulioridhia ile "Open Goverment Initiative" badala ya kufanya kazi kwa uwazi, sasa Bunge linaendeshwa behind the closed doors kwa kuzuia matangazo ya moja kwa moja, na kupitisha miswada ya muhimu kwa mtindo wa "fast track" kwenye kutimiza hapa kazi tuu.
Baada ya mhimili wa serikali kufanya mambo ya kiimla, sasa ni zamu ya Mhimili wa Mahakama tukishuhudia danadana ya kuchezea haki ya mtu, ambayo imetolewa kama right na katiba lakini sasa mahakama inaifanya ni favour!, jana mahakama imeanza kutoa hukumu za fasta fasta za "hapa kazi tuu" kwa kuanza na Kilombero, Lema wa Arusha anafuatia kwa kosa la kuota ndoto na kuisema!.
Mhimili wa Serikali utanyamaza na mhimili wa Bunge utanyamaza!. Where is the doctrine of separation of powers?!, where is the checks and balance?. Who will check who na bila kuwepo balance mambo si yatakuwa vululu vululu na vurugu mechi kwa jahazi letu kwenda mrama huku likinesa nesa, jee hatuna hatari kweli ya kupinduka au kuzama kabisa huko mbele ya safari?!.
Ukijumlisha na huu ukata wa fedha mtaani, maisha ni shida juu ya shida, dhiki juu ya dhiki, na taabu juu ya taabu kwa watu wa chini!, ukijumlisha na hili tishio la baa la njaa linalonukia, japo wenyewe wanakanusha ila kama kweli kuna njaa, then soon ukweli utadhihiri!.
Hali hii imenifanya nimemkumbuka mwandishi mmoja wa vitabu aliyetumia pen name ya Prince Kangwema aliandika kuhusu "Quo VadisTanzania?". Na mimi pia ninakiri kuwa Tanzania sasa tuko kwenye situation ya "Quo Vadis Tanzania". Mungu tusaidie!.
Watu wa kulisaidia taifa hili wapo ila kama ilivyo kawaida, nabii huwa hakubaliki nyumbani, lakini humu JF, tunao manabii wetu, Tuwakubali watatusaidia.
Someni hapa kumhusu huyu jamaa.
Nimeota ndoto kuna Mbunge atakula mvua wiki ijayo
Mkuu Mzushi, kwanza Hongera, pili mimi nakuamini, na tatu nabii huwa hakubaliki nyumbani.
Kitu kikubwa kuhusu wewe ni you have the powers!
Kwa msio jua, ndoto za kweli huwa zipo na zinaitwa lucid dreams.
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, Wewe Unazo?
"Will Powers!", "Faith Healing!"-NgMiujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. -Kila Mtu Anazo!
Ndoto za kupaa na kuelea hewani zinaashiria nini?
Kuna siri gani kwenye ulimwengu wa kiroho ukilala chali?
Mambo mengi ninayo yawaza au kuyaota huwa yanatokea kweli tangu Nina mika 12 na sasa Nina mika 18.
Ndoto za kupaa na kuelea hewani zinaashiria nini?
Tusiwadharau kabisa watu kama hawa waota Naoto, hivi ni vipawa kutoka kwa Mungu, tuwatumie, tuwasikilize, watatuepushia na mengi na kulisaidia taifa kusonga mbele kwa kuisikiliza sauti ya Mungu ikileta ujumbe kupitia ndoto.
Najua kwa bandiko hili watu humu mtabeza sana kama mlivyombeza kule huyu muota ndoto, lakini ndoto yake imetimia, tutakapofika 2020 na zile ndoto za waota ndoto wengine zitakapotimia, ndipo wenye kumbukumbu watalikumbuka bandiko hili!.
Naomba msishangae kwa waota ndoto kuwa persecuted, hata Yusufu "Mzee wa Ndoto", alifungwa gerezani, kwa ajili ya ndoto tuu!, hata Shadraki, Meshaki na Abednego walifungwa gerezani kwa ajili ya ndoto!, hata wale watabiri waliposhindwa kuitafasiri ile ndoto ya Mfalme Nebukadreza ya "Mene Mene Takeli na Peresi " pia walifungwa gerezani!, hata Paulo na Sila nao walifungwa gerezani!, hadi milango ya gereza ikafunguka!, na mimi pia nina ndoto, iko siku milango ya gereza letu hili tuliomo ikafunguka na watu tutaziheshimu baadhi ya ndoto za kweli.
Paskali
Rais hawezi kushitakiwa
Maandamano ninjia pekee iliyobaki!
Aisee umeandika nilichokuwa nikikifikiria.Huyu mtu hakika nawaambieni atakuja kujiongezea miaka ya kukaa pale jengoni naona ameanza kulewa na umasikini na unyonge wa watanzania amechukulia kama mtaji.Viongozi wengi waliokatalia madarakani waliingia kwa mgongo wa umasikini na unyonge wa wananchi wa nchi wanazozitawala ni mda tu kila kitu kitakuwa wazi.
Mwaka huu lazima mtaisoma namba
Ebu funga hilo bakuli lakoHata wewe unaisoma tena wewe unaisoma ya KIRUMI.Kesho nyie ndiyo wakwanza kumtukana huyo MTUKUFU.Wanafiki wakubwa nyie
Ebu funga hilo bakuli lako
Kwa jinsi ambavyo CCM imejipanga kuua sijui inawezekanaje,maelefu watauawa.
Ndio gharama za kudai haki, ukiogopa kifo vumilia kunyanyaswa.
Sijui kinachoendelea vichwani mwa watanzania kwa sasa
Kinachoendelea ni matumaini hewa!
Kukata tamaa na kutoelewa wapi wanaelekea. Umasikini kuongezeka,akiba kukauka na maisha ya kishetani.
Mkuu unawaombea wengine matatizo!!. Unajitahidi kutafuta suluhisho kwa nguvu hiyo hiyo unayotumia kuwaombea mabaya wengine?.Tulieni kila mtu afikiwe........
Kenge uwa asikii mpaka damu itoke masikini........
Naomba kila mtu afikiwe na aguswe kabisa ili akili ziwaingie.
Wonderful,
Hii nchi inanyooshwa kwa kuvunja katiba,wanasema uchumi wa nchi unakua kasi huku imepinda.
Hii nchi iliyopinda halafu uchumi wake unakua kwa kasi na rais yupo busy kuinyoosha inatakiwa iingie kwenye maajabu ya dunia