SoC04 Tanzania tuitakayo na mfumo wa malezi katika lishe

Tanzania Tuitakayo competition threads

TUKUSWIGA MWAISUMBE

New Member
Jul 27, 2023
1
2
TANZANIA TUITAKAYO NA MFUMO WA MALEZI KATIKA LISHE

Mimi ni mwanachama wa Jamii Forums, Jina langu ni mchechemuzi.

Ushahidi wa tafiti za kisayansi umeonyesha kwamba msingi wa Taifa lolote lile unategemea sana uwekezaji kwa binadamu katika umri wa awali wa maisha ya mwanadamu hususani umri 0 -2 yaani siku 1000.

Nchini Tanzania kati ya watoto 100 wenye umri chini ya miaka 5 watoto 30 wamedumaa, mikoa ya nyanda za juu kusini inaongoza kwa kila watoto 100 kati yao 46 wamedumaa, inayoongoza kwa kilimo cha mazao ya chakula.

Takwim zinaonyesha, kwa mkoa wa Iringa pekee katika watoto 100 watoto 56 wamedumaa. ( Takwimu kwa mujibu wa NBS, 2023).

Kiwango hiki cha udumavu sugu kinatia shaka ya watoto kutowza kufikia ukuaji ulio timilifu na Taifa kuwa na mzigo mkubwa hapo baadae, hivyo endapo hatua za utafiti wa kina hazitachukuliwa kwa kipaumbele cha pekee basi itakuwa vigumu kufikia TANZANIA TUITAKAYO.

Hivyo kunahitajika kuwepo kwa Makala maalum zenye kufanya uchechemuzi kwa jamii ili kusaidia kuleta mabadiliko ya haraka katika tatizo hili sugu.

  • Kufanya utafiti wa kina kubaini eneo athirika zaidi ya tatizo hili.
  • Kufanya utafiti wa hatua ambazo zimechukuliwa katika sababu tajwa ambazo ni sugu kwenye jamii.
  • Kufanya utafiti uwepo wa mikataba ya lishe ilivyosaidia kupunguza tatizo la udumavu
  • Kuja na suluhisho la kupunguza usugu wa tatizo hili.
TAZAMA:
View: https://www.youtube.com/watch?v=BpXsTDrgp0Q&t=66s

Takwim zinaonyesha, kwa mkoa wa Iringa pekee katika watoto 100 watoto 56 wamedumaa. ( Takwimu kwa mujibu wa NBS, 2023).
Duuuh! Hatari sana tunafeli wapii?

kunahitajika kuwepo kwa Makala maalum zenye kufanya uchechemuzi kwa jamii ili kusaidia kuleta mabadiliko ya haraka katika tatizo hili sugu.

  • Kufanya utafiti wa kina kubaini eneo athirika zaidi ya tatizo hili.
  • Kufanya utafiti wa hatua ambazo zimechukuliwa katika sababu tajwa ambazo ni sugu kwenye jamii.
  • Kufanya utafiti uwepo wa mikataba ya lishe ilivyosaidia kupunguza tatizo la udumavu
  • Kuja na suluhisho la kupunguza usugu wa tatizo hili.
Yas tutafiti tujue nini kinatukwamisha?
 
Back
Top Bottom