Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,260
- 5,257
Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) umeibuka kuwa dhana maarufu sana Duniani, Afrika na hususani Tanzania, huku makampuni yakizidi kujishughulisha na shughuli za uhisani. Hata hivyo, Makala hii itakwenda kuonesha uhitajiwa wa mtazamo kamili zaidi wa CSR ni muhimu ili kufikia maendeleo endelevu na yenye matokeo katika jamii za Kitanzania. Huku tukiendela kuona utayari na michango, makampuni yanahitaji kupitisha mbinu ya kimkakati na shirikishi ambayo inatanguliza ushirikiano wa muda mrefu na kuwezesha jamii kujitegemea.
Picha kwa hisani ya submittable blog
Mazingira ya sasa ya CSR nchini Tanzania yana sifa ya kuzingatia afua za muda mfupi tu, kwani mara nyingi kampuni hushiriki katika michango ya mara moja, kama vile kujenga shule au kutoa vifaa vya matibabu au kutoa huduma za dharura. Ingawa vitu hivi hutoa unafuu wa muda, mara nyingi hushindwa kushughulikia sababu kuu za umaskini na maendeleo duni ya wananchi. Kwa mfano, kampuni inaweza kutoa kompyuta kwa shule, lakini bila kushughulikia ukosefu wa walimu waliofunzwa au suala la umeme wa uhakika, matokeo ya mchango huo bado ni mdogo, kwani unakuta kompyuta hizo zinaishia kukaa tu stoo na kukosa Matumizi. Kampuni hizi zitazame mbali wakiwa watakwenda kufanya CSR kwa wahusika, shule ikiwa haina umeme weka umeme wa uhakika kwanza, kisha ndo ufanye kupeleka kompyuta hizo, huku ukiwa na uhakika pia wa walimu wenye taaluma hiyo wanapatikana.
Picha kwa hisani ya Food Business Africa.
Zaidi ya hayo, mtindo wa sasa unaweza kukuza utamaduni wa utegemezi ndani ya jamii. Wakati makampuni yanakuwa chanzo pekee cha usaidizi wa mahitaji ya kimsingi, jamii hupoteza motisha ya kuendeleza suluhu zao na kujitegemea. Hii inaunda mzunguko wa utegemezi ambao unazuia maendeleo ya muda mrefu. Kwani jamii zingine zitakuwa zikisubiria tu CSR kutoka kwa Seven-Up Bottling Co maarufu kama Pepsi au Coca Cola bila kuumiza vichwa vyao kuangalia upande wa pili wa namna ya kujiendeleza zaidi kimaisha.
Ufanisi bora wa dhana hii ya CSR huanza na uelewa kamili wa mahitaji mahususi na changamoto zinazokabili jamii lengwa, huwezi kupekeleka msaada wa nyama ya nguruwe kwa wahanga wa mafuriko katika jamii ya watu wenye Imani ya kiislamu. Makampuni yanapaswa kushiriki katika tathmini ya mahitaji shirikishi, ikihusisha wanajamii katika kutambua vipaumbele vyao muhimu zaidi, jamii iwe mstari wa mbele kuainisha mahitaji ambayo wanaona ya umuhimu zaidi kuliko mengine. Mbinu hii shirikishi inahakikisha kwamba mipango ya CSR inashughulikia mahitaji ya kweli na kuwa na matokeo ya kudumu sio kupeleka mahitaji ya muda mfupi ambayo yatachukua muda mchache na jamii kuanza tena kupata taabu.
Picha kwa hisani ya SBC.
Harakati na juhudi zozote za CSR zinapaswa kuundwa kwa kutazama athari za muda mrefu, huku wakilenga zaidi kukua au kukuza dhana ya kujitegemea ndani ya jamii. Hii inaweza kufanikiwa endapo wakiangalia na kuzingatia mipango ya kujenga uwezo wa jamii husika. Kwa mfano, kampuni inaweza kushirikiana na taasisi za ndani za kilimo kutoa mafunzo juu ya mbinu endelevu za kilimo au kutoa mikopo midogo midogo ili kuwawezesha wanajamii kuanzisha biashara ndogo ndogo, ambazo zinaweza kuwafanya wakawa na kipato endelevu. Juhudi hizi huzipati jamii ujuzi na rasilimali zinazohitajika ili kujitegemea kwa muda mrefu, ili hata Wakati kampuni fulani inapokoma kufanya shughuli zake eneo hilo basi wanakuwa wameacha alama ya milele.
