SoC04 Tanzania Tuitakayo: Elimu ya Afya ya Akili itasaidia kupunguza matukio mengi ya uhalifu nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Xpertz

Member
May 3, 2024
10
7
UTANGULIZI
Kumeendelea kutokea matukio mengi ya uhalifu nchini Tanzania yenye viashiria vya kuwepo tatizo kubwa la afya ya akili miongoni mwa wananchi. Miongoni mwa matukio hayo ni visa vya mauaji kutokana na visa vya wivu wa mapenzi, watu kujinyonga, kujiua kwa sumu, uraibu wa kamari, ubakaji, unyanyasaji wa kingono na kijinsia pamoja na utapeli kwa njia ya mtandao. Matukio hayo yanahitaji hatua za dhati zichukuliwe ili kuyakomesha.

JE NINI KIFANYIKE?
Napendekeza elimu ya afya ya akili ipelekwe kwenye jamii katika nyanja mbalimbali ili kuwafikia wananchi wote.

1. ELIMU YA AFYA YA AKILI KWA UMMA KUHUSU MAHUSIANO NA NDOA (Ngazi ya familia)
Hii itasaidia sana kuepusha mauaji yatokanayo na wivu wa kimapenzi. Elimu ya mahusiano, haki ya kuacha, kuachwa na talaka ziwe wazi jamii ielimishwe kuepusha mauaji holela endelevu sababu ya wivu wa mapenzi nchini. Wazazi, walezi na taasisi za dini pia zipewe miongozo ya mafunzo sahihi kuhusu mahusiano na ndoa, kuachana au kuvunjika mahusiano au ndoa isiwe vita bali makubaliano.

2. ELIMU YA AFYA YA AKILI IPELEKWE KWENYE MABARAZA YA MIGOGORO YA ARDHI KATA, YABORESHWE YATUMIKE KAMA MABARAZA YA USULUHISHI NA USHAURI(Ngazi ya kata)
Kwenye kila kata nchini yale mabaraza yaliyokua yakitatua migogoro ya ardhi pekee yapewe elimu ya afya ya akili na yaongezewe wigo wa majukumu na kuwa mabaraza ya migogoro yote ambayo yatasaidia kutatua migogoro mbalimbali kwenye jamii na tutoa suluhu za haraka kuepusha uhalifu. Migogoro mingi hutokana na baadhi ya wadai au wadaiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili pia hivyo mabaraza haya yatasaidia kuchochea mabadiliko chanya

3. ELIMU YA AFYA YA AKILI NA UJASIRIAMALI IWE LAZIMA MASHULENI(Ngazi ya kitaifa)
Moja ya tatizo kubwa la afya ya akili kwa vijana ni uraibu wa kamari(Betting) na madawa ya kulevya kutokana na msongo wa mawazo kutokana na upungufu wa ajira ila elimu ya UJASIRIAMALI inaweza kutatua tatizo hili na kuokoa kundi kubwa la vijana wanaoatumbukia huko.

4. VYOMBO VYA HABARI VIWE CHACHU YA KUENEZA ELIMU YA AFYA YA AKILI KWA UMMA (Ngazi ya kitaifa na kimataifa)
Vyombo vya habari vina nafasi kubwa kutoa elimu ya afya ya akili kwenye jamii kwa kukazia vipindi na matangazo mengi yenye kuhamasisha maamuzi sahihi miongoni mwa jamii ikiwemo kuhamasisha watu kutochukua sheria mkononi, watu kuripoti matukio kwenye vyombo na mamlaka husika pamoja na kuhamasisha matumizi ya njia sahihi kutatua migogoro mbalimbali kwa kurusha vipindi vingi maalumu vyenye kuelimisha kuhusu utatuzi wa migogoro.

5. JAMII IRIPOTI WATU WENYE VIASHIRIA VYA MATATIZO YA AFYA YA AKILI KWA WAKATI(Ngazi ya jamii)
Jamii ipewe elimu kuhusu umuhimu wa kuripoti watu wote wenye viashiria vya matatizo ya afya ya akili kwa wakati kwenye mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe kuwadhibiti na kuwaokoa kabla hawajaleta madhara
 
3. ELIMU YA AFYA YA AKILI NA UJASIRIAMALI IWE LAZIMA MASHULENI(Ngazi ya kitaifa)
Moja ya tatizo kubwa la afya ya akili kwa vijana ni uraibu wa kamari(Betting) na madawa ya kulevya kutokana na msongo wa mawazo kutokana na upungufu wa ajira ila elimu ya UJASIRIAMALI inaweza kutatua tatizo hili na kuokoa kundi kubwa la vijana wanaoatumbukia huko.
Yaani kweli, tunalo ombwe kubwa la watu wanaoishi bila falsafa ya maisha yao. Falsafa ifundishwe toka watu wadogo. Maana ni vigumu sana mwenye falsafa zake kutumbukia kwenye mambo yasiyoeleweka kisa pesa tu.
4. VYOMBO VYA HABARI VIWE CHACHU YA KUENEZA ELIMU YA AFYA YA AKILI KWA UMMA (Ngazi ya kitaifa na kimataifa)
Vyombo vya habari vina nafasi kubwa kutoa elimu ya afya ya akili kwenye jamii kwa kukazia vipindi na matangazo mengi yenye kuhamasisha maamuzi sahihi miongoni mwa jamii ikiwemo kuhamasisha watu kutochukua sheria mkononi, watu kuripoti matukio kwenye vyombo na mamlaka husika pamoja na kuhamasisha matumizi ya njia sahihi kutatua migogoro mbalimbali kwa kurusha vipindi vingi maalumu vyenye kuelimisha kuhusu utatuzi wa migogoro
Na wale wanaotoa habari za kukatisha tamaa, au kupotosha jamii wafungiwe mara moja. Habari zina nafasi kubwa sana kuitengeneza jamii vile tunavyotaka iwe
 
Back
Top Bottom