Picha kwa hisani ya Art in Tanzania Blog.
Ushirikiano baina ya makampuni na jamii ndo nguzo kuu ya ufanisi wa CSR, umuhimu wa ushiriki kati ya makampuni, mashirika ya serikali, NGOs, na jamii kwa ujumla ni suala lisilopingika endpao lengo lilikiwa ni kuifanya jamii ipige hatua katika harakati zake za kimaisha. Kwa kuunganisha rasilimali na utaalamu, washikadau wanaweza kutengeneza suluhu za kina ambazo zitaelekezwa moja kwa moja katika kushughulikia changamoto nyingi zinazokabili jamii. Kwa mfano, kampuni inaweza kushirikiana na Malamka za Maji mathalani NGO yenye uzoefu katika usimamizi wa rasilimali za maji ili kuendeleza mradi endelevu wa miundombinu ya maji kwa kijiji cha vijijini. Kwa kufanya hivi wanaweza kusaidia jitihada za serikali katika kutengeneza miundombinu ya maji haswa maeneo ya vijijini.

Mfano bora kabisa ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Kwa kutambua umuhimu wa usalama wa maji kwa jamii, TBL imeshirikiana na serikali za mitaa na mashirika yasiyo ya kiserikali kutekeleza programu za usimamizi wa rasilimali za maji. Programu hizi sio tu zinatoa upatikanaji wa maji safi lakini pia hufundisha jamii juu ya mazoea ya kuhifadhi maji. Mpango huu ni mfano wa CSR ambao unapita zaidi ya suluhu za muda mfupi na kukuza uendelevu wa muda mrefu. TBL wametengeneza jina lao na kujenga umainifu mkubwa kwa wananchi hususani Kanda ya Ziwa ambao ni wateja wa kudumu wa vinywaji kama Castle Lager, Castle Lite, Kilimanjaro Lager, Eagle, Balimi, Ndovu Special Malt, Safari Lager, Castle Milk Stout na zingine ambazo zimepata wapenzi wengi Tanzania.
Picha kwa hisani ya Dar24.
Kwa kukumbatia maono haya mapya ya CSR, makampuni yanaweza kuunda hali ya ushindani imara ambapo jamii itajenga mahaba katika bidhaa au huduma kutoka makampuni husika. Jamii hunufaika kutokana na mipango ya maendeleo endelevu inayoziwezesha kujitegemea ila sio ile ya muda mfupi. Kampuni mengi Tanzania yatumie CSR, kwa upande chanya, ili wadumishe nia njema, kuongeza sifa ya chapa, na uwezekano wa kupata wafanyakazi wenye ujuzi na utulivu kutoka kwa jamii zinazostawi. Jamii imepata kunufaika sana kwa kazi inayofanywa na Benki ya MIB, kampuni ya Saruji ya Twiga Cement pamoja na Coca-Cola. Miradi ya CSR ni sehemu ya faida kubwa kwa nchi na jamii ambayo ipo tayari kuipokea vyema, CSR ni muhimu zaidi kwa Tanzania, kwa sababu CSR ni sehemu pekee bora ambayo kampuni zinaweza kujenga urafiki endelevu na jamii huku wakihakikisha kuwa Tanzania inadumisha rasilimali zake muhimu.
Picha kwa hisani ya csr ready.
Kwa kumalizia, mazingira ya sasa ya CSR nchini Tanzania yanahitaji mabadiliko ya kimtazamo kwa ukubwa sana. Kampuni zinahitaji kupitisha mbinu kamili ambayo inatanguliza ushirikiano, uendelevu, na uwezeshaji wa jamii, huku wakiruhusu mawazo bora kutoka kwa kampuni ambazo zinafanya vizuri katika CSR, wasione aibu au uhasama kuuliza na kuomba msaada wa mawazo wa namna CSR bora na endelevu inavyofanyika. Mbinu hii ya kimkakati kwa CSR ina uwezo wa kufungua mabadiliko chanya ya muda mrefu na chanya katika jamii za Kitanzania, kuweka njia kwa mustakabali wenye mafanikio na usawa kwa wanajamii wote.